Binadamu wasio na upendo wanaandaliwa!

Tatizo wazazi wanatofautiana vipaombele, wengine swala la malezi ya watoto wanalichukulia kiwepesi Sana kiasi kwamba wanaona ni sawa mtoto alelewe mbali ili kukimbizana na maisha (utafutaji),ila inasahaulika kuwa ata huko wanakopelekwa watoto kuna mabadiliko pia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanawake ninyi ndio wa kulaumiwa kwa kila hatua. Ninyi ndio wa kwanza kuuonja huo uchungu siku ukianza kuonekana hapa duniani. Kwa nini?? 1. Ninyi ndio mliwaleta hapa duniani

2. Ninyi ndiyi mliwalisha maziwa yenu yaani damu yenu hadi wakaujua ugali

3. Ninyi ndiyi mlikaa nao chumbani mkisema nao na kuwaambia baba zao walivyo wabaya walipowaacheni chumbani wakalala kwa mchepuko.

Ghafula, mkaona waende boarding school hata kabla hawajajua jina la baba yao. Huyo mtoto alikuwa analililia penzi la mamake sio la babake.

Ndo maana tunawapata watu makatili kama hao wasojulikana. Wanawaua wenzao bila hata hofu yoyote ndani yao. Hawajui nnini maana ya kupendana
 
Ni kweli mkuu!Maafisa usalama wengi wanachukuliwa wale waliosoma boarding seminary!!!makatili kama wasiojulikana nchini!!hawana uchungu na ndugu zao!!!
 
Hii ni mbaya sana wazee,nina ndugu yng mmoja daaaah,sasa hv ni mtu mzima kidogo kuliko hata mimi,alipitia maisha hayo,haelewani kabisa na wazazi wake wala ndugu zake,yaani haoni umuhimu wao kabisa,anawatukana atakavyo,anawajibu anavyojisikia,yaani jamaa kawa kama mnyama vile,hajawahi kulelewa na wazazi wake,yaani yeye kila mtu anamchukulia poa tu
 
Nina ushahidi katika hilo mkuu
Hii ni serious case........ushahidi upo wa kutosha....hata kama mama na baba mna confrontation zetu.....mustakabali wa watoto ni jukumu lenu pamoja.........watoto wanateseka kweli...
 
Natamani sana Mheshimiwa waziri wa Elimu angeusoma uzi huu. Natamani sana. Natamani sana angewanusuru watoto wasio na hatia, watoto wanaoathirika na maamuzi mabaya ya wazazi wao. Nimesoma maoni ya wadau mpaka machozi yakanilengalenga!
 
Hii ni serious case........ushahidi upo wa kutosha....hata kama mama na baba mna confrontation zetu.....mustakabali wa watoto ni jukumu lenu pamoja.........watoto wanateseka kweli...
wanaoelewa ni wachache wengi huchukulia kama sehemu ya kuthibitisha utajiri wao
 
Back
Top Bottom