Bima ya Afya

Mimi ni mmoja wa familia ninayetumia kadi ya bima ya taifa, lakini chakushangaza huduma ya bure niliyoiona ni kua niliandikiwa dawa lakini dawa nilizopewa bure kupitia bima hii ya taifa ni Paracetamol lakini dawa nyingine nikaambiwa nikanunue!

Mnanishauri nini?
Kaka Ndallo kuna fomu ulitakiwa ujaziwe kwenye hicho kituo ulichokosa huduma ukachukue hizo dawa kwenye duka ambalo limesajiliwa na NHIF, kila kituo cha matibabu ambacho kimesajiliwa na Mfuko huo kinatakiwa kuwa na fomu hizo wakiwa hawana dawa lazima ujaziwe ili ukachukue dawa ulizokosa kwenye pharmacy au duka la dawa muhimu lililosajiliwa na Mfuko!!
 
Kaka Ndallo kuna fomu ulitakiwa ujaziwe kwenye hicho kituo ulichokosa huduma ukachukue hizo dawa kwenye duka ambalo limesajiliwa na NHIF, kila kituo cha matibabu ambacho kimesajiliwa na Mfuko huo kinatakiwa kuwa na fomu hizo wakiwa hawana dawa lazima ujaziwe ili ukachukue dawa ulizokosa kwenye pharmacy au duka la dawa muhimu lililosajiliwa na Mfuko!!
Asante Karikenye! Ngoja niugue tena halafu nifuate ushauri wako.
 
Mimi ni mmoja wa familia ninayetumia kadi ya bima ya taifa, lakini chakushangaza huduma ya bure niliyoiona ni kua niliandikiwa dawa lakini dawa nilizopewa bure kupitia bima hii ya taifa ni Paracetamol lakini dawa nyingine nikaambiwa nikanunue!

Mnanishauri nini?

kuna kadi aina mbili au tatu,kuna green na yellow,blue,kama sijakosea,mimi ni green,na siongezi ki2,nahudumiwa daraja la kwanza,
 
Simpotoshi. Unajua kama una kadi ya bima lazima upate huduma first class bila ubaguzi wowote. Anyway labda experience yako tofauti na yangu. Tena mimi nina green card na ninakatwa hela nyingi sana kwa mwezi lakini huduma za hospitali si nzuri.
wacha kumpotosha mwenzako. wengine wana kadi hiyo ya nhif na wanaishukuru kila kukicha. mwacho aipate ajionee mwenyewe. akishindwa atahamia hizo zingine.
 
nenda kurasini kwenye makao makuu yao watakupa utaratibu mzima. iwapo unatokea kariakoo shuka kurasini get na.3 hapo utaziona ofisi zao
 
Nina experience mbaya sana na hii Bima pamoja na kuwa nakatwa hela nyingi sana. Sipati value for money. Ila mtu kama anataka bora kwenda hospitali tu bila huduma bora it is ok. Mie nataka huduma bora maana wanachukua hela zangu nyingi sana. Kama unakaa hospitali hours bila huduma ya maana utasemaje?

kama matibabu ni expensive mpaka uende ukaombe upewe kibali. Naomba nini wakati wana hela zangu? Mbona hela zetu wanachukua tu hawaombi kibali kwetu? hii experience niliyoipata nawe utaipata tu siku moja halafu utakubaliana na mimi. Hapa naongelea magonjwa sugu sio magonjwa madogo madogo. Haya mbona hayana shida!!!!
wacha kumpotosha mwenzako. wengine wana kadi hiyo ya nhif na wanaishukuru kila kukicha. mwacho aipate ajionee mwenyewe. akishindwa atahamia hizo zingine.
 
Nina experience mbaya sana na hii Bima pamoja na kuwa nakatwa hela nyingi sana. Sipati value for money. Ila mtu kama anataka bora kwenda hospitali tu bila huduma bora it is ok. Mie nataka huduma bora maana wanachukua hela zangu nyingi sana. Kama unakaa hospitali hours bila huduma ya maana utasemaje? kama matibabu ni expensive mpaka uende ukaombe upewe kibali. Naomba nini wakati wana hela zangu? Mbona hela zetu wanachukua tu hawaombi kibali kwetu? hii experience niliyoipata nawe utaipata tu siku moja halafu utakubaliana na mimi. Hapa naongelea magonjwa sugu sio magonjwa madogo madogo. Haya mbona hayana shida!!!!

magonjwa gani NHIF hayatibii? umekwenda wapi? kama vipimo vya MRI siku hizi kupitia bima ya afya vinatolea kama njugu mawe, wagonjwa wa cancer na kisukari wanatibiwa wewe usitibiwe kwa nini? je ulienda sehemu sahihi.

vibali vinavyozungumzwa hapa kwa magonjwa makubwa ni utaratibu tu ambao ukiufwata vyema unapata matibabu yako. na vibali vimewekwa baada ya watoa huduma kutoa vipimo hivi na huduma na dawa hizi ambazo ni gharama bila mpango huku wakijipatia faida bila sababu za msingi lakini kama kweli unastahili na umeandikiwa na daktari na ugonjwa ulio nao unahitaji kupewa dawa au kufanya kipimo fulani NHIF wanakupa hiyo huduma.

swala la kukaa hospitali kwa muda mrefu si tu kwa sababu una NHIF card mimi ninayo kadi hiyo na kadi ya jubilee ya mume wangu, nikitumia yoyote kati ya hizi foleni ipo palepale, kero ndogondogo na hata wakati mwingine kubwa zipo pale pale. hivyo tatizo lipo mahospitalini sio kadi fulani.

nakushauri, kama kweli unatumia NHIF kwa utaratibu sahihi utapata mahitaji unayoyataka. mengine hayo yapo tu.

mimi nilitumia kadi ya jubilee kupata miwani nilikaa wk 2 hadi sijui wapige simu head office ya jubilee waone kama miwani hiyo haijapia kiwango cha fedha zilizopangwa na mambo kadha wa kadha.
nilishawahi kutumia strategies card, wao ndio kabisa unaambiwa unaweza kutibiwa hadi ugonjwa fulani tu mengine kadi yako haikuruhusu.

NHIF card inatubeba sana mengine ni changamoto za kimifumo tu.
 
Mimi ni mwanachama na nimekuwa nikifaidika na Bima ya Afya Tangu mwaka 2002 na nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mafao ya hawa jamaa. Kitaalamu NHIF au Bima ya afya wanatumia system inayoitwa FEE FOR SERVICE ambayo hakuna kikomo cha gharama kwenye matibabu na unaweza kupata huduma wewe na wategemezi wako watano kwa maana ya wewe,mwenzi wako wa ndoa,watoto wako na wazazi wakoau hata wakwe zake na kuwa na jumla ya wanufaika sita na wote mnapewa vitambulisho ambavyo unaweza kupata huduma popote Tanzania kwenye hospitali zote za serikali,mashirika ya dini,za watu binafsi na na pia wamesajiri pharmacy ili ukienda na kukosa dawa kwenye hospital unapewa form ya kwenda kuchukua dawa.

Na gharama ya kujiunga kwa mtu binafsi ni Tshs 964,800 na unapaswa tu kuandika barua kwao na kuwa na wadhamini wawili ambao ni wanachama wa NHIF. Hao wanaokushauri kwenda Private Insurance ni kwamba wao wana tumia capitation Method ambayo ina ceiling limit ya cost za matibabu na wana pima Health status ya wanachama wake na especially kama una mtu mwenye clonic desease wanamkataa hasa kansa,kisukari,figo wakati bima ya afya wao wanasema Organisation yao haiku katika misingi ya kibiashara wala lengo la kutengeneza faida bali kutoa huduma.

Kwa Dar ofisi zao ziko Makao Makuu ni Kurasini Bendera tatu jirani na makao makuu ya Bandari,Temeke jirani na Hospitali ya Temeke,Kinondoni wako Mwenge njia ya cocacola JOSAM House na Ilala wako Ocean Road hospital au watafute kwenye www.nhif.or.tz au wa email info@nhif.or.tz
 
nawashukuru sana Iron Lady pamona na NCHIMI kwa maelezo mujarabu kabisa.

Sasa nimegundua NHIF ndio suluhisho la huduma ya afya nchii hii.

Asanteni nyote
 
Last edited by a moderator:
mimi binafsi naishukuru sana bima ya afya ya taifa na hata nikikosa dawa hosptal kuna maduka yana huduma hizo kwa hiyo nikiugua na sina pesa bado ni na amani




maduka hayo yako wap na wap mzee, inawezekana tukafa na kadi ndani kwa kukosa taarifa, orodhesha kama unayajua mzee.
 
maduka hayo yako wap na wap mzee, inawezekana tukafa na kadi ndani kwa kukosa taarifa, orodhesha kama unayajua mzee.
Maduka yako mengi sana kwenye karibia miko yote na takribani wilaya zote itategemea wewe uko wapi cha msingi hawa jamaa wana ofisi kila mkoa unaweza ukaenda ofisini kwao wakakupa list of acceredited facilities kwa eneo unaloishi au hata ukiwatumia email watakutumia tu
 
Dahh!nlikimbilia thread nikidhani kuna updates kumbe...!muulize google atakupa info zoote
 
Ukweli bima ya afya ya afya inasaidia sana na imeokoa sana familia yangu kwani kipato changu kidogo lakini bima ya afya imenifanya kuweza kuingia karibu zote dsm anayesema haifai ni mnafiki wala si mteja wa bima hiyo maana nilianza kupata huduma tumaini hospital nikapewa rufaa regent kwa ufupi ni hospital aghali sana lakini nimetibiwa bila pingamizi ila uhaba wa dawa ni wa nchi nzima si nhif maana kama ukienda hosp ndogondogo dawa utakosa tu hata kama unayo pesa mkononi .nhif ukitaka kuijua tembeleamtandao
 
Mimi ni mwanachama na nimekuwa nikifaidika na Bima ya Afya Tangu mwaka 2002 na nimekuwa mfuatiliaji mzuri wa mafao ya hawa jamaa. Kitaalamu NHIF au Bima ya afya wanatumia system inayoitwa FEE FOR SERVICE ambayo hakuna kikomo cha gharama kwenye matibabu na unaweza kupata huduma wewe na wategemezi wako watano kwa maana ya wewe,mwenzi wako wa ndoa,watoto wako na wazazi wakoau hata wakwe zake na kuwa na jumla ya wanufaika sita na wote mnapewa vitambulisho ambavyo unaweza kupata huduma popote Tanzania kwenye hospitali zote za serikali,mashirika ya dini,za watu binafsi na na pia wamesajiri pharmacy ili ukienda na kukosa dawa kwenye hospital unapewa form ya kwenda kuchukua dawa. Na gharama ya kujiunga kwa mtu binafsi ni Tshs 964,800 na unapaswa tu kuandika barua kwao na kuwa na wadhamini wawili ambao ni wanachama wa NHIF. Hao wanaokushauri kwenda Private Insurance ni kwamba wao wana tumia capitation Method ambayo ina ceiling limit ya cost za matibabu na wana pima Health status ya wanachama wake na especially kama una mtu mwenye clonic desease wanamkataa hasa kansa,kisukari,figo wakati bima ya afya wao wanasema Organisation yao haiku katika misingi ya kibiashara wala lengo la kutengeneza faida bali kutoa huduma. kwa Dar ofisi zao ziko Makao Makuu ni Kurasini Bendera tatu jirani na makao makuu ya Bandari,Temeke jirani na Hospitali ya Temeke,Kinondoni wako Mwenge njia ya cocacola JOSAM House na Ilala wako Ocean Road hospital au watafute kwenye www.nhif.or.tz au wa email info@nhif.or.tz

Mkuu Nchimi maelezo yako nadhani yatakua yamekata kiu ya wengi! Mwenyewe nilikua na kiu ya kujua kama mimi mtu binafsi nitawezaje kupata huduma hii ya NHIF, kumbe ni kujiandaa tu na naweza pata huduma,ila naomba kujua kitu kimoja toka kwako,hii gharama ya kujiunga ya 964,000/= unatakiwa uitoe mara moja au kwa installment?na je gharama ya mchango wa kila mwezi/kila mwaka ikoje kwa mimi mtu binafsi?asante mkuu
 
Ndugu zangu napenda kufahamu taratibu za kujiunga na mfuko wa bima ya afya kwa ambao sio waajiriwa. Mimi nashughuli zangu binafsi nataka kujiunga na bima ya afya pamoja na familia yangu. Naombeni taratibu kama inawezekana kujiumga.
 
Salaam wakuu,

Mimi sijaajiriwa na ngependa niweze kuwa na bima ya Afya kwa ajili yangu na family yangu.
Nifanyeje ili nuweze kuingia huko kwa sasa nipo Mwanza ndio shughuli zangu zilipo..
natanguliza shukrani
 
Back
Top Bottom