jiwe angavu
JF-Expert Member
- Aug 28, 2015
- 21,691
- 41,849
binti sasa anashindia mihogo...poor girl papuchi sio uwekezaji wenye tija.
Nakuamini kuwa si binti tena maana leo umekumbukia enzi za appetiteI wishi bado niitwe binti.
Lakini wakati huo maafande waliwafaidi nyie bidhaa adimuNimbekumbuka mbali sana, mtu hajui kitu alafu anajifanya mjuaji, tuliwachora sana maafande😀😀😀
Wait a minute! Mgonjwa wa kwanza wa ukimu hapa Tanzania aligundulika mwaka 1983. Hivyo umechanganya masomo au?Na ukiambiwa watu walitoka HIV -ve wewe acha tu.
BintiMpeni pole huyu binti,
Binti huyu alizaliwa mrembo mwenye sura ya kuvutia, tangia akiwa shule wavulana aliosoma nao walimsumbua kumtaka ki mapenzi, alipomaliza kidato cha nne hakuwa na matokeo mazuri ya kuendelea na elimu ya juu. Wazazi wake ni wa hali ya kawaida, binti huyu alianza kujihusisha na shughuli za urembo.
Katika mashindano ya urembo katika mkoa wao, mgeni rasmi alikuwa kigogo mmoja kutoka serikalini, majaji wa waamuzi wote walipendekeza jina la binti kama mshindi, mgeni rasmi alimuachia binti namba yasimu.
Binti alianza mawasiliano na kigogo, kutokana na majukumu na uzito wa kazi zake, kigogo alimwambia binti ingawa kuonana kwao kutakuwa ni kwa shida, lakini atahakikisha account yake siku zote ina pesa, hataki kumwona mtoto mzuri kama yule anapata shida.
Binti alianza kuwekewa pesa, ankara zilizokuwa zinaingia kwenye account yake zilikuwa milioni 50, 30, kwa uchache 20. Binti alipata boyfriend wa kutanua nae, boyfriend alimwonyesha binti jinsi ya kula bata Mombas, Dubai na sehemu nyinginezo.
Kigogo alipomhitaji binti, alisafiri mpaka katika mji mkuu wa nchi yao na alikaa hotelini kwa siku mbili au tatu. Kigogo alimpenda sana binti na alimwambia ajiheshimu na pia amheshimu yeye kwani wadhifa wake ni mkubwa pia anaiheshimu ndoa yake.
Baada ya uchaguzi mkuu, kigogo alikosa wadhifa alioshikilia, pia rais aliyechaguliwa alibana sana mianya ya fursa, kigogo alishindwa pesa ya kuendesha familia yake licha ya pesa ya kumpa binti. Binti alichanyanyikiwa, hakumpenda kigogo kabisa lakini alipenda pesa, baada ya kuona pesa imekata, kigogo akipigiwa simu anashindwa kupokea kutokana na aibu na ufalme alijitangazia kwa binti.
Boyfriend alipoona binti hana pesa ya matanuzi ameanza kumwonyesha wasichana wengine tena wadogo kuliko binti anatanua nao wazi wazi. Binti hakuwahi hata kununua bodaboda wakati wa neema, licha ya hayo alihama nyumbani na kupanga nyumba ya kifahari ili awe free na boyfriend.
Binti amepata msongo wa mawazo (depression) anafikiria kuutoa uhai wake.