KndNo1
JF-Expert Member
- Oct 26, 2021
- 627
- 2,025
- Thread starter
- #641
Aisee hiyo ADK inaweza kuwa gari ya Jumapili.. Kusema ipo tangu namba A sio ishu.. Kilometers za engine hazipimwi kwenye namba au mwaka.. Dashboard ndio kila kitu.. ADK dashboard inasoma ngapi..!!?Kuna gari ina 2000cc namba ADK ni nzima na kuna gari 4500cc ipo juu ya mawe. Na kuna gari nyingi tu za namba A na B zinadunda mitaani, kwanini hazijafa?
Usipotunza gari yako kama inavyotakiwa hata iwe na cc 13,000 lazima ife.
Ukizitunza zote lazima zitadumu mpaka either body ife au uamue kuiuza scrapper.
Nini kinafanya engine ya 900cc inayotunzwa vile inavyotakiwa ife? Yani unaamka asubuhi gari imejifia tu? Kuna gari namba D engine imeshaanza kukongoroka na ingine namba B engine bado inadai. Zote 2500cc.
Kuna huyo alifikisha 500k kwenye 1.6l engine. Hiyo ni engine kubwa?
BTW, kukariri engine codes hakukufanyi uwe mtabe, experience na simple reasoning inaweza ikakushinda vilevile.
Iwe inapiga masafa isingekuwepo..
Sasa hayo ndio maswali ya msingi ya kuuliza.. Engine inakufaje..!
Engine ndogo kwenye same chassis na engine kubwa kinachotokea ni kwamba itabidi ifanye kazi ya ziada kupush same car..
Movements za engine ndio mwanzo wa engine kuwear n tear.. Piston na block wall ya engine ndogo itasagika zaidi ya engine kubwa sababu you need kuipush engine ndogo zaidi kupata results ya engine kubwa.. Engine kubwa zina advantage inaproduce power effortless..! Rpms ndogo kwenye engine kubwa inatoa power kuliko same rpms kwenye engine ndogo..!
Huko ndio kufa kwa engine.. Piston na block ya engines ndogo haiwezi kulast kama mashine kubwa..!
Huyo aliyefikisha hizo kms kwenye hiyo gari ni mmoja kati ya wengi..
Usisahau knowledge is power..!
Yes experience na simple reasoning umeshindwa kuelewa engine ndogo ina life span ndogo..!!!
Pikipiki ya 150cc na 250cc blocks zake zitalast sawa..!!!? Hizi ndio simple reasoning..!