Bingu alishaandaa kaburi lake ndani ya jumba la kifahari?

alikula akashiba mno,
akaandaa nyumba ya milele,
na Mungu akamsikia akamlaza humo,
kazi yake imekwisha.

Hapa nimepata somo, maana jumba kama hilo hata watoto watarithije, maaha huwezi kulikata kama keki na kugawana vipande, hatari yake wataishia kugombana. Kwa nini asingejenga nyumba kadhaa ambazo watoto wake wangegawana urithi vizuri? Angejenga jengo kubwa la kupangisha mjini watoto wake wake kuridhi wangeuza au kuwa kitegeuchumi na kuchuma kutokana na wapangaji? Labda waliuze jengo hilo na shamba kwa mtu, lakini ameshazikwa ndani ni zuio la wazi jengo kubaki kama maktaba.
 
JK lazima atakopi na kupesti hii.......MSOGA get prepared!!

Nahisi kwani anaonekana kuwa mfuasi wake, pamoja na mchoko wa safari ndefu ya Kutoka Brazil, licha ya wimbi la mageuzi lililoongozwa na makamanda huko dodoma kuishtaki serikali yake, Kikwete aliridhia kuwahi Maziko ya Bingu wa Mutalika, bila shaka amesharudi na michoro ya jengo hilo tayari kwa wasanifu mahiri kuanza kuandaa Kule kijijini Msoga.
 
Ni kweli mwendo ameumaliza lakini je ni kweli aliilinda imani na taji atavishwa?

Na haya ndo maneno yake kutoka kwenye bible
2 Timothy 4: "[SUP]7[/SUP] I have fought the good fight, I have finished the race, I have kept the faith. [SUP]8[/SUP] Now there is in store for me the crown of righteousness, which the Lord, the righteous Judge, will award to me on that day—and not only to me, but also to all who have longed for his appearing. "
 
na hata hao watoto wanaweza kuamua kuishi ulaya
wakaacha hayo majumba.

kaka yangu parisi (R.I.P) aliishi pale moshi mjini
alijitahidi sana kujenga majumba mengi makubwa
hata pale kijijini akabadili akajenga majengo
imara ya kisasa.

akiwa katikati ya ujenzi Mungu akamchukua,
watoto alikuwa nao wengi tena wengi ni wa nje ya ndoa na mbaya zaidi hakuwaendeleza kielimu
baada ya hapo sijaona tena maendeleo toka alivyoondoka
zaidi ya kuuza uza zile mali.

tutafute vya kiasi kwa kuwa tutaviacha vyote.

Hapa nimepata somo, maana jumba kama hilo hata watoto watarithije, maaha huwezi kulikata kama keki na kugawana vipande, hatari yake wataishia kugombana. Kwa nini asingejenga nyumba kadhaa ambazo watoto wake wangegawana urithi vizuri? Angejenga jengo kubwa la kupangisha mjini watoto wake wake kuridhi wangeuza au kuwa kitegeuchumi na kuchuma kutokana na wapangaji? Labda waliuze jengo hilo na shamba kwa mtu, lakini ameshazikwa ndani ni zuio la wazi jengo kubaki kama maktaba.
 
Ngwazi maana yake nini?

Waafrika mataito ndo yenyewe haswa. Wewe huoni siku hizi hadi wahandisi na wanasheria wanaweka taito zao kwenye majina yao....eti advocate (adv.) Bwa'Nchuchu....eng. Kichuguu....lazima watu wajue bana.

Na sisi wengine tutaandika hivi. Mheshimiwa Kibaka Eeka Mangi, ukiwa mzoefu zaidi utaitwa Mheshimiwa Jambazi Eeka Mangi. Sasa kila mtu ataje la kwake litaanza na nini! Hata wale wa Ohio ka wapo siku hizi nao waweke titles zao bana!
 
na hata hao watoto wanaweza kuamua kuishi ulaya
wakaacha hayo majumba.

kaka yangu parisi (R.I.P) aliishi pale moshi mjini
alijitahidi sana kujenga majumba mengi makubwa
hata pale kijijini akabadili akajenga majengo
imara ya kisasa.

akiwa katikati ya ujenzi Mungu akamchukua,
watoto alikuwa nao wengi tena wengi ni wa nje ya ndoa na mbaya zaidi hakuwaendeleza kielimu
baada ya hapo sijaona tena maendeleo toka alivyoondoka
zaidi ya kuuza uza zile mali.

tutafute vya kiasi kwa kuwa tutaviacha vyote.

Dhana nzuri ni watoto kuwajengea uwezo wa kuanza kujitegemea, si wakute mali wakati hata uwezo wa kuzitunza hawana, kwani wazazi hawajui lini watamwendea Baba wa Milele.
 
Ni kweli mwendo ameumaliza, lakini je ni kweli imani aliilinda na ni kweli atavalishwa taji na bwana?

Wawe wanaangalia maneno ya kuandika kulingana na marehemu alivhoishi hapa duniani

Na haya ndo maneno yake kutoka kwenye bible
2 Timothy 4: "[SUP]7[/SUP] I have fought the good fight, I have finished the race, I have kept the faith. [SUP]8[/SUP] Now there is in store for me the crown of righteousness, which the Lord, the righteous Judge, will award to me on that day—and not only to me, but also to all who have longed for his appearing. "
 
kweli mkuu,
Miaka ya kuishi ni sabini kama una nguvu ni 80 tu
lakini unaweza kuondoka mapema pia kama wengine
walivyoondoka,
but tuwasomeshe hawa madogo
waje washindwe wenyewe mkuu wangu.

Dhana nzuri ni watoto kuwajengea uwezo wa kuanza kujitegemea, si wakute mali wakati hata uwezo wa kuzitunza hawana, kwani wazazi hawajui lini watamwendea Baba wa Milele.
 
Mutharikas-ndata-house-550.jpg

Nyumba yenyewe inaonekana mpya kabisa, na bado umaliziaji ulikuwa haujakamilika kutoka na mwonekano wa vifusi vya mchanga upande wa kulia wa zile bendera, na hata uwanja ulikuwa bado kusanifiwa. Ni kama aliandaa tu kaburi la kupumzishwa.

Binadamu tumefumbwa mambo mengi ya ajabu.
Twajiona tulivyo bila kujua hatima ya maisha yetu yetu duniani ni lini, ni siri ya Mungu pekee.
Twaandaa mengi ya kujistarehesha bila kujua hatima yetu.
Twafikiria kesho wakati tumefumbwa kutojua kesho tutaifikia au la!
Hili la kutojua siku wala saa lini tutamwendea baba wa milele ni funzo kubwa kutodharau uwepo wa Muumba kwani hata hatujui tulipojiona tuna akili wapi tulitoka na wapi tutakwenda.
Mungu katufumba mengi, tukidharau tutaumbuka.

Waungwana tusiwe watumwa wa mali bali utendaji wetu na uwajibikaji wetu ndio dhana bora ya maisha na yenye kutupa amani mioyoni. Katu utajiri hasa utokanao na hujuma hakuna kula kwa starehe kabisa, ni balaa tupu. Ulaji gani ni mtamu huku mtu unanyooshewa kidole usoni?
 
kweli mkuu,
Miaka ya kuishi ni sabini kama una nguvu ni 80 tu
lakini unaweza kuondoka mapema pia kama wengine
walivyoondoka,
but tuwasomeshe hawa madogo
waje washindwe wenyewe mkuu wangu.

Mamndenyi@ asante kwa wazo lako zuri na nakubaliana kwa maoni yafuatayo hapa chini.
Sijatoka nje ya wazo hilo, ndio maana nimesema kuwajengea watoto na vijana uwezo wa kujitegemea. Haina maana waanze kuhangaika kama hawakuwa na wazazi, ila kuwaandalia mazingira ambayo watanzia maisha yao.

Ni dhamira nzuri kuwa na uzazi wa mpango, ambapo mtu kuwa na watoto wawili au watatu haitamwia ngumu kuwaachia mazingira mazuri ya kuendesha maisha kutokana na alivyowaandalia msingi. Kama mtoto amepata elimu ya kutosha na papo kuwa na pa kuweka kichwa chake sidhani atahangaika kama mie mzazi wake niliyeanza na kuchunga ng'ombe huku nimevaa lubega kufurukuta hadi umri wa makamu ndipo niwe na pa kuhifadhi kichwa changu.

Ndio napendekeza kama mtu unajenga bora jaribu kujanga nyumba kadhaa kama mbili au tatu kadiri ya idadi ya watoto ili urithi usiwe nongwa kwa watoto kuanza kugombania nafasi ikikuruhusu, kwani ukishahakikisha hilo ni wazi hati ya mirathi itaonyesha nani apate kipi au nyumba ipi, na watoto wenye busara wataridhia hekima na ridhaa ya mzazi wao kwani kawaandalia pa kuanzia maisha, kama wakishindwa ni uzembe wao.

mkuu asante kwa somo lako,
nami Mungu akinipa uwezo
nitaongeza walau nyumba moja
kwa kuwa maeneo tayari Mungu
keshanipa.

Mamndenyi@ asante kwa wazo lako zuri na nakubaliana kwa maoni yafuatayo hapa chini.
Sijatoka nje ya wazo hilo, ndio maana nimesema kuwajengea watoto na vijana uwezo wa kujitegemea. Haina maana waanze kuhangaika kama hawakuwa na wazazi, ila kuwaandalia mazingira ambayo watanzia maisha yao.

Ni dhamira nzuri kuwa na uzazi wa mpango, ambapo mtu kuwa na watoto wawili au watatu haitamwia ngumu kuwaachia mazingira mazuri ya kuendesha maisha kutokana na alivyowaandalia msingi. Kama mtoto amepata elimu ya kutosha na papo kuwa na pa kuweka kichwa chake sidhani atahangaika kama mie mzazi wake niliyeanza na kuchunga ng'ombe huku nimevaa lubega kufurukuta hadi umri wa makamu ndipo niwe na pa kuhifadhi kichwa changu.

Ndio napendekeza kama mtu unajenga bora jaribu kujanga nyumba kadhaa kama mbili au tatu kadiri ya idadi ya watoto ili urithi usiwe nongwa kwa watoto kuanza kugombania nafasi ikikuruhusu, kwani ukishahakikisha hilo ni wazi hati ya mirathi itaonyesha nani apate kipi au nyumba ipi, na watoto wenye busara wataridhia hekima na ridhaa ya mzazi wao kwani kawaandalia pa kuanzia maisha, kama wakishindwa ni uzembe wao.

MIMI NIKIFA HILI LANITOSHA

Kaburi_la_Meya_wa_Kwanza_wa_Moro_shambani_kwake_Mkundi.jpg
Mbona umetumia matofali mengi sana ya kujenga chumba cha shule ya watoto wanaosomea chini ya mti.
Hata hivyo umejitahidi maana waliotoa hoja wote ni wanafiki kwani sijaona aliyetaka kuzikwa katika kitoba au mfuko ea rambo.
Atakayefanya hivo atakuwa ndo mzalendo wa kweli latila kuokoa matumizi yasiyo ya lazima.
 
Hilo jengo la kaburi alizikwa kwanza mke wake wa awali, na liliisanifiwa kwa ajili ya kuzika watu wawili; Huyo mkewe na yeye mwenyewe. Baada ya mkewe wa kwanza kufariki, hatimaye Bingu alioa tena. Sasa huyu mjane aliyeachwa itabidi azikwe nje ya kijijengo hicho - kwani hakuna nafasi yake humo maskini!
 
MIMI NIKIFA HILI LANITOSHA

Kaburi_la_Meya_wa_Kwanza_wa_Moro_shambani_kwake_Mkundi.jpg

Nimeipenda hii, lakini jambo moja ambalo naweza kutofautiana nawe ni hili. Tujitahidi kutenga maeneo ya kuzikia, maana kaburi hili laonekana katikati ya shamba, kwa maneno mengine linazuia uhuru wa kutumia eneo hili kwa vile kuna kaburi. Kwa nini tusitumie maeneo yaliyotengwa kwa kuzikia na maeneo kama haya yabaki na uhuru kwa watumiaji au wanandugu wa familia?
 
Back
Top Bottom