Binadamu wachomwa kama ndafu Mkoani Dodoma

Binadamu wachomwa kama ndafu Mkoani Dodoma

Kama wamekamatiwa sehemu ya tukio au kama ushahidi upo kwamba ni wezi then no way acha walipe gharama ya matendo Yao.

Tatizo kuna watu wanachomwa kwa kudhaniwa tu kuwa ni wezi ama kwa chuki zingine kabisa.

These are signs of a failed. state.

Na ndo kinachoonekana hapa,wameenda kufuatwa walipokuwepo then wakapelekwa sehemu ya tukio af ndo wakateketezwa
 
Ni tukio la kusikitisha sana, limetokea mkoa wa Dodoma,wilaya ya chemba,tarafa ya goima,kijiji cha Igunga ambapo watu wawili wanaosadikika kuwa ni wezi wamechomwa moto hadi kufa. Ni kitendo cha kikatili kwa kweli.

Wacha walipuliwe wanakera sana hawa
Juzi hapa mtaani kwetu wamemkata mzee na mkewe asubuh wanaenda zao kununua bidhaa za genge daaa
 
Mkiona mnauhakika hao ni wezi, halafu mkaona hakuna aliye tiari kupoteza muda kwenda mahakamani kutoa ushahidi ili mtu afungwe, na mkaona kifungo atakachopata hakiendani na kosa. Mnafikia uamuzi wa kummaliza

Pale wamehisi mkuu hawana uhakika na inafahamika hivyo kwa wanakijiji wote
 
Ila inabidi mjue chanzo. Kuna wezi wanaudhi sana unakuta walikua wanasumbua sana mtaani...
 
Dah!inasikitisha sana, wabongo watu wa ajabu sana!mambo kama haya walitakiwa wafanyiwe mafisadi,lakini cha ajabu wanafanyiwa vibaka.
 
Na ndo kinachoonekana hapa,wameenda kufuatwa walipokuwepo then wakapelekwa sehemu ya tukio af ndo wakateketezwa
wewe uliyekuwa eneo la tukio ulifanya jitihada gani sasa?Umesubiria wamechomwa ndo ukawa busy kupiga picha?Kutokuchukua hatua kwenu ndo kumeifikisha dunia hapa ilipo.
 
Dah!inasikitisha sana, wabongo watu wa ajabu sana!mambo kama haya walitakiwa wafanyiwe mafisadi,lakini cha ajabu wanafanyiwa vibaka.
Yeah ni hatari pale inapotokea watu kwa kuhisi au kwa sababu wanazojua wao kufanya hivi. Imeniuma sana binafsi
 
wezi na vibaka kuchomwa moto sio kitu kipya Tanzania.... Lakini wale mafisadi papa na majoka wenye makengeza kutandikiwa mazulia na kuchezewa ngoma kamwe hutasikia wakichomwa, wakati wao ndio wanatuletea maafa zaidi
 
wewe uliyekuwa eneo la tukio ulifanya jitihada gani sasa?Umesubiria wamechomwa ndo ukawa busy kupiga picha?Kutokuchukua hatua kwenu ndo kumeifikisha dunia hapa ilipo.

Jitihada zimefanyika kabla hata hawajachomwa ila kikundi kinachoonekana kinunuliwa kwa kazi hiyo kilikuwa na nguvu kuliko raia wengine, pia kijijini ni ngumu kufikiri kama wanaweza kuwadhibiti wenye fedha. Ila hadi sass watuhumiwa wamekamatwa pamoja na kuonyesha tambo kwamba sio muda watarudi uraiani
 
wezi na vibaka kuchomwa moto sio kitu kipya Tanzania.... Lakini wale mafisadi papa na majoka wenye makengeza kutandikiwa mazulia na kuchezewa ngoma kamwe hutasikia wakichomwa, wakati wao ndio wanatuletea maafa zaidi

Hii ndo Tanzania, zaidi ya unavyo ifahamu
 
mgh.................... walofanya hivi hawawez kua na roho ya kibinadamu kabisa yaani kumfanya hivi binadamu mwenzio hata kama unamtuhumu kua ni mwizi bado maisha yanathaman zaid ya kitu kilichoibiwaa
 
Natamani mtu anayeona kuwa hii kitu ni halali angekuwa eneo la tukio then ajionee mwenyewe, hii kujichukulia sheria mkononi sometimes inapelekea kupoteza maisha ya watu wasio na hatia
 
ila sometimes wezi nao ni kero mi hapo nawaonea tu huruma ndugu zao
 
Jose mjasiriamali,kuna kitu inaonekana unakifahamu zaidi juu ya mauaji haya,funguka unaficha nini?inaonekana unaona jamaa hawakuwa na kosa lolote,sasa chamno?
 
basi tubadili adhabu..

Next time tukikamata wezi, shughuli itakayofuata ni kuwakata viganja vya mikono halafu tuwaachie waende zao kwa amani.

Rest In peace Kaka Jambazi.
 
Kwa Kondoa/Chemba ni suala la kawaida sana. Kuna kipindi cha nyuma 2006---2010 baadhi ya watu waliodhaniwa kuwa ni majambazi waliuawa sana kwa style hiyo. Watu walikuwa wanajitolea gari zao na mafuta juu ili kupakia watu wakwenda kufanya msako msituni na majambazi walidakwa wengi sana wakati huo ila haya matukio hayakuripotiwa kabisa. Mie binafsi nimewahi kushuhudia hayo matukio. Ili saidia sana hadi kukawa na utulivu ila sasa wameanza kuja tena.
 
Vipi kama waliofanya mauwaji walinunuliwa maana kinachoonekana hapa wauwaji walibebwa kwa fuso kwenda kuwateketeza watuhumiwa

Wanakijiji wanasemaje juu ya tabia ya hao marehemu kabla ya tukio, yaani maisha yao yalikuwaje mwaka mmoja uliopita, je hawakuwa mafuska, je hawakuwa dhurumati, je hawakuwa makuwadi? Tupe majibu ya haya maswali kama unayo.
 
Kwa Kondoa/Chemba ni suala la kawaida sana. Kuna kipindi cha nyuma 2006---2010 baadhi ya watu waliodhaniwa kuwa ni majambazi waliuawa sana kwa style hiyo. Watu walikuwa wanajitolea gari zao na mafuta juu ili kupakia watu wakwenda kufanya msako msituni na majambazi walidakwa wengi sana wakati huo ila haya matukio hayakuripotiwa kabisa. Mie binafsi nimewahi kushuhudia hayo matukio. Ili saidia sana hadi kukawa na utulivu ila sasa wameanza kuja tena.

Ila inahitaji moyo wa tofauti sana kutekeleza hivi vitendo,mauaji kwa haya maeneo ni mambo ya kawaida hadi wanajisahau. Halafu sijui huku pako vipi maana unakuta wahusika wapo tu mitaani wanwendelea na shughuli kama kawaida
 
Back
Top Bottom