Black Jesus (Based on true story)

Late 70s and early 80. Tulihamia Sumbawanga 1979 mitaa ya regional block. Mkuu wa mkoa alikuwa anaitwa baruti. Hakukaa hapo anapokaa mkuu wa mkoa wa sasa. Ikulu ilikuwa pale mpango kabambe wa maji lea Mbele. Tulihamia wakati wa mvua ilikuwa balaa. Mkurugenzi wa mkoa alikuwa Masinde. Afisa elimu Mbeyela, mkewe alitufundisha English Jangwani primary school std 3. Kichaa tuliyemkuta aliitwa Checheche. Alikuwa anatembea naked dudu hilooo. Nilianza std 1 hapo Jangwani primary school. Ndugu zangu wote na walisoma Sumbawanga primary school, mama yetu na yeye alifundisha hapo hapo swanga primary school. Katandala ilikuwa almost pori tupu nyumba chache sana tena za nyasi. Sumbawanga ni mabingwa wa kukamata Nswa yaani kumbi kumbi. Ile mitego kwenye vichuguu ni balaa. Tulikula sana migagi hahaha wafipa tu wanaijua hii. Tajiri alikuwa bhojak, lkn wakati Ile bidhaa hazikuwepo madukani. Game la Sumbawanga primary na Mazwi primary ilikuwa km simba na Yanga. Always Mazwi ilipigwa bao. Askofu katoliki alikuwa Kalolo msakila alikuwa hapendi mzaha. Naikumbuka maktaba pale karibu na kanisa katoliki, ilipoanza tulikuwa hatukosi mimi na kaka yangu, tukawa wanachama, nilijifunzia hapo kusoma vitabu. Kakanyangu akiwa la nne nipo la pili vitabu km kambi ya Makava, riwaya za Willy Gamba, kuna vitabu vya ki Russia wakati you Urusi. Kabla ya Mandela mbele yake kulikuwa na uwanja wa mwanzo km unaelekea Swanga Wenyeji. Wakati wa power mabula anakuja, tunatoka regional block hadi kule. Timu kubwa kulikuwa na RTC na Ujenzi, RTC always wakiichapa Ujenzi. RTC walikuwa na jamaa anaitwa mpambwe alikuwa anapiga mashuti balaa. Simba walitaka wamchukue sijui Ikawaje. Ilipojengwa ikulu mpya akaja na mkuu wa mkoa mpya aliitwa Mnyawami. Basi mtoto wake alikuwa kanizidi darasa moja. Basi tulikuwa na timu yetu uwanja ndani ya ikulu. Katandala tulikuwa tunawapiga bao. Swanga ipo siku ntatia maguu tena. Izia bangwe, kizwite, chanji, regina Mundi.
Migagi na Inswa mkuu umenikubusha mbali Sana. Barikiwa
 
Huyu jamaa mleta mada (story) tangu Alhamisi iliyopita hajakanyaga jf. Kumbe pia ni mtumoshi wa kile chama cha kijini. Green network.
Screenshot_20180506-122757.jpeg
Screenshot_20180506-122748.jpeg
 

Similar Discussions

21 Reactions
Reply
Back
Top Bottom