Binti wa Kichaga- tuijiandaaje kwa Posa? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Binti wa Kichaga- tuijiandaaje kwa Posa?

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Twilumba, Jan 4, 2012.

 1. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280
  Habari wanajamvi!
  Nina ndugu yangu wa karibu sn amebahatika kupendana na binti wa kichaga. Wapo katika hatua za awali kwenda kupeleka posa huko Marangu kwa wazazi wa huyu dada!

  Swali:
  Je tujiandaeje kwa ajili ya kupeleka posa hiyo kwa namna nyingine ni vitu gani tuviandae ikiwa ni pamoja na vile vya kimila ili kufanikisha zoezi hili muhimu tusije kosa mke!

  Naomba kuwasilisha kwa mchango!
  Asante.
   
 2. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,077
  Likes Received: 10,436
  Trophy Points: 280
  mbege lazima kama debe tano,mbuzi. vingine nimesahau ngoja wadau wafike.
   
 3. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280
  Asante nangojea zaidi!
   
 4. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Ana nyumba huyo, ana gari huyu, akaunti yake ya benki iko sawia, anafanya kazi gani na asisahau kubeba kuwa na kadi ya NBC Master Card! Natania mkuu ila kwa ushauri wangu ni kwamba mtafuteni mzee wa kichaga mmarangu atawajuza juu ya mambo yao ya kikabila la marangu
   
 5. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #5
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Debe tano ni zamani, last month tulimsindikiza mkaka mmoja kupeleka posa nkashangaa manake aliambiwa mbege debe 48, mbuzi 5, na makorokoro kibao. Kwa mahesabu ya haraka anahitajika kupeleka kama 1m na zaidi manake wamempigia mahesabu ya debe 1 ya mbege times 48.. Na hapo huyo binti wanaishi wote na wamepata mtoto mmoja ( ana 6 month)...huko ni marangu pia.
   
 6. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #6
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  msisahau mgolele wa babu na kilemba cha bibi
   
 7. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #7
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280
  hizo debe 48 wanakunywa ukoo mzima?
   
 8. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #8
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  Mbege na ndafu lazima, maana ulabu ni kama kupiga mswaki kwa maji
   
 9. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #9
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280

  Asante mkuu ndyoko hii hata kule kwetu ipo, tutazingatia! Ingawa kule kwetu huwa rangi zinazingatiwa pia!
   
 10. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #10
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 278
  Trophy Points: 180
  we si unataka mke, toa tu hizo debe 48 usitake kujua wanakunywa wangapi. Toa hiyo pombe chukua kinyoya chako yaishe uende ukaanzishe genge then duka mtoto akuletee maendeleo na maisha yaendelee. Wamarangu wako poa tu hawana kwere!
   
 11. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #11
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280
  Tutatoa mkuu!
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  Jan 4, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Na marafiki + majirani unawaacha wapi?

  Msisahau blanket, nadhani la bibi au sijui mama mtu.
   
 13. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #13
  Jan 4, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  mwaka huu umekuwa wa wachanga
  haya endeleeni kuwadadavua.

  Japo naamini unachangamsha baraza
  sababu ana wazee wake wanaweza kufuatilia vizuri.
   
 14. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #14
  Jan 4, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Jiandae na Mbege na Debe 20 hivi za kunywa Ndugu, Jamaa na Marafiki na Mjirani, Blanketi la Bibi, Kuna vitenge vya Mashangazi, Mbuzi kadhaa na Bia Kreti kama tano hivi
   
 15. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #15
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280
  Asante kumbe taratibu ni kama kule kwetu!
   
 16. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #16
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280
  JF ni zaidi ya uifikiriavyo!
   
 17. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #17
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Ukoo mzima pia bado hawatazimaliza, labda wanawagawia na majirani...afu hawataki mbege live, wanataka pesa mf. Debe 1 inauzwa sh elfu 30, unafanya 30'000 times 48 then unawapa cash yao... Papo kwa hapo zilinunuliwa debe 5 za ukweli afu ndio akaambiwa hizo 48 zilizobakia alete pesa... Ila labda itakuwa ni tofauti kati ya ukoo na ukoo..
   
 18. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #18
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,077
  Likes Received: 10,436
  Trophy Points: 280
  hapana mkuu kama sikosei hivyo vitu hutolewa siku ya send off.
   
 19. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #19
  Jan 4, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,077
  Likes Received: 10,436
  Trophy Points: 280
  Lizzy blanket sijui na kapu la mama hivyo vyote hotolewa siku ya send off.
   
 20. Twilumba

  Twilumba JF-Expert Member

  #20
  Jan 4, 2012
  Joined: Dec 5, 2010
  Messages: 6,142
  Likes Received: 869
  Trophy Points: 280
  Huku huwa hawatoi kaniki ya bibi?
   
Loading...