Bilioni moja ni chicken feed kwa MO lakini...

Bilioni moja ni chicken feed kwa MO lakini...

Mwenye namba za yule mama mganga/mchawi aliyembebesha yule mwizi wa kiroba cha mahindi hadi mwizi akaripoti kituo cha polisi Mlandizi kiroba kikiwa kimemganda naziomba nina shida nazo
 
Kwa wale wasiojua bilioni moja inaandikwaje au ina masifuri mangapi hii hapa... 1,000,000,000/=... Bilioni moja ina sifuri 9....!
Kwa pesa yetu ya kibongo (sipendi kuiita madafu) ni kukidharau cha kwangu mwenyewe hivyo ni kujidharau, bilioni moja si kiwango haba cha minoti ila ukija kubadili kwa dola haifiki dola laki nne na nusu(450,000$)... Kwa utajiri wa MO alionao hii tunaita kimombo... Chicken [emoji239] feed.... Yaani ni kidogo sana...! Kuku hawezi kumaliza punje 30 za mahindi... Akimaliza ujue atavimbiwa na kuvimbiwa...
Familia ya MO imetangaza rasmi donge nono la shilingi za kitanzania BILIONI MOJA kwa atakayefanikisha kupatikana kwa ndugu yao (pengine akiwa hai)
Familia imechukua uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa dhumuni la kutekwa ndugu yao halikuwa kikomboleo(ransom) bali ni sababu nyinginezo.... Kama sababu ni kikomboleo tayari watekaji wangeshaongea kuwa wanataka bei gani! Na hili lingeganyika ndani ya saa 72! Jamaa huwa hawapendi kupoteza muda... Wanaweka dau mezani halafu muamie kunyoa ama kusuka!
Kwa kutangaza zawadi nono kama hiyo ni wazi na ni dhahiri sasa mambo ni magumu na wako tayari hata kupanda dau ili tu kumpata ndugu yao akiwa salama salimini... Pesa zinatafutwa lakini sio uhai..
Nimeona watu wengi wakiijadili B1, hiyo sio pesa ya mchezo na haipatani kirahisi kama kuokota mwekundu njiani.... Ni pesa ambayo kila mtu anatamani kuipata, lakini huu mnanda ni next level... Hii sio singei.... Ni MNANDA!
Sio watu binafsi tu hata private investigations nyingi ndani na nje ya nchi zingependa kuchangamkia tenda.... Tusichokijua wengi ni kwamba tunaiwaza tu B1 na masifuri yake 9.... Lakini kuipata ni jambo la kwanza na maisha utakayoishi baada ya kuipata ni jambo jingine kabisa.... Unaweza kuipata leo na baada ya wiki tu tukaanza msako wako!
Tuwe watu wa tafakari na tuo... Dunia ina siri nyingi na kwamwe hatuwezi kuzijua zote... B1 ni chicken feed lakini ukiwapa nyenyere kundi zima ni msosi wa msimu mzima!

Good morning Tanzania
Hivi timamu yeyote atapiga zile number eti kutoa taarifa ili apate hiyo bilioni moja?
 
Hivi timamu yeyote atapiga zile number eti kutoa taarifa ili apate hiyo bilioni moja?
People will try... The metals are very tight.... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hiyo hela itabidi TBL nihamishie nyumbani kwa muda nkipata!

Ova
 
Uko sahihi mkuu!
Ukipata hiyo 1B wape familia yako hata 600Million ili iwe kama akiba ya dau la kukusaka pale utakapo potea.
Tuwe na tafakuri kidogo... Watekaji wanaweza pia kutengeneza mchongo kwenye hili.... Tusiwachukulie poa kivile
 
Kabla ya hao kuna
Liberty desk
Snowden
Na marekani anaweza kuwa na taarifa zote kwa hakika kabisa
Liberty desk ni taasisi yenye matawi dunia nzima... Ina kila taarifa muhimu na ya siri kila dakika kila saa popote duniani, kuanzia magenge ya mafia, biashara haramu, ishu za serikali nk
Snowden ni mdukuzi mahiri
Mmarekani ni mbea aliyejipa ukiranja wa dunia.... Kama akiona jambo fulani ana maslahi nalo atatafuta mbinu mpaka lijulikane, akiona hana mahaba nalo atalipotezea
Kwasasa jambo hili liko ngazi ya CLASSIFIED INFORMATION.... Wanalijua wale wanaotakiwa kulijua tuu.. Na kwa mtu kama MO si ajabu hata wale waliomteka hawapo tena nchini na hawajui alipo
Pamoja na yote naamini mwisho wa jambo hili utafika salama, naamini hadi sasa KILINGENI kunaonyesha jamaa yupo salama.,au sio Mkuu!!
 
Pamoja na yote naamini mwisho wa jambo hili utafika salama, naamini hadi sasa KILINGENI kunaonyesha jamaa yupo salama.,au sio Mkuu!!
Ndio bado kuna vibration(mitetemo) ukanda fulani kuonesha uhai
 
Back
Top Bottom