Bilioni moja ni chicken feed kwa MO lakini...

Bilioni moja ni chicken feed kwa MO lakini...

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
375,432
Reaction score
869,858
Kwa wale wasiojua bilioni moja inaandikwaje au ina masifuri mangapi hii hapa... 1,000,000,000/=... Bilioni moja ina sifuri 9....!

Kwa pesa yetu ya kibongo (sipendi kuiita madafu) ni kukidharau cha kwangu mwenyewe hivyo ni kujidharau, bilioni moja si kiwango haba cha minoti ila ukija kubadili kwa dola haifiki dola laki nne na nusu(450,000$)... Kwa utajiri wa MO alionao hii tunaita kimombo... Chicken [emoji239] feed.... Yaani ni kidogo sana...! Kuku hawezi kumaliza punje 30 za mahindi... Akimaliza ujue atavimbiwa na kuvimbiwa...

Familia ya MO imetangaza rasmi donge nono la shilingi za kitanzania BILIONI MOJA kwa atakayefanikisha kupatikana kwa ndugu yao (pengine akiwa hai)
Familia imechukua uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa dhumuni la kutekwa ndugu yao halikuwa kikomboleo(ransom) bali ni sababu nyinginezo.... Kama sababu ni kikomboleo tayari watekaji wangeshaongea kuwa wanataka bei gani! Na hili lingefanyika ndani ya saa 72! Jamaa huwa hawapendi kupoteza muda... Wanaweka dau mezani halafu muamie kunyoa ama kusuka!

Kwa kutangaza zawadi nono kama hiyo ni wazi na ni dhahiri sasa mambo ni magumu na wako tayari hata kupanda dau ili tu kumpata ndugu yao akiwa salama salimini... Pesa zinatafutwa lakini sio uhai..
Nimeona watu wengi wakiijadili B1, hiyo sio pesa ya mchezo na haipatani kirahisi kama kuokota mwekundu njiani.... Ni pesa ambayo kila mtu anatamani kuipata, lakini huu mnanda ni next level... Hii sio singeli.... Ni MNANDA!

Sio watu binafsi tu hata private investigations nyingi ndani na nje ya nchi zingependa kuchangamkia tenda.... Tusichokijua wengi ni kwamba tunaiwaza tu B1 na masifuri yake 9.... Lakini kuipata ni jambo la kwanza na maisha utakayoishi baada ya kuipata ni jambo jingine kabisa.... Unaweza kuipata leo na baada ya wiki tu tukaanza msako wako!
Tuwe watu wa tafakari na tuo... Dunia ina siri nyingi na kwamwe hatuwezi kuzijua zote... B1 ni chicken feed lakini ukiwapa nyenyere kundi zima ni msosi wa msimu mzima!

Good morning Tanzania
 
ukidhamiria kutoa taarifa,huchukui interms of cash wala muamala hautakiwi kusoma kwenye account za benki zatu hapa

mnazama kwenye dark web na mnamalizana kwa njia ya bitcoin baada ya hapo wewe utajua utaigeuzaje kuwa pesa halali kwenye account isiyo kua ya hapa nchini nawaza tu.

nami natoa ofa kama unataarifa ila unahofia usalama wako baada ya hapo nicheki tuone namna gani tutapata hilo dau bila kuacha alama
 
Umesema kweli kuhusu maisha baada ya kusema sehemu alipo hilo uko sawa lakini tukiwa wakimya hivi haina maana yeyote inamaana ndugu zetu wakakua wakipotea kila siku halafu tusiweke jitihada za kuwatafuta eti kisa tutashikwa?

NOO mkuu napinga, mm nachoshauri watu wawe jasiri wasikubali kuonewa onewa daily. Iwapo anafahamika sehemu alipo mbona raia yeyote anaweza kutumia njia mbali mbali kutaarifu pasipo yeye kujulikana?
Anaweza peperusha karatasi zenye jumbe kimya kimya mbele za wapita njia au makusanyiko ya watu? Anaweza kutumia lain mpya asambeze ujumbe whatsapp groups au kutuma jumbe polisi?
Any thing is possible kikubwa muhusika amentain anonymity akimaliza atupe lain na simu au achome moto.
 
Mbona unatisha watu Somoo, vp uganga wako haujakuonyesha alipo MO.. Kuanzia leo nimeamini waganga wanatudanganya sisi masikini... Na kutupa ujasiri bandia
 
ukidhamiria kutoa taarifa,huchukui interms of cash wala muamala hautakiwi kusoma kwenye account za benki zatu hapa

mnazama kwenye dark web na mnamalizana kwa njia ya bitcoin baada ya hapo wewe utajua utaigeuzaje kuwa pesa halali kwenye account isiyo kua ya hapa nchini nawaza tu.

nami natoa ofa kama unataarifa ila unahofia usalama wako baada ya hapo nicheki tuone namna gani tutapata hilo dau bila kuacha alama
Unaakili sana ww
 
Mshana acha utani bro, hio ni hela yako ya pensheni ya kutunza maiti kwa zaidi ya mara 8! Acha masihara na B moko kaka!!!
 
sipati picha bus za kutoka mara to dar zinavyojaza wakurya wanaokuja town kuchangamkia fursa maana wazee wa kukamuliwa na wapemba hiyo kazi hawataiweza.
 
Leo nmekushusha hadhi Mkuu,, wewe na ulozi wako wote umeshindwa kujua mahali ambapo MO yupo,, Kweli we bure kabisa ,,ulozi Kumbe hauna faida,,, =
amekuambia kuipata hiyo 1b ni issue moja na utaishije baada ya kuipata ni another issue. Huenda anaogopa msako usije hamia kwake akapotea akamwacha Demiss bure!
 
Back
Top Bottom