Binadamu wachomwa kama ndafu Mkoani Dodoma

Binadamu wachomwa kama ndafu Mkoani Dodoma

Wanakijiji wanasemaje juu ya tabia ya hao marehemu kabla ya tukio, yaani maisha yao yalikuwaje mwaka mmoja uliopita, je hawakuwa mafuska, je hawakuwa dhurumati, je hawakuwa makuwadi? Tupe majibu ya haya maswali kama unayo.

Wenyeji wanadai jamaa hawakuwahi ku ripotiwa kwa kosa lolote kabla ya hili tukio ambalo hata wanachodaiwa kuiba hakikuibwa, na wengi wameonekana wakilia huku wanalalamika kuwa umasikini wao ndio chanzo cha yote hayo, kwamba hawana uwezo wa kufanya chochote
 
Jitihada zimefanyika kabla hata hawajachomwa ila kikundi kinachoonekana kinunuliwa kwa kazi hiyo kilikuwa na nguvu kuliko raia wengine, pia kijijini ni ngumu kufikiri kama wanaweza kuwadhibiti wenye fedha. Ila hadi sass watuhumiwa wamekamatwa pamoja na kuonyesha tambo kwamba sio muda watarudi uraiani

mleta mada nahisi unauhusiano kimaada na marehemu..
 
mleta mada nahisi unauhusiano kimaada na marehemu..
Nawatambua marehemu kwa kuwaona tu, sikumbuki hata kama niliwahi kusalimiana na yeyote kati yao, anyway una uhuru wa kuona na kusema chochote
 
Ila angalau uthibitishe basi, ila kuhisi tu mkachukua maamuz kama hayo ni hatari, halafu kwenye kijiji kidogo kama hiki?? Nakosa amani sana kuwa hapa maana mauwaji ya watu yamezidi

Image ya watanzania sasa hivi ndivyo inavyoonekana. Roho mbaya, wivu, chuki na ushirikina. Ni watu wachache wafanyao haya lakini sifa inaenea kote
 
Mi naona hapo kuna Mengi siyo bure haiwezekani watu watoke walikotoka wakamate watu na kuanza kuwachoma bila sababu. Ni lazima kunasababu wasiyo ijua wananchi wa kijiji hicho.
 
Image ya watanzania sasa hivi ndivyo inavyoonekana. Roho mbaya, wivu, chuki na ushirikina. Ni watu wachache wafanyao haya lakini sifa inaenea kote

Haya matendo sijui yanawafundisha nini watoto wetu,jamaa wamekuwa hivyo kutwa nzima, kuna kitu watoto walioliona hili tukio hawatakisahau na kita waharibu sana
 
Mi naona hapo kuna Mengi siyo bure haiwezekani watu watoke walikotoka wakamate watu na kuanza kuwachoma bila sababu. Ni lazima kunasababu wasiyo ijua wananchi wa kijiji hicho.

Ila ukweli hatuwezi jua kuna nini hapo sisi wanakijiji wa hapa, labda tuwaache polisi wafanye yao
 
adui wa mtu ni mtu mwenyewe kuna haja gani ya kumbanika binadam mwenzio kiasi hikii hata kama mwizi??hakika damu ya hawa watu itawalilia hawa waliofanya unyama huu, mi naona hawana utofauti na Jihad Jonh wa ISIS
 
Auaye kwa upanga atakufa kwa upanga, damu ya hawa watu itawalilia, NI UKWELI USIOPINGIKA
 
Kadiri walivyoyenda na ndiyo malipo yao hiyo!

Ogopa wananchi wenye hasira kali!
 
Hapa ndipo ninapoamini kuwa ubin adam umetoweka wamebaki wanyama watupu sasa duniani.

Mimi Mgeni wa Mungu kwenu haya kwangu ndio maajabu ambayo siamini kama binadam anaweza kumchoma moto mwenzake
 
Mimi binafsi nawaunga mkono hao Wananchi waliofanya hilo tukio.

Wezi ni watu hatari sana, ndani ya dk moja wanaweza kubadili mfumo wa Maisha yako.

Kwa ambao hawajawahi kukutana na hawa viumbe unaweza kuona wameonewa... Ila walichokipata ni haki yao.

Ikulu watu wakubwa kabisa wameshirikiana na Rugemalira kwenye ESCROW kukuibia pesa ya umma. Umewachoma moto?
 
Na hawajathibitisha ila wanahisiwa tu!!ila ni kitendo ambacho hata wenyeji hapa kijijini hawajaridhishwa nacho, ni kama ubabe flani iv kwamba mtu ana hela kwa hiyo anaweza kufanya chochote
jose mjasiriamali

Kwahiyo ina maana wahusika wa uchomaji huo wanajulikana? mimi kwa kweli pamoja na kero wanayoleta wezi lakini kitendo cha kuwaua sikubaliani nacho kabisa mara mia kuwakata mkono mmoja tu ili waishi wakijutia madhambi yao
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom