Binadamu wananikatisha tamaa ya kuendelea na mapambano ya kusaka fedha

Sela Son

JF-Expert Member
Dec 31, 2018
2,623
6,089
Wanajf, habari zenu. kiukweli Mimi Ni mzima wa afya. Hili Ni la kushukuru. kwa miaka 42 sasa nimeendelea kuwa miongoni mwa walio hai. Nisiwe wa kushukuru kwani akina flani tuliowazika juzi hawapendi kuishi?

Nimeamua leo kuandika hili si kwasababu niwafurahishe kwa wino huu adhim, Bali nina jambo.

Kiukweli leo nina hasira na kukata tamaa Sina furaha. Hasira ya wazi moyoni. Leo hata mke wangu nimemsalimia mara moja nikaamua kulala.

Binadamu wana ubaya wa kutisha sana. Wengine huua, wengine huroga maisha yasiwanyookee wenzao, lakini wengine huzini nk. Lakini je mungu kwa uovu huu mkuu kwa mujibu wa vitabu vyake hutoa adhabu kuu? Hapana!

Waswahili husema mungu si Athumani. HakiyaMungu, Mungu angekuwa Boss wangu Kazini bwana Vesper ( si jina lake) Mimi nisingepata ridhiki ya kulisha familia yangu initegemeayo.

Leo nilichelewa kidogo kuelekea job. Kufika hapo job nikakuta boss kashafika Yuko na chawa wake wawili. Kuniona tu wakaanza kelele.Mara kwanini umechelewa.

Mara kwanini huchomekei. Mara ghafla boss wangu akapayuka hello br unaonekana kibri kimekujaa. Nimekaa Hapa ninaapa hutafanikiwa kimaisha popote duniani. Huna kazi humu. Umejawa na kibri na dharau. Nikauliza mkuu kwani shida nini? Akaniambiaje br sikiliza.

Humu ndani we unajifanya ndo umesoomaa kumbe masters yenyewe ya ( akitaja sehemu za nyum a za mwili. Hakika nimemvulilia mtu Yule lakini moyo wangu unaniuma. Kosa langu ni Nini hasa?
Cha kujiuliza .

Maneno yake yananichoma moyo. Hadi kuna muda nimejaribu kuwaza je wafu nao huteseka Kama mimi?
Nikiikumbuka hiistoria yangu hujifungia ndani na kulia .

Je walimwengu hawanipendi? Lakini je nimekosa Nini?
Nimetoka mbali Sana . Huko udhalilifu kisa umaskini lilikuwa Jambo la kawaida.

Je, Mungu angekuwa anatoa ridhki kwa uchache wa dhambi za kumkosea yeye na wanadamu Kuna mtu angefanikiwa?
 
Sijaelewa hapo. Huyo jamaa mswahili Swahili amekuwaje bos kwako ngadu huyo?. Kama utaweza Kaka fikiria beyond mana hapo kibarua kitaota nyasi muda wowote ule
 
Kaka maisha ya siku hizi kama adhabu vile ila ndo kumbe TUNAISHI NA KUISHIA
 
Ahaaaa hata usiumie ukiona watu kazini wanakusema vibaya kaaa ukijua kuna vitu unawazidi. Au wengine wanatafuta sababu ureact kisha wapate sababu. Dawa yao ni kuongeza bidiii katika kazi.Ukiwaona tabasamu kama hakuna kilichotokea trust me u will kill them. Maisha mafupo usijipe stresss sababu ya watu. Keep it up
 
Kwanza pole.

Pili usiweke moyoni hayo mambo. Potezea.

Chapa kazi kaka. Bosi kaona unatishia nafasi ya cheo chake. Mjibu kwa kuchapa kazi.
 
Back
Top Bottom