Ni kweli kabisa, kuna familia moja niiona siku moja ya visiting day shule ya boarding, wamekuja na magari mawili ya Noah baba na mama ages 40+ wamemvisit mtoto wao wa nursery, niliumia. Mtoto alipowaona alilia, akalia, akalia kilio kikuu, wazazi wakabembeleza wakala mazagazaga waliyoleta, wakashusha na kwenye magari matakataka chungu mzima meeengiii, kimbembe saa ya kuondoka mtoto alianza kulia tena kwa maumivu makali sana, huwezi amini wale wazazi waliondoka na kumwacha pale sijamini mpaka leo. Yaani mtoto alilia kwa uchungu mpaka akaishiwa nguvu wakambeba kumpeleka dorm!