BIN ZUBERY sasa anavuka vipaka. Anapata kiburi wapi kusema haya. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

BIN ZUBERY sasa anavuka vipaka. Anapata kiburi wapi kusema haya.

Discussion in 'Sports' started by adakiss23, Aug 12, 2012.

 1. adakiss23

  adakiss23 JF-Expert Member

  #1
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 3,265
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
 2. Daudi Mchambuzi

  Daudi Mchambuzi JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 30,187
  Likes Received: 32,726
  Trophy Points: 280
  [h=3]SIMBA KUMKOSA MBUYU TWITE, RAGE ANASTAHILI LAWAMA[/h]

  MWENYEKITI wa Simba SC, jana amekaririwa na vyombo vya habari nchini akimshutumu mtoto wa kigogo kimoja nchini kumshinikiza Rais wa APR ya Rwanda, Meja Alex Kagame ampeleke Yanga, beki Mbuyu Twite, wakati alikuwa amekwishasaini Simba na kupewa fedha.
  [TABLE="class: tr-caption-container"]
  [TR]
  [TD="align: center"][​IMG][/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD="class: tr-caption, align: center"]Na Mahmoud Zubeiry[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  Rage amelalamika sana na akapiga hatua kubwa zaidi, akaanza kuwakashifu viongozi wa Yanga, wana fedha chafu za EPA.
  Yote haya yanakuja baada ya kuzidiwa kete katika kuwania saini ya Twite. Namfahamu Rage na hii ndio desturi yake. Anapopandisha jazba huweza kusema lolote, bila ya kujali chochote.
  Kabla ya kuzungumzia sakata la mchezaji huyo, nianze kwa kumuelewesha tu Rage, asitazame boriti kwenye jicho la wapinzani wake, Yanga akasahau kibanzi kilichopo kwenye jicho lake.
  Rage anafahamu fika, mambo ambayo yako mahakamani huwa hayajadiliwi nje ya Mahakama na hakuna asiyefahamu kwamba suala la wizi wa fedha kwenye Akaundi ya Madeni ya Nje (EPA), lilifikishwa mahakamani na baadhi ya waliokutwa na hatia, hivi sasa wanatumikia kifungo jela.
  Na hivi karibuni, rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete alipokutana na Wahariri wa vyombo vya Habari nchini, Ikulu mjini Dar es Salaam, amerudia kusema juu ya hilo, kwamba serikali haimlindi yeyote na ilizikabidhi mamlaka husika zichukulie hatua hilo na kwa kuwa mamlaka hizo ni huru, hawawezi kuziingilia.
  Sasa inakuwa jambo la ajabu, Rage anapothubutu kumuhukumu mtu mwingine nje ya Mahakama juu ya EPA.
  Ni sawa tu na leo hii, atokee mtu aanze kumzungumzia yeye kuhusu dola 40,000 za Yanga za mwaka 1998 alizochukua CAF (Shirikisho la Soka Afrika) au tuhuma nyingine lukuki za ubadhirifu wa mali za Chama cha Soka Tanzania (FAT, sasa Shirikisho, TFF), atakuwa hamtendei haki, kwa sababu Mahakama ilikwishaamua.
  Awali, Rage alihukumiwa kifungo jela, kabla ya kutoka kwa msamaha wa Rais, baadaye akaenda Mahakama ya Rufaa, kukata rufaa kupinga hukumu hiyo, akafanikiwa, mahakama ikamsafisha na ndio maana leo ni Mbunge na Mwenyekiti was Simba, vinginevyo asingeweza kupata haki ya kugombea hata Ukatibu Kata.
  Naomba niwaombe radhi wasomaji wangu na Rage pia, kwa kukumbushia suala la dola 40,000 na kifungo cha Rage kabla ya kutoka kwa msamaha wa Rais, kwa kuwa natambua si busara kuzungumzia mambo ambayo yamefikishwa Mahakamani.


  MTOTO WA KIGOGO;
  Hajamtaja jina, lakini dhahiri hapa anazungumziwa Ridhiwani, mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Nani asiyejua kama Ridhiwani ni Yanga na Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na sidhani kuna dhambi katika hilo, ikiwa Waziri Mkuu wa zamani, ‘Simba wa Vita', Mzee Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Simba.
  Simba na Yanga ni timu za Watanzania, na ndio maana Profesa Juma Athumani Kapuya, Rage mwenyewe, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Zitto Kabwe, Iddi Azzan na wengine miongoni mwa vigogo wa nchi yetu ni Simba.
  Kama Ridhiwani alijaribu kuisaidia Yanga, timu yake kuna dhambi gani, ikiwa mwaka 2005 Kapuya aliisaidia timu yake, Simba SC kutompoteza beki Victor Costa, ingawa alikuwa amesaini Yanga na kupewa fedha?
  Mimi namheshimu rais wetu, Kikwete na sidhani kama ana muda wa kushughulika na ‘upuuzi' wa Simba na Yanga- lakini kama mzazi pia ambaye anatambua Ridhiwani kijana wake naye ni baba wa familia pia, ana uhuru wake katika mambo yake. Hawezi kumuingilia.
  Yanga imepitia wakati mgumu na Kikwete yupo pale pale Ikulu na hajaonyesha hata dalili za kutaka kuwasaidia Yanga. Kikwete akiwa Ikulu, alileta kocha kwa ajili ya timu ya taifa, turudi enzi zile Rage na Samuel Sitta wakiwa CDA, walilitumia shirika hilo kwa manufaa ya timu ya taifa au Simba? Watu wanakumbuka haya mambo ndio maana namtahadharisha Rage, asiangalie boriti kwenye jicho la wapinzani, wakati jicho lake lina kibanzi.
  Mambo ya kuchafuana si mazuri na yamepitwa na wakati- Rage kama ameamua kuwa Mwenyekiti was Simba, basi apambane na changamoto zote bila ya kumnyooshea mtu kidole na kwa kweli umefika wakati Rage aachane na ‘Saisa za Majitaka', kwanza hata umri wake tu haumruhusu tena kufanya mambo kama hayo, amekwishakuwa mtu mzima sasa.
  Huyo Ridhiwani kama ndio staili yake hiyo kutisha watu, kwa nini asianzie hapa nyumbani kuwatisha viongozi wa Azam katika suala la Mrisho Ngassa wampeleke Yanga? Rage amewahi kupewa onyo kali na TFF kwa kosa la kutoa kauli za uchochezi na ajabu hajaacha, kwani kauli zake dhidi ya mtoto wa kigogo ni za uchochezi. Ni za hatari.


  SAKATA LA MBUYU TWITE
  Kama kuna mtu wa kwanza wa kulaumu juu ya Simba kumpoteza Mbuyu Twite, basi ni Aden Rage. Kwa nini? Alipofika Kigali, baada ya kumpa fedha beki huyo na kumsainisha mkataba, alijua fika na Yanga nao wanamfuatilia mchezaji huyo.
  Yanga wale wale, waliomchukua Kevin Yondan na kumsainisha mkataba, wakati tayari amesaini mkataba (kwa mujibu wa Simba) wa kuendelea kuichezea klabu yake, Simba SC.
  Ajabu Rage akijua kabisa, Yanga si waungwana, akamuacha Twite Kigali, yeye akawahi Mkutano Mkuu na baadaye shughuli za Bunge, huku nyuma Yanga wakafanya ambacho kinamsababisha leo yeye azungumze huku mapovu yanamtoka mdomoni.
  Rage alitakiwa arudi Dar es Salaam na Mbuyu Twite, apokewe na maelfu ya wana Simba halafu tungeona kama angethubutu kusaini Yanga. Rage pamoja na uzoefu wake wote katika masuala ya usajili na fitina za mpira, hapa alichemka na badala ya kutafuta mchawi, ni vema akajilaumu mwenyewe.
  Nimependa alivyomalizia mazungumzo yake jana, alisema wao watatafuta mchezaji mwingine mzuri na anachoomba tu, Simba warudishiwe fedha zao, kiasi cha dola 40,000 hivi, pamoja na gharama za nauli, kwake, mchezaji mwenyewe na mawakili waliotayarisha mkataba aliosaini Twite. Safi.


  TUACHE UHUNI KATIKA SOKA YETU:
  Soka yetu imegubikwa na mambo ya kihuni, ambayo wenyewe wanayaita ya kimjini, ambayo siku zote mimi tangu nipo DIMBA, kuanzia Mwandishi hadi Mhariri, nilikuwa nayapinga vikali, kwa sababu najua athari zake ni kuididimiza soka yetu.
  Leo Simba wakilia kuhusu Twite, Yanga watawaambia; Mnakumbuka Costa? Na bado historia inaanzia mbali tangu ya 1960, Simba na Yanga zilikuwa zinapokonyana wachezaji.
  Ila katika dunia ya leo, inayotawaliwa na utaalamu, taratibu, kanuni na sheria, kwa nini tuendelee kuyalea mambo kama haya?
  Siyo tu sijapendezewa na staili waliyoitumia Yanga kumsajili Twite, lakini pia sijapenda staili waliyotumia Simba kumsajili Ramadhan Chombo ‘Redondo', ambayo leo inawaliza Azam.
  Huo ni upande mmoja, upande wa pili, kuhonga wachezaji wa timu pinzani na marefa- hili pia silipendi na ni sehemu ya uhuni, ambao unapoteza maana halisi ya soka ambayo FIFA wanaitaka. Soka ya kiungwana. Hayo yalikuwa mapitio tu, leo ujumbe wangu ulikuwa Mh. Alhaj Rage; asikumuke EPA tu, kuna dola 40,000 za Yanga, je watu wakumbushie hizi? Nawatakia saumu njema na kwa ujumla mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhan inshaallah.
   
 3. Ukwaju

  Ukwaju JF Bronze Member

  #3
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 8,104
  Likes Received: 630
  Trophy Points: 280
  Sasa inakuwa jambo la ajabu, Rage anapothubutu kumuhukumu mtu mwingine nje ya Mahakama juu ya EPA.
  Ni sawa tu na leo hii, atokee mtu aanze kumzungumzia yeye kuhusu dola 40,000 za Yanga za mwaka 1998 alizochukua CAF (Shirikisho la Soka Afrika)

  Awali, Rage alihukumiwa kifungo jela, kabla ya kutoka kwa msamaha wa Rais, baadaye akaenda Mahakama ya Rufaa, kukata rufaa kupinga hukumu hiyo, akafanikiwa, mahakama ikamsafisha na ndio maana leo ni Mbunge na Mwenyekiti was Simba, vinginevyo asingeweza kupata haki ya kugombea hata Ukatibu Kata.


  MTOTO WA KIGOGO;
  Hajamtaja jina, lakini dhahiri hapa anazungumziwa Ridhiwani, mtoto wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete. Nani asiyejua kama Ridhiwani ni Yanga na Mjumbe wa Kamati ya Uchaguzi ya Yanga na sidhani kuna dhambi katika hilo, ikiwa Waziri Mkuu wa zamani, ‘Simba wa Vita’, Mzee Rashid Mfaume Kawawa alikuwa Simba ndio maana Profesa Juma Athumani Kapuya, Rage mwenyewe, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye, Zitto Kabwe, Iddi Azzan na wengine miongoni mwa vigogo wa nchi yetu ni Simba.

  Kama Ridhiwani alijaribu kuisaidia Yanga, timu yake kuna dhambi gani, ikiwa mwaka 2005 Kapuya aliisaidia timu yake, Simba SC kutompoteza beki Victor Costa, ingawa alikuwa amesaini Yanga na kupewa fedha?
  Mimi namheshimu rais wetu, Kikwete

  mm naanza kuwa na Mashaka na weledi wa Rage hata km ni mshabiki wa Simba lakini uongozi wa huyu jamaa toka alipokuwa hapa CDA siuamini na haja majuzi kati wakati kafunga Ramadhani alipomuita Mbunge mwenzake FOOL
  Hizo hasira zitajamgeukia na sio uungwana km mwenzake kamzidi hiyo hela je akilipwa na huyo Ridhi 1 atatutangazia?
   
 4. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #4
  Aug 12, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  ukisoma mfululizo wa makala yake tangu kipindi cha uchaguzi wa yanga alivyokuwa akiwanadi hasa Manji na Ben Kleb, pia alivyokuwa akiandika kuhusu Ngasa kwenda Simba na nafasi ya Azam kumchukua tena Ngasa, pia jinsi alivyokuwa wa kwanza kuandika kwamba Simba kupitia Rage walimpa Twite dola 10,000 tofauti na kauli ya Rage ya kumpa dola 30,000 na gharama zingine zinazofikia sasa Dola 39,000 na laki kadhaa, na zaidi ukifuatilia kauli ya Rage jana kuhusu kilichotokea na leo anamtaja Ridhiwani na zaidi kumshambulia Rage. Anafika mbali zaidi na kuongelea mambo ya EPA kama vile na yeye siku hizi ana uelewa wa mambo ya kisiasa tofauti na makala yake anayoandika siku zote.Utaweza kugundua kitu kimoja tu kwamba huyu jamaa Bin Zubeiry anajichanganya sana na yeye mwenyewe ndiyo anatokwa na mapovu tofauti na anavyotaka watu waamini.

  Jana aliandika kwa hakika kwamba Rage au Simba walimpa Twite dola 10,000 tu na leo anakubaliana na kiasi alichotaja Rage jana cha dola 39,000, na anahitimisha kwa kuandika SAFI SANA. Pia anajenga hoja yake katika historia hafifu ya Victor Costa na sasa anasema kwamba Rage alaumiwe kwasababu gani alimuacha Twite Rwanda badala ya kuja naye moja kwa moja. Haoni sababu ya Rage kuwahi mkutano mkuu wa Simba na badala yake angerudi na Twite mkononi. Anajaribu kuonyesha kwamba kwake mkutano mkuu ilikuwa vemaifanyike bila mwenyekiti na yeye aendelee kumsubiri Twite aje naye kwasababu Yanga nao wanamfuatilia huyo mchezaji.

  Bin Zubeiry inaelekea haelewi nini maana ya mkataba ambao umesainiwa kwa kuzingatia taratibu zote. Pia inaonekana haelewi ingemchukua Twite siku ngapi kukamilisha mambo yote, kwani anakuja kazini nchi nyingine, mazingira tofauti, n.k, hivyo alipaswa akaweke mambo yake sawa ikiwa ni pamoja na mambo ya familia na taratibu za safari kama hati zinazohitajika. Ndiyo maana Rage alitumia gharama zingine ya dola 9,000 nje ya dola 30,0000 alizokabidhiwa Twite ila akamilishe taratibu zote na aje ajumuike na wenzake Dar. Huyu mwandishi hawezi kutuhaminisha kwamba hilo ni kosa kwa Simba wakati tayari mchezaji ameingia mkataba na klabu na ameshapewa haki yake.

  Bin Zubeiry haonyeshi uelewa hata kidogo kuhusu taratibu za kiuhamisho na mambo ya mkataba, ndiyo maana anaonekana kuunga mkono uhuni uliofanywa na Yanga, na hapa nashawishika kwamba hawezi kufanya hivi parsonal attack kwa Rage na zaidi fuatilia makala yake siku zote kuhusu Simba utaona kwamba ana maslahi binafsi katika haya yanayofanywa na viongozi wa Yanga. Kama ni makosa Rage kumuacha Rwanda kama anavyotaka tuamini, basi ni kwanini hao yanga anaowafagilia nao bado wamemuacha huko huko na hawajamleta Tanzania?

  Katika sakata hili, naweza nikaona hatari zaidi kwa huyu mchezaji, japo yeye kwa akili yake na tamaa zake binafsi na kwa kudanganywa na viongozi wa Yanga hakuweza kuona hilo. Huyo mchezaji anawafanyia Simba Uhuni kiasi hicho na bado anakuja kufanya kazi Tanzania, tena Dar es Salaam, sipati picha kuhusu hali ya ulinzi atakaopewa na klabu yake mpya ya Yanga kwa kipindi chote cha mkataba wake na mazingira atakayoishi, na kwa msingi huo Yanga watalazimika kutumia gharama kubwa sana. Na uhakika wa hizo pesa chafu za viongozi au mtoto wa kigogo ambaye kwa hakika simjui, nahisi hauko mbali sana, kwani mwaka 2015 kuna mabadiliko makubwa sana na hakika Tanzania itaanza historia mpya na hata wahujumu uchumi waanze kujiandaa kwenda THE HAGUE.
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 9,752
  Likes Received: 4,620
  Trophy Points: 280
  Rage ametoka povu na akatoa mchozi kidogo!jamani kweli mzee wa watu anaipenda Simba,duuu hapo tu anagombea mchezaji ...kazi ipo! Namshauri ajipange sawa sawa maana uchaguzi wa Tabora Mjini waja soon na anaweza asipite kwenye kura ya maoni...na pia ajipange wana Tabora wamekata tamaa na maisha yao ya kila siku,hakuna fursa za ajira vijana woote wameishia kuvuta bangi na kuwa fundi magari ingawa mkoa una shule nyingi sana za maana za sekondari ....lile wimbi la wale vijana ndio litamtesa sana pale mjini
   
 6. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2012
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,280
  Likes Received: 922
  Trophy Points: 280
 7. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #7
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,700
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Hii ni moja ya sababu inayonifanya nimkubali sana huyu (Jamaa Bin Kleb),the guy is so intelligent.
   
 8. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2012
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,454
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Mkuu wewe ni wa hapo Tabora?
   
 9. KANYIMBI

  KANYIMBI JF-Expert Member

  #9
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 260
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Nikiziangalia hizi timu zote mbili Simba na Yanga. Ni dhahiri kuwa Simba ndio waliokuwa na shida hasa ya kuwa na huyu beki Twite. Wanachokifanya yanga ni ili kuwakomoa viongozi wa simba huku wakijua wazi hawana uhitaji huo. Binafsi ninamashaka sana juu ya usalama wa huyu Twite kama ni kweli atachezea Yanga. Mimi binafsi liwahi kuvaa shati la njano na kukatiza kwenye jukwaa la Simba pale uwanja wa Taifa lakini kilichonikuta ni siri yangu ila sitokuja kurudia tena.
   
 10. The Magnificent

  The Magnificent JF-Expert Member

  #10
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 2,666
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Na mimi nimuongelee kidogo huyu BIN ZUBEIR…
  Kwanza siamini kama ni mwandishi wa habari aliyehitimu na kutunukiwa kitu Fulani(either cert,dip au shahada) kwa sababu katika blog yake ameonekana ni mtu wa kuandika habari kishabiki zaidi(as if inasomwa na watu wa upande mmoja,nafananisha habari zake na habari zinazoandikwa na gazeti la UHURU,ambazo huwa zimelenga wasomaji wafuasi wa CCM na sio wananchi wote kwa ujumla)
  Sina haja ya kumshauri aiandike anavyotaka kuandika….la hasha,,huyu mwandishi ana maslahi yake binafsi kwa anachokiandika na anafanya MAKUSUDI tu na bila kutafuna maneno nahisi huyu jamaa anatumiwa…..
  Imefika wakati sasa sfuatilii tena blog yake kwa sababu habari zake nyingi hazina uhakika,(mfano,jana aliandika kuhusu twite kupewa dola 10000 na leo mtu huyu huyu anaandika kapewa 30000 baada ya press ya bw.Rage ya jana…uandishi wake umekaa kinazi nazi sana mpaka anaboa……)
  Nawashauri wale wadau wa michezo walio Neutral kama mimi…kama unahitaji habari ambazo atleast hazijakaa kishabiki,bora utembelee blog ya shaffih dauda,japokuwa sikatai kuwa nayo sio efficient for 100% lakini angalau jamaa hana ushabiki wowote katika uandishi wake……


  I STAND TO BE CORRECTED. The Magnificient
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #11
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,700
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha ha
  Embu wadau wa michezo walio neutral kama the magnificient pateni baadhi ya habari zisizoegemea upande wowote kutoka kwa blog pendekezwa na Mdau (Blog ya TSC):-
  Shaffih Dauda in Sports.: HIVI NDIVYO ADEN RAGE ALIVYOWAPIGA BAO YANGA NA KUMSAINI MBUYI TWITE
  Shaffih Dauda in Sports.: SUALA LA KELVIN YONDANI KUCHEZA KAGAME NA UTATA WAKE WA KIKANUNI: IWEJE YEYE ARUHUSIWE KUCHEZA WAKATI KISIGA NA EMMANUEL GABRIEL WALIZUIWA?-

  Naomba niweke hizi mbili tu kwa leo.
   
 12. The Magnificent

  The Magnificent JF-Expert Member

  #12
  Aug 12, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 2,666
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  ok,sawa....sioni ubaya wowote hapo,au kwa kuwa amiongelea simba?
  Duh!! nna mashaka sana na upeo wako wa kufikiri
   
 13. Anselm

  Anselm JF-Expert Member

  #13
  Aug 12, 2012
  Joined: Nov 16, 2010
  Messages: 1,700
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Eti?.....basi Kaka tusibishane,wacha nikubali upeo wangu wa kufikiri una walakini,hakuna tatizo kabisa katika sample 2 hizo za habari.
   
 14. M

  Mahongole Member

  #14
  Aug 12, 2012
  Joined: May 5, 2009
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mpira wa miguu umeaibishwa. TFF wanalipalilia hili na tutegemee kuona madudu ya ajabu kwenye ligi. Kama wamesogeza mbele tarehe ya usajili ili kufurahisha timu waipendao si ajabu wakapangiwa marefa wa kuchezesha ligi. Aibuu!
   
 15. C

  Chipolopolo JF-Expert Member

  #15
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 876
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Bin Zubery?Waandishi wanazi wa aina yake ni hatari sana. Pengine ana ndoto za kuwa msemaji wa Yanga, amrithi Sendeu?Who knows??
   
 16. M

  Masuke JF-Expert Member

  #16
  Aug 12, 2012
  Joined: Feb 28, 2008
  Messages: 4,604
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 160
  Mimi nimesoma hiyo makala leo nikaishiwa nguvu, nashukuru nilikuwa na bundle langu toka kwa wakoloni, lakini huyu jamaa bora angekuwa anaripoti kuliko kujaribu kuweka analysis zake za ajabu ajabu, halafu anasema alikuwa mwandishi na mhariri, jamani watu kama hawa sijui wanasoma shule gani maana hata mimi kipindi niko form two nisingeweza kujichanganya hivyo kama alivyojichanganya huyo jamaa.

  Anaongelea habari za Sarungi na Kapuya kuibeba Simba, hataki kueleza ni katika mazingira gani hawa jamaa waliibeba Simba, Ishu ya Victor Costa Yanga ndio walikuwa wachokozi hivyo Kapuya alifanya jambo la maana kumidhinisha achezee Simba.
   
 17. B

  Baba Kiki JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2012
  Joined: May 31, 2012
  Messages: 1,327
  Likes Received: 461
  Trophy Points: 180
  Bin Zubeiry - una safari ndefu sana ya kuwa mchambuzi makini. Fact zako na mifano yako ni ya kitoto sana. Criticism dhidi ya Rage haina mashina na iko ki personal zaidi. Kwa ufupi haujawatendea haki wasomaji wako.

  Mwandishi kama wewe jua una wajibu wa kufanya uchambuzi ambao unakuwa neutral kiasi cha kushawishi hata asiyekubaliana na wewe kimtazamo, akubaliane na wewe hata katika data baadhi. TOO SHALLOW BROTHER, SORRY
   
 18. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,639
  Likes Received: 222
  Trophy Points: 160  ndetichia like this
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. Bwana Mapesa

  Bwana Mapesa JF-Expert Member

  #19
  Aug 12, 2012
  Joined: Apr 28, 2011
  Messages: 1,849
  Likes Received: 627
  Trophy Points: 280
  kuna kitu kitaaluma kinaitwa "BLACKOUT PROJECT" hii inatumika kwenye sekta ya uandish kama njia ya kuwazuga watu kutoka kufikiria jambo fulan muhim na ku divert mind zao kwenye jambo lingine..sasa hawa kina BIN ZUBEIRY Ndo Agents wa hii project..wanakuwa paid monthly kwa kutoandka madudu na ufisadi ili wananch walale.wewe huwez kuwa mwanahabar wa michezo uliyetimia ukashindwa kuona uharamu wa timu kumshawish mchezaji aliye ndani ya mkataba na timu nyingine?let alone Yondan,kuna Ishu ya Kapombe,Ngassa,OKWi wote wamethbitisha kufuatwa na viongoz wa Yanga wakat wanamikataba halali na SIMBA,he still attack on Rage..leaving behind oll these fu***ckn tricks wanacheza viongoz wa Yanga.UKWELI NI HIVI BIN ZUBEIRY ANAJUA ANACHOFANYA SABABU YUPO KWA AJILI YA WATU FLANI FLANI AMBAO WANAMFANYA AVIMBE TUMBO KISHA AENDE CHOONI.
   
 20. m

  matambo JF-Expert Member

  #20
  Aug 12, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 728
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  mimi nilisema janahapa huyu jamaa anaandika kinazi sana, akatokea mtoto hapa anaitwa Anselm nae ana u majununi uleule akaanza kumtetea, lakini haina shida wanawatumkia mabwana zao waliowatuma
   
Loading...