Birthdays ............!!!!!!!!!!!!!!!

Birthdays ............!!!!!!!!!!!!!!!

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,920
Tuna mazoea ya kufanya mambo bila kujiuliza sababu ya kuyafanya,lakini hatuna mazoea ya kujiuliza ni kwanini tuna hayo mazoea ya kufanya hayo mambo bila ya kujiuliza wakati tuna akili timamu

Tangu nikue huwa naona watu wakisherehekea siku zao za kuzaliwa na hata hapa kuna "nyuzi' nyingi tu huwekwa kwa minajili hiyo ya kupongezana

Siku ya kuzaliwa inamaana kuwa miaka yako imeongezeka na hiyo inamaana pia kuwa unaendelea kuzeeka na hiyo inamaana kuwa unakikaribia kifo

Hivi ni kweli tunafurahia kukaribia kufa?
Kama ni ndio kwanini tunalia na kusikitika msibani?

Sidhani kama mtu akiambiwa kuwa wiki ijayo siku kama ya leo atakufa hala fu siku moja kabla ya kuifikia leo ni siku yake ya kuzaliwa,sidhani kama huyo mtu atachekelea tena siku yake ya kuzaliwa

Tofauti na hiyo,hivi siku yakuzaliwa ni siku gani hadi tuisherehekee na kupongezana?
Kuna kitu gani hasa cha kusherehekea?
Kuna jambo gani hasa la kufurahia?

Inawezekana kuwa mtu kuzaliwa ni furaha,lakini ni furaha kwenye kitu gani hasa?
Hivi kuzaliwa ni kitu cha ajabu hadi ifikie ikifika hiyo siku uanze kuwachangisha watu na kukopa ili tu ufanye sherehe za kukumbuka kuzaliwa?

Mnaweza kunipa sababu za msingi hadi na mimi niiweke hiyo siku kwenye ratiba zangu za kusheherekewa?
Tafadhali sitaki sababu za kimazoea!
 
Wanaochangisha watu kwaajili ya birthday zao ni washamba, sio lazima ukusanye watu kama huna uwezo unaweza ku- celebrate na familia. To me birthday ni wakati wa kumshukuru Mungu kwa kuendelea kunipa hii oxygen bure na pia ku-reflect malengo niliyojiwekea. Kufa tutakufa tu hata usiposheherekea siku yako ya kuzaliwa
 
Kabla ya maendeleo ya sayansi kuzaa kuliua 30% ya kina wazazi, kuzaliwa kuliua 20% ya watoto kufika miaka 5 kuliua 20% ya waliobaki, kufika miaka 10 kuliua 10% ya waliobaki tena. Afrika ukifika miaka 35 asilimia >60 ya watu wa umri wako wamekufa.
Hapo ndio umuhimu ulipoonekana.
 
Kuna kuadhimisha na kusherehekea..
Ninavyofahamu kuadhimisha ni kukumbuka tukio flani lililokugusa.
Kimsingi tukio la kuzaliwa ni kubwa kwa sababu its just happen once na lina quencequences nyingi..
Kwa hivo kuwa na kawaida ya kukumbuka tukio hilo ni jambo zuri tu..
Binafsi huwa naadhimisha na sisherehekei siku yangu ya kuzaliwa..
 
Hujajibu ni kivipi ufurahie kulisogelea kaburi!
 
Umuhimu wa nini ulipoonekana?
Au umuhimu wa kusherehekea kulisogelea kaburi?
 
Hujanipa sababu za msingi wa kusherehekea au kuadhimisha hilo
Niambie ni kitu gani kinakufanya uadhimishe na sio kusherehekea!
 
Soma tena post yangu ya mwanzo utaona kwa nini naadhimisha siku ya kuzaliwa..
Unaposema 'birthdays' ni kusogelea kifo huu ni mtazamo wako ambao ambao umeamua kuuchukua..
Kimsingi siku ulipozaliwa ndio siku ulipoumbiwa kifo..hivyo dhana ya kuogopa kifo sidhani kama inamashiko..

Hujanipa sababu za msingi wa kusherehekea au kuadhimisha hilo
Niambie ni kitu gani kinakufanya uadhimishe na sio kusherehekea!
 
haina maana sana kusheherekea na me nilikuwa najiuliza wa kusheherekea ni wewe au mama yako aliyekuona na uliyemuumiza wakati wakujifungua? kwa sababu tunafurahia kiitu mabacho ukijui wala hujui kilitokea nini? ni mtazamo wangu tu....
 
mimi huwa sina furaha kwenye birthdays zangu, natamani zisifike maana nakuwa namuwaza sana mama yangu.
 
Soma tena post yangu ya mwanzo utaona kwa nini naadhimisha siku ya kuzaliwa..
Nimesoma na hakuna mahali uliponipa sababu
Umeishia kusema "Kimsingi tukio la kuzaliwa ni kubwa kwa sababu its just happen once na lina quencequences nyingi.."
bila hata kusema hizo quencequences ni nini na zipi
Au kusema tu hivyo ndio unakuwa umesema sababu?
Unaposema 'birthdays' ni kusogelea kifo huu ni mtazamo wako ambao ambao umeamua kuuchukua..
Sio kweli hata kidogo
Wewe umeamua kuukataa mtazamo wangu bila kuniambia mtazamo sahihi ni upi na kwanini

Kwa mujibu wa kamusi yangu ni kuwa ukweli ni kile kinachosemwa kukubaliana na hali halisi,sasa mimi nimesema kufikia siku yako ya kuzaliwa kuna maana kuwa unazidi kuongeza umri wako na unazidi kulisogelea kaburi yaani siku yako ya kufa

Sasa nakuuliza,je hayo maelezo yangu sio kweli au ni kweli kwa mujibu wa tafsiri yangu ya ukweli?
Je kiuhalisia sio kweli kuifikia siku yako ya kuzaliwa sio kuzeeka?
Je kuzeeka hakuna maana ya kulisogelea kaburi?
Kimsingi siku ulipozaliwa ndio siku ulipoumbiwa kifo..
Kivipi?
Hata kama ni hivyo kuna uhusiano gani na kuadhimisha siku yako ya kuzaliwa?
hivyo dhana ya kuogopa kifo sidhani kama inamashiko..
Ni wapi mimi nimesema kuhusiana na kuogopa kifo?
Mini nimesema kuwa hakuna anaefurahia kifo

Au kutokufurahia kuna maana ya kuogopa?

Tafadhali nipe sababu za kuadhimisha siku ya kuzaliwa kama ulivyosema!
 
Umuhimu wa nini ulipoonekana?
Au umuhimu wa kusherehekea kulisogelea kaburi?
Just be positive minded,,,kufa kupo tu....nadhani kusingekua na maendeleo kama watu wangekuwa wanafikiria afterall tutakufa tu...unajua umuhimu wa furaha hata kama ni ya muda mfupi?..UNAJUA KITU KINAITWA UTILITY?...ITS ALL ABOUT BEING HAPPY,,FOR YOUR SELF BEING AS WELL AS OTHERS..tukuanza kufikiria kufakufa tu,ndio misongo ya mawazo yenyewe hiyo,,,
 
Umuhimu wa nini ulipoonekana?
Au umuhimu wa kusherehekea kulisogelea kaburi?

kifo kipo na kila mtu lazima aonje mauti, umuhimu wa kusherehekea unakuja pale mtu anakua amekwepa vikwazo vingi ambavyo kwa namna moja au nyingine vingeweza kupelekea kulisogelea kaburi mapema zaidi.
 
Soma tena post yangu ya mwanzo utaona kwa nini naadhimisha siku ya kuzaliwa..
Unaposema 'birthdays' ni kusogelea kifo huu ni mtazamo wako ambao ambao umeamua kuuchukua..
Kimsingi siku ulipozaliwa ndio siku ulipoumbiwa kifo..hivyo dhana ya kuogopa kifo sidhani kama inamashiko..

Hujanipa sababu za msingi wa kusherehekea au kuadhimisha hilo
Niambie ni kitu gani kinakufanya uadhimishe na sio kusherehekea!

Umuhimu wa nini ulipoonekana?
Au umuhimu wa kusherehekea kulisogelea kaburi?

Wanaochangisha watu kwaajili ya birthday zao ni washamba, sio lazima ukusanye watu kama huna uwezo unaweza ku- celebrate na familia. To me birthday ni wakati wa kumshukuru Mungu kwa kuendelea kunipa hii oxygen bure na pia ku-reflect malengo niliyojiwekea. Kufa tutakufa tu hata usiposheherekea siku yako ya kuzaliwa

Kabla ya maendeleo ya sayansi kuzaa kuliua 30% ya kina wazazi, kuzaliwa kuliua 20% ya watoto kufika miaka 5 kuliua 20% ya waliobaki, kufika miaka 10 kuliua 10% ya waliobaki tena. Afrika ukifika miaka 35 asilimia >60 ya watu wa umri wako wamekufa.
Hapo ndio umuhimu ulipoonekana.

Hujajibu ni kivipi ufurahie kulisogelea kaburi!

Advantages of Celebrating Birthdays!

“Birthdays are good for you. Statistics show that people who have the most live the longest”
Here are a few examples:

  1. Attitude to life changes, for the better – more positive and able to take life one day at a time
  2. Totally given up on trying to keep everybody happy — how liberating!
  3. Knowing I am so far from perfect and happy to be a “work in progress”
  4. Better able to be in the moment – “don’t sweat the small stuff”
  5. More appreciative of the simplest of experiences
  6. Resilience, Perspective, and Humour
Birthdays are also a time to celebrate with the people you care about… they are also opportunities to review the year; what “worked” and what “needs improvement” — set goals for the next year of life to ensure we are living the life that is congruent with our True Self…
 
haina maana sana kusheherekea na me nilikuwa najiuliza wa kusheherekea ni wewe au mama yako aliyekuona na uliyemuumiza wakati wakujifungua? kwa sababu tunafurahia kiitu mabacho ukijui wala hujui kilitokea nini? ni mtazamo wangu tu....

Hilo la mama angalau linaweza kuwa na mashiko kwa sababu ni siku aliyotimiza lengo lake la kuzaa

Tatizo huyo anaezaliwa kuisherehekea au kuiadhimisha!
 
Advantages of Celebrating Birthdays!

"Birthdays are good for you. Statistics show that people who have the most live the longest"
Here are a few examples:

  1. Attitude to life changes, for the better – more positive and able to take life one day at a time
  2. Totally given up on trying to keep everybody happy - how liberating!
  3. Knowing I am so far from perfect and happy to be a "work in progress"
  4. Better able to be in the moment – "don't sweat the small stuff"
  5. More appreciative of the simplest of experiences
  6. Resilience, Perspective, and Humour
Birthdays are also a time to celebrate with the people you care about… they are also opportunities to review the year; what "worked" and what "needs improvement" - set goals for the next year of life to ensure we are living the life that is congruent with our True Self…

Wewe umeelewa nini kwenye haya maelezo uliyoyaweka hapa?
 
Just be positive minded,,,kufa kupo tu....
Kwani mimi nimesema hakupo?
nadhani kusingekua na maendeleo kama watu wangekuwa wanafikiria afterall tutakufa tu...
Your running out of the line
Sijazungumza kuhusiana na watu kuacha kufanya mambo kwa sababu ya kifo
Ninazungumza sababu ya watu kufurahia kuikaribia siku ya kufa
Usijichanganye
unajua umuhimu wa furaha hata kama ni ya muda mfupi?..
Kabla ya kuniuliza kuhusiana na furaha unatakiwa uniambie furaha ni nini
Halafu uniambie hiyo furaha inahusiana nini na siku yako ya kuzaliwa
Kisha uniambie inahusiana nini na kuiadhimisha
UNAJUA KITU KINAITWA UTILITY?...ITS ALL ABOUT BEING HAPPY,,FOR YOUR SELF BEING AS WELL AS OTHERS..
Unaongeza maswali badala ya kujibu maswali
Unaniambia kuhusiana na Utility bila kuniambia hiyo ni kitu gani na inahusiana nini na siku yako ya kuzaliwa
Acha kujipa kazi kubwa
tukuanza kufikiria kufakufa tu
Nani amefikiria kufa tu?
Au mimi kuhoji kusherehekea siku ya kuzaliwa tayari nakuwa nazungumzia kufa?
Acha woga
Nimesema kuifikia siku ya kuzaliwa ni sawa na kukisogolea kifo
Je,wewe unalifurahia hilo?
,ndio misongo ya mawazo yenyewe hiyo,,,
Huu ni woga wa kutofautiana na mazoea
Msongo wa mawazo ni mamboi yako ya kufikirika tu

Kama unasema kifo kipo tu ni kitu gani kikufanye uwe na msongo wa mawazo?
Acha woga!
 
Hilo la mama angalau linaweza kuwa na mashiko kwa sababu ni siku aliyotimiza lengo lake la kuzaa

Tatizo huyo anaezaliwa kuisherehekea au kuiadhimisha!

me hapo huwa siwaelewi kabisa aisee, mama mzazi ndo anatakiwa asheherekee....
 
Wewe hujaelewa nini kwenye hayo maelezo niliyoweka hapo?
Kwanza sijasema sijaelewa
Hiyo minaonesha huelewi hata ulibandika nini

Halafu,

Kuuliza ni rahisi sana lakini kujua unataka kujua nini kwenye swali lako ni mtihani mkubwa sana

Wacha nikuambie ni kitu gani nilichokuwa nataka nijue kwenye swali langu halafu na wewe uniambie na wewe unataka kujua nini kwenye swali lako

Wewe umeniletea copy hapa inayozungumzia siku ya kuzaliwa
Hiyo haimaanishi kuwa wewe ndie mwandishi
Wewe kutokuwa mwandishi kuna uwezekano hujaelewa kwa ufasaha lengo la mwandishi wa maandiko hayo kitu kilichonifanya mimi nikuulize ulichokielewa ili nikuulize maswali huku nikijua ninaemuuliza anaelewa alicholea na kile ninachomuuliza

Kuleta copy hapa hakuna maana kuwa umeelewa
Pia unaweza kuwa umeellewa nusu au hujaelewa kabisa
Hayo yote nitayajua kutokana na majibu yako kuhusiana na namna ulivyoelewa hiyo copy and paste yako

Sasa niambie lengo la swali lako!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom