GT,
Unajua nimekuwa nikiiangalia hii naona haieleweki eleweki.
Mwanakijiji anapenda kuleta habari kwa vifumbo fumbo (halafu hapo hapo anasema "we dare talk openly"). Hii ilivyokaa kama si sawa, kama wapemba hawanufaiki na utalii kumuweka Bill Gates at the center of the saga si sawa kabisa, kwa sababu yeye hatakiwi kuwa na interests za wapemba (ingawa Bill and Melinda Gates Foundation inatoa misaada Mafia na Pemba).Tuna serikali, viongozi, wabunge raia wenzetu, wako wapi? Wanafanya nini? wanahakikishaje safari hizi zinanufaisha wananchi wa kawaida? Halafu hizi mentality za kutegeshea kwenye natural resources ni noma, inabidi tusome tuweze kuwa na mental capital, siku wanyama, dhahabu na natural resources za hivi nyingine zikiisha tutakuwa wageni wa nani?
Mimi ninachoshuhudia sasa nii hii culture ya kuwa jumpy, which is not entirely a bad thing given our history and the entire history of the encounters of civilizations.
Concern yangu ni kwamba, inabidi tufikirie more originally, hizi habari za kusimama doria bandarini Zanzibar na kuangalia nani kaingia nani katoka na kuanza kupiga kelele bila ya kuwa na data, mwishowe tutampigia kelele Bill Gates anayeenda kutoa misaada ya "Bill and Melinda Gates Foundation" na kuwaacha masultani na wtaliani wanaokwiba kwa kalamu.Tunataka data, no data no right to accuse, no research no right to speak.
Na kuhusu wapemba wanafaidikaje ni swala relevant, lakini tuongelee utalii kiujumla, kumuweka Gates pale kunatoa picha kama vile Gates kaja kununua kisiwa Pemba halafu wapemba wamebanana, unless una scandal ya kumhusu Gates, kumchoresha hivi si sawa.
Reputation ni kitu muhimu sana katika mahusiano, na kama huna solid data kumpaka mtu matope, au kumuandika katika jinsi inayoweza kutafsirika kirahisi kama ni kumpaka matope, ni kitu kibaya sana.
Halafu tusitake shida zetu zote tuzimalize kwa sababu tu Bill Gates kaja Zanzibar, hizi zitakuwa fikra mgando. Ingawa mimi si mfuasi wa wanafalsafa wahafidhina, Ayn Rand alinifanya nifikiri aliposhambulia dhana nzima ya "ku transfer wealth" (if you are poor tax the rich) as opposed to the concepr of genuine wealth generation, tusije kuwa kama yule msafiri ambaye akiona kichaka tu haja inambana.Tutataka tupandishe bei za huduma kiholela kwa sababu yeye ni Bill Gates? Vipi mtu akisema Wapemba wanatakiwa wafaidike na kodi na fees anazolipa Bill Gates na kama hawafaidiki ni tatizo la serikali ya Zanzibar (huku ndiko ulikokuwa unaelekea mkuu? If so, spell it out usiache mambo hewani watu wakamwona Gates mitaa ya kati wakamshambulia bure, kumbe mtu kaja kutoa misaada)