Binafsi sijaielewa hii picha

Binafsi sijaielewa hii picha

Hili ni jukwaa la siasa - mbn unaleta picha kwani hapa ni habari mchanganyiko?
 
wakuu mimi binafsi nashindwa kuelewa hii picha na jinsi huyo mdada aliesimama alivoshika tama sijui alikua anamaanisha nini.. kama umeielewa tuelezeeee tuelewe na sisiView attachment 1093972
Huo ni uonevu.

Wanawatoza hao wamama 20k then Bashite anatumia mamilioni kununua ma infinity na kwanza vile viti vyake pale bandarini inawezekana alishavitoa
 
Wabunge wa ccm Mungu anawaona miaka miachache iliyopita “uchumi wa Gas” miaka kadhaa baadaye Gas yetu imechukuliwa na “Mapepari by jpm” sasa mnakaba walalahoi mtaani
 
Zaidi ya kuwasaidia na kuwapa hata miamvuli ya kuwakinga na jua na mvua ni kuwaonea tu

I wish i could be a millionaire
 
Mimi nimeielewa hiyo miguu ya bia huko nyuma ya mama huyo.
 
wakuu mimi binafsi nashindwa kuelewa hii picha na jinsi huyo mdada aliesimama alivoshika tama sijui alikua anamaanisha nini.. kama umeielewa tuelezeeee tuelewe na sisiView attachment 1093972
Hapana, maelezo yako yanaonyesha kwamba hukuelewa kabisaaaa katika kuisoma hiyo picha. Maana kubwa haipatikani kwa huyo mdada aliyeshika tamaa. Angalia mkusanyiko mzima wa watu waliozunguka hapo. Utaanza kuielewa picha ukifanya hivyo.
 
Tangu zamani wauza nyanya, mchicha na Karanga wapo kila eneo la masoko na barabara zetu. Kawaida ni wao kuchangia ushuru wa kawaida wa soko.
Sasa hiki kinachofanyika Cha kuwalazimisha Hadi Bibi zetu kulipa Kodi ya kichwa kwa kisingizio kuwa ni machinga ni kupotosha neno "Machinga"
Tatizo ni kuwa wanakosana na matajiri wa dunia wakidhani wanaweza, matokeo yake wanalazimika kuwawanyang'anya maskini ili waendeshe nchi!!!
 
Japo aliyeshika kitambulisho anaonesha kuwa na furaha labda kwa kuwa ameshika kitambulisho cha mama muuza mboga ambacho kwa upande wake kina thamani ya 20,000/= ila sura ya mama muuza mbona inasema mengi ambayo kwa hakika angepewa nafasi aongee labda asingesema chochote zaidi ya kutokwa machozi.

Kiukweli ni picha ambayo imenifanya nimejisikia huzuni sana..nimejikuta najawa chuki juu yao.
 
Anasikitikia uonevu.mkuu wa wilaya kama na vx akina mama wanawaza hawajauza hats fungu moja MTU anataka 20
.
Aibu kwa Serikali inayoimba kila kukicha kuwa inawajali na kuwawezesha Wanyonge wa nchi hii.
 
Hivi wale watoto walioamua kujiingiza kwenye biashara ndogo ndogo baada yakukatiza elimu yao kwa mimba za utotoni na Mheshimiwa kuamua kuwatoza kisa hataki kuwasomesha wamama. Leo ndio wanaonekana wamaana sana na wanafaa kulichangia Taifa kwa kununua vitambulisho vya Wamachinga?? Tufikiri kwa pamoja juu ya hili.
 
Hii hali mbona iko sana tu leo nimeshuhudia mkulima mmoja ktk soko la mazao mjini Kasulu amenyang'anywa gunia la maharage yamepakiwa kwenye gari na maafisa wa halmashauri kisa hana kitambulisho cha mjasilia mali nimejaribu kuhoji inakuwaje huyu si ni mkulima nikaambiwa mkulima ni kulima na kula tu akishaleta sokoni kuuza eti huo ni ujasilia mali imeniuma sana vijijini raia wa hali za chini wanaonewa sn na hao maofisa
 
wakuu mimi binafsi nashindwa kuelewa hii picha na jinsi huyo mdada aliesimama alivoshika tama sijui alikua anamaanisha nini.. kama umeielewa tuelezeeee tuelewe na sisiView attachment 1093972
Hapo ni Mama wa Kimeru na mafungu yake 3 ya mboga za majani amevalishwa kitambulisho cha rais na kutozwa kwa lazima sh.20,000/= taslim, hivyo vitambulisho vipo vingi sana vinatakiwa viuzwe viishe vyote upesi.
Hao walioshika tama wamehamaki jinsi mama alivyokutwa na makuu hadi akalazimika kufungua fundo la kanga yake na kutoa 20,000 ya akiba ya pekee ya familia waliyokuwa nayo.
 
Mtaji wa huyo mama muuza mchicha ni Buku moja tu, lakini amelazimishwa kuchujua kitambulisho cha mjasiriamali kwa Buku 20!!
Yan picha inaonyesha jinsi jamii inayotazama tukio hilo haijapendezwa na kitendo hicho kabisa na hawana cha kufanya zaidi ya kubaki na sonono
 
Back
Top Bottom