Binti asusa kula

Binti asusa kula

IDyangu

Member
Joined
Apr 24, 2014
Posts
99
Reaction score
22
Kuna binti hapa mtaani kwetu mwenye umri wa miaka 21. Amesusa kula tangu juzi kisa uncle wake amemwambia akapime damu(HIV test) kama yupo safe kwa sababu anaugua malaria mara kwa mara. Kwa madai ya huyu binti ni kwamba aliuugua malaria miezi 2 iliyopita.Na mwezi huu ameugua tena. Na mwenendo wake si mbaya sana hapa mtaani. Binti analalamika kwamba uncle wake hamuamini ndo maana amemwambia akapime. Naombeni ushauri wenu wakumpatia huyu binti. ...... UPDATE...... Binti amekubali ushauri, ameanza kula. Ila suala la kupima bado. Asanteni kwa ushauri wenu.
 
Mwambie atakama haendi kupima, bhas ale chakula ashibe maana akiacha kula, atakonda af ndo hali Itakua mbaya zaidi...
 
kupiiima! unaweza kukimbia majibu yako ila mpe pole na mwambie ale coz kutokula co solution
 
Mwambie atakama haendi kupima, bhas ale chakula ashibe maana akiacha kula, atakonda af ndo hali Itakua mbaya zaidi...

Nimemshauri hivyo lakini hajanielewa. Nimemtumia rafiki yake wa karibu naye hakufanikiwa. Analia tu
 
Mpe pole,mwambie ale chakula na maji ya kutosha,halafu asiogope chochote muda ukifika kila kitu kitakuwa sawa,ajaribu kwenda hospital kubwa kwa uchunguzi zaidi juu ya malaria.
 
Sawa kwa sasa nashindwa kumshauri akapime. Majibu yakitoka mabaya anaweza akafanya uamuzi mbaya. Ngoja nijitahidi kwa suala la kula.

Hivi mbona mnapenda kuwasingizia marafiki? huyo rafiki yeye ndio hajui kutumia internet siyo?
 
Kuna binti hapa mtaani kwetu mwenye umri wa miaka 21. Amesusa kula tangu juzi kisa uncle wake amemwambia akapime damu(HIV test) kama yupo safe kwa sababu anaugua malaria mara kwa mara. Kwa madai ya huyu binti ni kwamba aliuugua malaria miezi 2 iliyopita.Na mwezi huu ameugua tena. Na mwenendo wake si mbaya sana hapa mtaani. Binti analalamika kwamba uncle wake hamuamini ndo maana amemwambia akapime. Naombeni ushauri wenu wakumpatia huyu binti.

Wewe kapime usisingizie nothing girl.
 
Hivi mbona mnapenda kuwasingizia marafiki? huyo rafiki yeye ndio hajui kutumia internet siyo?

Hapana mkuu Matola ni binti wa mtaani kwetu. Kutumia internet anajua. Ingekuwa mimi nahitaji msaada ningeomba direct hapa jukwaani. Na kama kupima ningeenda kupima. Siogopi majibu wala. Najua kuna majibu ya aina 2.
 
Last edited by a moderator:
Akila ulete mrejesho...
Akienda hosp ulete mrejesho...
Akipima ulete mrejesho...
Akikimbia majibu ulete mrejesho...

Naona kufungua sredi imekua fashen...
 
Kupima tuu ndo aache kula, mwambie asile wiki kama hajaenda kwetu pazuri.
 
Kanatest hako,sister wangu alijifanya anatakakunywa Sumu mama akaanza kulia mzee alipokuja akaambiwa akamkorogea ndoo nzima ya sumu akamuwekea chumbanikwake mbona hakuinywa mpakaleo yupo,ngoja aumwe njaa atakula tu.
 
Back
Top Bottom