Tuna mazoea ya kufanya mambo bila kujiuliza sababu ya kuyafanya,lakini hatuna mazoea ya kujiuliza ni kwanini tuna hayo mazoea ya kufanya hayo mambo bila ya kujiuliza wakati tuna akili timamu
Tangu nikue huwa naona watu wakisherehekea siku zao za kuzaliwa na hata hapa kuna "nyuzi' nyingi tu huwekwa kwa minajili hiyo ya kupongezana
Siku ya kuzaliwa inamaana kuwa miaka yako imeongezeka na hiyo inamaana pia kuwa unaendelea kuzeeka na hiyo inamaana kuwa unakikaribia kifo
Hivi ni kweli tunafurahia kukaribia kufa?
Kama ni ndio kwanini tunalia na kusikitika msibani?
Sidhani kama mtu akiambiwa kuwa wiki ijayo siku kama ya leo atakufa hala fu siku moja kabla ya kuifikia leo ni siku yake ya kuzaliwa,sidhani kama huyo mtu atachekelea tena siku yake ya kuzaliwa
Tofauti na hiyo,hivi siku yakuzaliwa ni siku gani hadi tuisherehekee na kupongezana?
Kuna kitu gani hasa cha kusherehekea?
Kuna jambo gani hasa la kufurahia?
Inawezekana kuwa mtu kuzaliwa ni furaha,lakini ni furaha kwenye kitu gani hasa?
Hivi kuzaliwa ni kitu cha ajabu hadi ifikie ikifika hiyo siku uanze kuwachangisha watu na kukopa ili tu ufanye sherehe za kukumbuka kuzaliwa?
Mnaweza kunipa sababu za msingi hadi na mimi niiweke hiyo siku kwenye ratiba zangu za kusheherekewa?
Tafadhali sitaki sababu za kimazoea!