Mary Moraa bingwa wa Dunia, atwaa tena taji la Diamond League

Dalton elijah

JF-Expert Member
Jul 19, 2022
216
478
651df01f5b3ee361b137059f.jpg


Mary Moraa ambaye ni bingwa wa dunia na Jumuiya ya Madola mbio za mita 800, ametwaa taji la riadha za Diamond League duru ya Doha nchini Qatar. Bingwa huyo wa Kenya ambaye ni afisa wa polisi, katika mbio za mita 400 na mita 800, aliweza kukamilisha mizunguko miwili kwa dakika moja na sekunde 57.96.

Katika nafasi ya pili, bingwa huyo aliweza kufuatiwa kwa karibu na Muingereza Jemma Reekie (1:58.42), Benin Noelie Yarigo wa uingereza (1:58.70) katika nafasi ya tatu, Muethiopia Habitam Alemu (1:59.08) katika nafasi ya nne na bingwa wa dunia mwaka 2019 Halimah Nakaayi kutoka Uganda (1:59.48) akatwaa nafasi ya tano, mtawalia. Mbio hizo ziliwahusisha wanariadha 11.

Taji hilo la Dora linajiri katika ziara yake ya kwanza nchini Qatar. Na kwa sasa Moraa anapanga kushiriki tena katika mbio za 600m katika mashindano ya USAF Los Angeles Grand Prix mnamo Mei 9, 2024 nchini Amerika ambako anapanga kuvunja rekodi nyingine.


Baadaye, Mei 25, 2024 anatarajiwa kushiriki katika mbio za 800m katika mashindano ya Eugune Diamond League, itakayofanyika nchini Amerika.

Kando na Moraa kutoka nchini Kenya, bingwa wa dunia wa kurusha mkuki, 2015, Julius Yego, mfalme wa mbio za 1500m, 2019 Timothy Cheruiyot, bingwa wa dunia na Afrika wa chipukizi wasiozidi umri wa miaka 20 wa umbali huo Reynold Cheruiyot, Abel Kipsang pamoja na Brian Komen, walishiriki katika mashindano hayo ya Dora.
 
Si ngoja tuendelee kuboresha elimu yetu kwa kuimarisha tuition mtoto anaingia darasani saa 1 asubuhi anamaliza kusoma saa 12 jioni
Na ndio tumeongeza madrasa shuleni 😥
 
Back
Top Bottom