jose mjasiriamali
JF-Expert Member
- Sep 17, 2014
- 1,772
- 1,614
- Thread starter
-
- #21
Kama wamekamatiwa sehemu ya tukio au kama ushahidi upo kwamba ni wezi then no way acha walipe gharama ya matendo Yao.
Tatizo kuna watu wanachomwa kwa kudhaniwa tu kuwa ni wezi ama kwa chuki zingine kabisa.
These are signs of a failed. state.
Ni tukio la kusikitisha sana, limetokea mkoa wa Dodoma,wilaya ya chemba,tarafa ya goima,kijiji cha Igunga ambapo watu wawili wanaosadikika kuwa ni wezi wamechomwa moto hadi kufa. Ni kitendo cha kikatili kwa kweli.
Mkiona mnauhakika hao ni wezi, halafu mkaona hakuna aliye tiari kupoteza muda kwenda mahakamani kutoa ushahidi ili mtu afungwe, na mkaona kifungo atakachopata hakiendani na kosa. Mnafikia uamuzi wa kummaliza
Kuna kipindi watu ubinadamu huwa unawatoka kutokana na matukio wanayotendewa na wanadamu wenzao.....
wewe uliyekuwa eneo la tukio ulifanya jitihada gani sasa?Umesubiria wamechomwa ndo ukawa busy kupiga picha?Kutokuchukua hatua kwenu ndo kumeifikisha dunia hapa ilipo.Na ndo kinachoonekana hapa,wameenda kufuatwa walipokuwepo then wakapelekwa sehemu ya tukio af ndo wakateketezwa
Yeah ni hatari pale inapotokea watu kwa kuhisi au kwa sababu wanazojua wao kufanya hivi. Imeniuma sana binafsiDah!inasikitisha sana, wabongo watu wa ajabu sana!mambo kama haya walitakiwa wafanyiwe mafisadi,lakini cha ajabu wanafanyiwa vibaka.
wewe uliyekuwa eneo la tukio ulifanya jitihada gani sasa?Umesubiria wamechomwa ndo ukawa busy kupiga picha?Kutokuchukua hatua kwenu ndo kumeifikisha dunia hapa ilipo.
wezi na vibaka kuchomwa moto sio kitu kipya Tanzania.... Lakini wale mafisadi papa na majoka wenye makengeza kutandikiwa mazulia na kuchezewa ngoma kamwe hutasikia wakichomwa, wakati wao ndio wanatuletea maafa zaidi
mgh.................... walofanya hivi hawawez kua na roho ya kibinadamu kabisa yaani kumfanya hivi binadamu mwenzio hata kama unamtuhumu kua ni mwizi bado maisha yanathaman zaid ya kitu kilichoibiwaa
Vipi kama waliofanya mauwaji walinunuliwa maana kinachoonekana hapa wauwaji walibebwa kwa fuso kwenda kuwateketeza watuhumiwa
Kwa Kondoa/Chemba ni suala la kawaida sana. Kuna kipindi cha nyuma 2006---2010 baadhi ya watu waliodhaniwa kuwa ni majambazi waliuawa sana kwa style hiyo. Watu walikuwa wanajitolea gari zao na mafuta juu ili kupakia watu wakwenda kufanya msako msituni na majambazi walidakwa wengi sana wakati huo ila haya matukio hayakuripotiwa kabisa. Mie binafsi nimewahi kushuhudia hayo matukio. Ili saidia sana hadi kukawa na utulivu ila sasa wameanza kuja tena.