Binadamu hapaswi kutawala, anaongoza

Binadamu hapaswi kutawala, anaongoza

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
761
Reaction score
6,985
Nimemsikia mzee kwa muda sasa akiomba nafasi ya kututawala, nikajiuliza ni kweli tunataka mtu wakututawala?

Vitabu vitakatifu vinaeleza wazi kuwa binadamu apewa mamla ya kutawala wanyama na vyote vilivyomo juu ya ardhi.

Binadamu Hana mamlaka yakumtawala binadamu mwenzake kwa sababu zifuatazo:

1. Ukitawala unajipa mamlaka yote juu ya ulochokitawala ikiwemo kuchinja, kula, kung'o na kukiaribu pale unapojisikia.

2. Kinachotawaliwa hakina haki yoyote juu ya yule anayekitawala.

3. Kinachotawaliwa hakina mamlaka ya kuchagua wakukitawala bali mtawala uamua namna ya kukitawala.

Je, ni sahihi kuomba wananchi wakutuhusu kuwatawala? Kwa msingi wa hoja namba tatu hapo juu, anayetaka kutawala haitaji ridhaa ya wale anaotaka kuwatala. Kisiasa, anayetaka kutawala hana sababu yakuheshimu Wala kusikiliza sauti ya anaotaka kuwatawala. Ujiamulia yeye lini na kwa njia gani awatawale.

Je, kwa msingi wa kisiasa tunahitaji kumpigia kura mtawala?
Hapana, Kama tukipata fursa ya kuchagua mtu wakutuongoza hatuhitaji kumchagua mtawala tunapaswa kumchagua kiongozi atakayesimamia maono yetu akiyapa tafsiri sahihi.

Shime kwa wanasiasa msiombe kututawala na msitutawale ombeni kutuongoza. Wakoloni walitutawala tukaomba Uhuru tujiongoze siyo tujitawale.
 
Mungu pekee ndiye hututawala na Kutuongoza.

Binadamu hana uwezo wa kutawala wala kuongoza binadamu mwenzie.

Binadamu ana uwezo wa kumtumikisha na kumuamrisha binadamu mwezie, na si kumtawala wala kumuongoza.
 
Huu ni utawala badala ya kuongoza. White colonialism was far better kuliko huu balck man colonialism. kinachoendelea tz sasa ni dola kuwatawala wananchi wake badala ya kuwaongoza.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom