Binti aliyepata hasara ya maisha.

Jeho

JF-Expert Member
Jul 2, 2011
5,053
5,502
Dada mmoja ambaye alikuwa anakaribia kufunga ndoa na mchumba wake, alikuwa na rafiki yake kipenzi ambaye alimshirikisha katika mambo mengi sana. Na wiki moja kabla ya ndoa, rafiki yake alimletea taarifa juu ya uaminifu hafifu wa mchumba wake. Ili kurahisisha naomba nirumie binti X kuwakilish rafiki wa bibi harusi mtarajiwa. Na taarifa zile zilimshitua sana yule bibi harusi mtarajiwa, basi akaamua kuomba ushauri wa nini cha kufanya toka kwa binti X. Binti X alimshauri kwa kumuambia kuwa amkatae siku ya harusi kama adhabu kwa mchumba wake. Siku zilijivuta, hatimaye siku ya harusi ikawadia, mchungaji alipoanza maswali kwa bibi harusi iwapo kweli binti anaridhia kuolewa, binti alijibu kama ifuatavyo simpendi huyo mwanamme, wazazi wangu ndio walionilazimisha kuolewa, kwa hiyo sipo tayari kuolewa. Mchungaji akamuuliza Bwan harusi, sasa tunafanya nini kama binti amekukataa?. Bwana harusi alisema, naomba kama kuna binti aliye tayari kufunga pingu za masha na mimi, ajitokeze maana leo ni siku yangu ya kuoa na zege haitalala. Mchungaji aliuliza kama kuna binti aliye tayari. Muda ulipita pasipo binti yeyote kujitokeza na hatimaye binti mmoja akanyanyuka na kusema yeye tuko tayari kumsaidi huyo kaka, kweli pale pale iabidi aliyekuwa bibi harusi avuliwe shela na harimaye binti aliyejitolea akavishwa shela na hatimaye ndoa ikaendelea kufungwa. Bibi harusi wa awali alipotazama vizuri nani aliyejitolea kuolewa, lahaula!!, alikuta ndiye yule rafiki yake yaani binti X. Aliyekuwa bibi harusi akapaza sauti na kusema nataka kufunga ndoa na mme wangu maana huyo aliyejitolea, ndiye aliyenidanganya nimkatae mpenzi wangu siku ya ndoa. Mchungaji akaamua kumuultiza Bwan harusi kuwa anamtaka yupi, naye akajibu anamtaka yule wa pili. Kwa hiyo bibi harusi original akawa amekosa kuolewa.
Ni vivyo katika upande wa mambo ya Mungu, kuna watu wanaondanganya watu ambao hatimaye wamedangantika. Ndiyo maana Mungu alitahadharisha katika kitabu cha Isaya 9:16 alionya kwa kusema haya Kwa maana wawaongozao watu hawa ndio wawakoseshao, na hao walioongozwa na watu hao wameangamia. Kumbe ukikubali kuongozwa na watu wapotoshao utakuwa umepotea na mauti ya milele yatakuwa yanakusubiri. Kuna watu akishasikia chochote kikitajwa na kiongozi wa dhehebu lake, basi anaamini, hata kama hayo ni maneno ya kupotosha. Nao wanatahadharishwa hivi katika Yeremia17:5-6, BWANA asema hivi, Amelaaniwa mtu yule amtegemeaye mwanadamu, amfanyaye mwanadamu kinga yake na moyoni mwake amemwacha BWANA, Maana atakuwa kama fukara nyikani, Hataona yatakapotokea mema, bali atakaa jangwani palipo ukame, katika nchi ya chumvi isiyokaliwa na watu. Mengi yapo ya kuandika lakini kwa sasa naomba kuishia hapo.
 
Stori za kusadikika hizo, ama ndo utatumia ibadani jumapili? Mchungaji aruhusu mtu kufunga ndoa kutoka kwa waumini bila kuandikisha, kutangaza siku 21 kwa mujibu wa sheria na kufanya mafundisho ya ndoa?
 
Stori za kusadikika hizo, ama ndo utatumia ibadani jumapili? Mchungaji aruhusu mtu kufunga ndoa kutoka kwa waumini bila kuandikisha, kutangaza siku 21 kwa mujibu wa sheria na kufanya mafundisho ya ndoa?

Hii ni habari ya kweli kabisa, kama wewe huamini kwamba ni ya kweli, endelea kutoamini.
 
Stori za kusadikika hizo, ama ndo utatumia ibadani jumapili? Mchungaji aruhusu mtu kufunga ndoa kutoka kwa waumini bila kuandikisha, kutangaza siku 21 kwa mujibu wa sheria na kufanya mafundisho ya ndoa?

Du! yaani King'asti mtata aisee, mwenzio atakuwa ametumia kama mfano tu huo jama, lengo ilikuwa kumwaga neno kwa chini pale ........
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom