Bingwa wa kupinga... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bingwa wa kupinga...

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Wa Nyumbani, Apr 5, 2011.

 1. Wa Nyumbani

  Wa Nyumbani JF-Expert Member

  #1
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 432
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35
  Bibi kizee mmoja alikwenda benki moja maarufu sana hapa nchini ili kuweka fedha zake. Alipofika mapokezi aliuliza.
  "Naomba kumwona meneja mkuu wa benki hii"
  Mfanyakazi wa mapokezi akamuuliza,
  "Unataka kumuona kwa shida gani?"
  "Nataka kufungua akaunti" akajibu bibi
  "Akaunti inafunguliwa hapa hapa mapokezi, sio kwa meneja" akajibu mtu wa mapokezi.
  "Mimi nataka kufungua akaunti ofisini kwa meneja maana nina pesa nyingi sana hapa" akasisitiza yule bibi kizee
  "Hata hapa unawezxa kufungua kwa pesa hizo zote na zitakuwa kwenye usalama tu"
  "Kama hutaki kunuruhusu kufungulia kwa meneja, basi nakwenda kufungua kwenye benki nyingine" akasema bibi huku akiwa amechukia.

  Kuona hivyo, mfanyakazi wa mapokezi akaamua kumpeleka kwa meneja.
  "Kwa nini mmeshindwa kumfungulia akaunti huko mapokezi" akauliza meneja
  "Amesema lazima afungulie kwako na nilipomsisitiza afungulie mapokezi alitaka kuondoka"

  Basi meneja akaamua amfungulie yeye akaunti. Bibi akazitoa pesa, zilikuwa shilingi milioni kumi taslimu! hadi meneja akashangaa na kumuuliza,
  "Bibi inaonekana pesa hizi umezidunduliza kwa muda mrefu sana ee"
  "Hapana, nimezipata juzi juzi tu"
  "Umezipataje?"
  "Kwa kupinga na mtu"
  "Kweli? kupinga tu hadi ukapata pesa zote hizo?"
  "Yaah, nimepinga tu. Tena hata na wewe tunaweza kupinga tu"
  "Ehe, tunaweza kupinga vipi" akauliza meneja kwa udadisi.
  "Kwa mfano, tunaweza kupinga kuwa kesho saa kama hizi, pumbu zako zitakuwa za square yaani pembe nne. Kama zikiwa hivyo, wewe utanipa milioni kumi na zisipobadilika mimi nitakupa hizo zangu"
  Meneja kusikia hivyo, akakubali mara moja na wakapinga. Bibi kizee akaondoka. Meneja alibaki akiwa na wasiwasi sana, hadi alipotoka ofisini kila mara alikuwa anazishika pumbu zake kuona kama zimebadilika. Hadi siku iliyofuata asubuhi bado pumbu zake zilikuwa kama kawaida.
  Saa nne asubuhi bibi kizee alifika benkikwa meneja akiwa ameongozana na jamaa mmoja nyuma yake.
  "Ehe naona bibi umekuja" meneja akasema huku akiwa na wasiwasi. Mara moja akatoka kwenda chooni kuhakikisha kama pumbu zake ziko sawasawa. Akakuta hazijabadilika, akarudi mara moja ofisini kwake.
  "Haya bibi, pumbu zangu hazijabadilika, ehe, si unaona ziko sawasawa? nimekushinda!" akasema meneja kwa kutamba. Bibi kizee akamsogelea meneja na kumwambia kwa sauti ya chini chini.
  "Sawa baba lakini mimi nitahakikishaje?"
  "Njoo tu uzishike" akasema meneja.
  "Sawa lakini lazima uvue suruali nizishike pumbu zako nihakikishe" alisema bibi.
  Meneja akavua suruali na bibi kizee akaanza kuzichezea pumbu zake.
  Wakati akiendelea kuzichezea (zilikuwa hazijabadilika) yule mtu aliyeongozana na bibi alikuwa anajibamiza ukutani kwa nyuma. Meneja akashangaa na kumuuliza bibi.
  "Mbona huyo jamaa uliyekuja naye anajibamiza ukutani? huoni ataumia?"
  "Heh he heee! huyo KALIWA!!" alisema bibi na kuendelea, "Nilipinga naye jana kuwa leo hii saa nne nitakuwa nazichezea pumbu za meneja wa benki kubwa hapa nchini, akakataa eti siwezi. Tulipinga shilingi MILIONI ISHIRINI! hivi anakwenda kuzitoa baba!"
  Meneja akachukua milioni kumi na bibi akapata milioni ishirini! ha ha haaa ahaaaaa!!!
   
 2. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #2
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ndefu kidogo lakini nzuri.
  ha ha ha ha!
   
 3. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #3
  Apr 5, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Makubwa haya
   
 4. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #4
  Apr 5, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Waungwana kuna watoto humu jamvini!!!!:tape:Lakini nzuri sana!!!
   
 5. t

  torres0909 Member

  #5
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Duuuuh! Huyo bibi noma.
   
 6. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #6
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  meneja faida, bibi faida. Mjinga kaliwa. Lkn katika neno pumbu mara nyengine tumia korodani. Si ndiyo lenye wepesi zaidi, au vipi?
   
 7. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #7
  Apr 5, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  kwe, kwe, kwe! Bibi balaaaa!
   
 8. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #8
  Apr 5, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  pasua kichwa:peep:
   
 9. a

  allydou JF-Expert Member

  #9
  Apr 5, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 1,485
  Likes Received: 572
  Trophy Points: 280
  huyo bibi ni bonge la mjasiriamali. nahisi alianza kwa huyo mzushi alieliwa kwanza, alipopata uhakika wa 20m, ndio akaenda kwa confidence sasa kwa meneja kuweka dau la 10m.
   
 10. Wa Nyumbani

  Wa Nyumbani JF-Expert Member

  #10
  Apr 5, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 432
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 35


  Ndugu yangu Mkwaruzo, nashukuru kwa kurekebisha lugha, lakini usingetaja neno lenyewe maana tayari umeshaharibu, ungesema usitaje jina la kitu alichokuwa anakichezea. Lakini poa!
   
 11. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #11
  Apr 6, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,023
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280

  Tafsida kidogo jamani..
   
 12. m

  mgalisha Member

  #12
  Apr 6, 2011
  Joined: Oct 16, 2010
  Messages: 60
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Daaah..., Bibi ametisha ile mbaya inaonekana ni mjasiliamali aliyebobea kwa ubunifu wa mbinu za kuingiza pesa
   
 13. T

  Tasia I JF-Expert Member

  #13
  Apr 6, 2011
  Joined: Apr 21, 2010
  Messages: 1,226
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  finally nimecheka. duh mjini jamani!!
   
 14. Globu

  Globu JF-Expert Member

  #14
  Apr 7, 2011
  Joined: Jan 12, 2011
  Messages: 7,975
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  Bibi mjanja sana huyo. Genius.
   
 15. Anko Sam

  Anko Sam JF-Expert Member

  #15
  Apr 7, 2011
  Joined: Jun 30, 2010
  Messages: 3,216
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Inachangamsha akili, ila kutaja pumbu siyo dhambi. mbona ingekuwa imeandikwa kwa kiingereza wangetaja direct "scrotum". maswala ya kuficha ficha inaleta matatizo.

  Weka vitu hadhalani tutazoea tu. Siyo Zeruzeru aitwe Albino (english), Kipofu-asiye ona! Kiziwi-Asiyesikia, Mwizi-kibaka, Mwogo-asiyesema kweli! Malaya-anayejiuza! Sema tu wazi tutasikia ukakasi lakini tutazoea kama wazungu.
   
 16. Idimi

  Idimi JF-Expert Member

  #16
  Apr 7, 2011
  Joined: Mar 18, 2007
  Messages: 10,222
  Likes Received: 2,088
  Trophy Points: 280
  ..Nilisoma mahali version yake ya Kiingereza, nilicheka sana
   
 17. Edward Teller

  Edward Teller JF-Expert Member

  #17
  Apr 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,818
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  teh teh teh-bibi mjanja sana
   
 18. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #18
  Apr 8, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 18,023
  Likes Received: 743
  Trophy Points: 280

  Sawa Anko lkn mtandao wasomwa na wote mkuu...
   
 19. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #19
  Apr 8, 2011
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,870
  Likes Received: 6,610
  Trophy Points: 280
  pumbu za Meneja?! Meneja baada ya kushikwa sana akasema:bibi endeleaaaa.....!
   
 20. Mkwaruzo

  Mkwaruzo JF-Expert Member

  #20
  Apr 9, 2011
  Joined: Feb 21, 2011
  Messages: 566
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Ni sawa ila sometime hatutakiwi kurekebisha peke yake bali kwanza tunabomoa na kujenga tena upya. Hii inasaidia kupata uimara zaidi. Lkn pia nakubaliana na ww ktk ulichoongezea kwa kile nilichokisema
   
Loading...