Leo katika kipindi cha magazeti yetu asubuhi nilisikia taarifa ya kutumbuliwa watumishi sita wa Mwaruwasa- Morogoro na Mhe. Waziri wa Maji.
Binafsi nimesikitika sana kwa tabia iliyozuka ambapo Mhe. Waziri anakuwa na mamlaka ya kutumbua watumishi bila kufuata utaratibu uliowekwa katika Utumishi wa Umma.
Kusimamishwa kwa mtumishi wa umma kuna taratibu zake. (1) Kwanza kuletewa tuhuma dhidi yake (2) Mtuhumiwa kujibu tuhuma alizoplekewa (3) Kuona kama kuna kosa na hatua za kuchukua dhidi ya mtuhumiwa.(4) Kama kusimamishwa/kufukuzwa kazi basi mtuhumiwa anayo nafasi ya rufaa kwenye ngazi za juu.
Sheria zipo lakini hazifuatwi hivi tuko nchi gani hii ambayo hata sheria hazifuatwi?. Wabunge ndo wanaotunga hizi sheria akiwemo Mhe. Waziri lakini baadaye wanazikiuka.
Katibu Mkuu wa Utumishi wa Umma yupo na anajua fika taratibu na yeye yuko kimya. Acheni uonevu dhidi watumishi wa umma.