kirikou1
JF-Expert Member
- Nov 8, 2016
- 4,802
- 6,468
Tuna mtukufu sana wa karne ya 21 yupo Tz anaitwa sizonje yy hadi ana malaika wanaoshuka akiomba kuja kuzima hata social networksView attachment 466257
“And I say to you, I have also decided to stick to love. For I know that love is ultimately the only answer to mankind's problems. And I'm going to talk about it everywhere I go. I know it isn't popular to talk about it in some circles today. I'm not talking about emotional bosh when I talk about love, I'm talking about a strong, demanding love. And I have seen too much hate. I've seen too much hate on the faces of sheriffs in the South. I've seen hate on the faces of too many Klansmen and too many White Citizens Councilors in the South to want to hate myself, because every time I see it, I know that it does something to their faces and their personalities and I say to myself that hate is too great a burden to bear. decided to love.”
Namtafakari sana huyu ndugu Martin Luther King JR. maisha yake namna alivyoishi na watu wa rika zote na kujitoa katika kupigania haki za watu weusi huko Marekani(USA).
Dr. Martin Luther King JR. alikuwa ni mchungaji/pastor na mwanaharakati kiongozi wa Civil right movement na wachambuzi wa mambo mbalimbali wanasema huyu ni mtu mwenye uwezo mkubwa sana akiwa anahutubia watu na kujenga hoja, kushawishi watu wanaomsikiliza na hakika katika karne ya 21 hajatokea mwingine zaidi yake duniani.
Falsafa yake ya passive na non violent resistance, misimamo yake thabiti ya kile anachokiamini na hasa upendo wake kwa wengine vilimfanya awe kipenzi cha wengi.
Hotuba zake nyingi zipo mtandaoni tafuta hii inayoitwa
- BEYOND VIETNAM,
- THE OTHER AMERICA,
- THE CASUALTIES OF THE VIETNAM WAR,
- I've been to the mountaintop nk,nk,nk.
Nyingine hii alipanga kuitoa lakini aliuawa kabla ya kuhutubu,
- Why America May Go to Hell.
Ninapomtafakari huyu mwanaharakati akiwa kama binadamu mimi binafsi sioni madhaifu yake, yani kama tulivyo binadamu wengi tuna mapungufu kama chuki dhidi ya wenzetu, sifa, tamaa, hasira, wivu, kulipa visasi, wagumu kusamehe, wabinafsi na tunapenda sana ukuu au madaraka/mamlaka na mengine mengi sana.
Sasa Martin Luther King JR. naona tu zile hulka zake nzuri daima inawezekana humu wapo wanaomfahamu vizuri huyu mtu zaidi nimjuavyo kwa mapungufu yake kama kweli yapo waeleze hapa ili tuyafahamu .