ndege joni
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 673
- 1,083
Habarini za muda huu wanajukwaa
Kwa wanaosoma chuo kikuu cha kilimo cha sokoine kuna tatizo gani kuhusu bima ya afya?
Mimi ni mfanyabiashara mdogo ila nasomesha mdogo wangu SUA ambaye pia ni mtumishi wa UMA (ana kipato kidogo kisichoweza kumsomesha) hivyo ananitegemea mimi kumsaidia kwa kiwango kikubwa.
Kwa leo nahitaji kueleweshwa kuhusu BIMA ya afya, maana anadai analazimika kulipia BIMA mara ya pili (Kiasi cha Tsh 50,000 wakati ana Kadi ya BIMA ya afya na anakatwa salary kila mwezi. Nikilinganisha na mdogo wangu mwingine wa UDOM yeye halipii kwa sababu ana Kadi ya BIMA ya afya. Sijajua kuhusu vyuo vingine zaidi ya hivyo.
Kwa waliopo SUA je hili ni kweli?
Pia sijataka kuongelea michango mingine ambayo haina maelezo (other fees) ambayo pia ni kubwa kuliko vyuo vingine. Na inadaiwa haijulikani matumizi yake.
Je ni sahihi kulipia huduma ya BIMA ya afya kwa mtindo huo? Kwa upande wangu naona ni wizi ambao Mh Raisi wetu wa wanyonge na Waziri wa Elimu anatakiwa atambue wizi huo