Binti kuwa karibu sana na baba yake

Binti kuwa karibu sana na baba yake

Naweza kusema ni nature, ila tamaduni ndio ruhusu/kataza kutegemea na tamaduni, ni namna ya kumwambia au kumfundisha kuwa nwanaume utakayekua nae awe na tabia hizi, au akutreat hivi, caring, loving, listening and all that, na mara nyingi wanawake waliokulia ktk mazingira hayo wanajiamini, wanajua nini wakitarajie kutoka kwa mwanaume(ukiondoa sex). Ndio maana baba huwa anamtoa binti wakati wa harusi, kwamba uko tayari sasa kumkabili.
 
Uhusiano wangu na baba yangu ulikuwa wa kipekee, Mimi ndo binti pekee katika familia yetu basi Mzee alinidekeza hadi basi, full kubebwa hadi jitu zima, alinifundisha kusoma na kuandika manake huko vidudu nilikuwa sielewi, Hadi kidato cha tatu nilikuwa nafuliwa uniform na Mzee.
Yani nilikuwa namjua akifurahi au akikasirika, na kuna kipindi ulitokea mgogoro kati yake na mama so akawa anachelewa kurudi ( ilikuwa sio kawaida yake kuchelewa kurudi home) Niliogopa, nikaanza kumpa huduma za kifalme ili asipachukie nyumbani kwake, nikawa nampikia vizuri( alikuwa anapenda kula vizuri) nahakikisha nyumba safi kabla hajarudi, namuandalia maji ya kuoga, nampigisha story za mpira( alikuwa shabiki wa simba), basi akaanza kuwahi kurudi nyumbani na akirudi yupo sebuleni na mimi. Mama akaanza kunimind, akawa ananambia yani angekuwa mama wa kambo angehisi kuna kitu kinaendelea kati yangu na Mzee.
na nadhani huu uhusiano wangu na baba umeniathiri katika kuanzisha mahusiano ya kimapenz, ili uuteke moyo wangu lazima uwe na sifa walau moja kama ya baba yangu. hapo najifeel secure mtoto wa baba mie.
Mola mlaze mahali pema peponi baba yangu mpenzi.
ameen.
Nlidhani peke yangu, kumbe hadi wewe watamani mwanaume mwenye sifa kama za your dad. The loss you feel after this loss yaan haielezeki.
 
sitamani kurudi nyumaaaaa
sitamani kuwa kama zamaniiiiii
waooow my dad richa ya mimi kuwa binti pekeee kwake na richa ya kunipata baada ya kukata tamaaa ya kuwa na mtoto wa kike maana mimi na kaka ninaemfuatia tumepishana ten years
but kanilea kikomandooo mnooooo
staki hatakukumbuka or may be kwa vile alikuwa mjeshi simlaumu but nilikuwa nakula bakora wacha kabisaaaa nikileta ripoti mbaya ni kiama ohoooops still yuko hai na nimeshakuwa binti mkubwa
nashukuru kidogo amejirekebisha baada ya siku moja kugundua anaposafiri mimi huwa nina furaha sana
atleast now tunaweza hata kupiga stori kuhusu na vita vya kagera na hunifanya nicheke mbele yake bila hofu tena
 
Wenye baba zenu hongeren sn na mshukurun mungu sn, ktk vitu ambavyo vimeniumiza ktk maisha yangu nikukosa mapenzi ya baba na sio kwmb alifarik, hatukuwa tunajua alipo ni kitu kigumu sn ndugu sn, baba na mama ni pande mbili za sarafu moja zinategemeana, wote wana umuhimu ktk mukuzi ya mtoto, bora ujue kwmb lbd alifariki angalau utakua huumii sn lkn kutokujua ni yupi, yuko wap, na je anafahamu km anawatoto au hafahamu hilo ni tatizo.

Hata mama ajitahd vip still kuna nafas tu atahitajika kusimama baba. Nampendasn mamangu na kajitahd sn mpk hapa nilipofika ni juhud zake na naziheshimu mno lkn bd kukosa nafas ya kusema maneno km "shikamoo baba" kwangu ni ndoto mpk sasa ninaandika comment. Lbd niwe naitoa kwa wengne lkn sio kwa aliyenizaa.

Ushauri wangu kwa wote (wanaume na wanawake) kuna umuhim mkubwa kwa wazazi wote wawil kushirik ktk malezi ya watoto unless kuna sababu zisizozuilika kwa kutokuwepo mmoja. Naomba niishie hapa unaweza usiamini ila hii thread imenitoa machozi.

Daah! Nimesoma thread yako imenitoa machoz,nawaonea raha sana wenye baba zao, nami katika maisha yangu sijawah kuita Baba. Ni bora angekuwa amekufa,yupo na hana msaada wowote kwangu. Mama yangu ndio kila kitu amenifikisha hapa nilipo. Hayo mapenzi ya baba wala hata siyajui mwenzenu.
 
Daah! Nimesoma thread yako imenitoa machoz,nawaonea raha sana wenye baba zao, nami katika maisha yangu sijawah kuita Baba. Ni bora angekuwa amekufa,yupo na hana msaada wowote kwangu. Mama yangu ndio kila kitu amenifikisha hapa nilipo. Hayo mapenzi ya baba wala hata siyajui mwenzenu.

Pole mpenzi tumshukuru mungu kwa kila jambo.
 
Back
Top Bottom