Kwa wale wasiojua bilioni moja inaandikwaje au ina masifuri mangapi hii hapa... 1,000,000,000/=... Bilioni moja ina sifuri 9....!
Kwa pesa yetu ya kibongo (sipendi kuiita madafu) ni kukidharau cha kwangu mwenyewe hivyo ni kujidharau, bilioni moja si kiwango haba cha minoti ila ukija kubadili kwa dola haifiki dola laki nne na nusu(450,000$)... Kwa utajiri wa MO alionao hii tunaita kimombo... Chicken [emoji239] feed.... Yaani ni kidogo sana...! Kuku hawezi kumaliza punje 30 za mahindi... Akimaliza ujue atavimbiwa na kuvimbiwa...
Familia ya MO imetangaza rasmi donge nono la shilingi za kitanzania BILIONI MOJA kwa atakayefanikisha kupatikana kwa ndugu yao (pengine akiwa hai)
Familia imechukua uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa dhumuni la kutekwa ndugu yao halikuwa kikomboleo(ransom) bali ni sababu nyinginezo.... Kama sababu ni kikomboleo tayari watekaji wangeshaongea kuwa wanataka bei gani! Na hili lingeganyika ndani ya saa 72! Jamaa huwa hawapendi kupoteza muda... Wanaweka dau mezani halafu muamie kunyoa ama kusuka!
Kwa kutangaza zawadi nono kama hiyo ni wazi na ni dhahiri sasa mambo ni magumu na wako tayari hata kupanda dau ili tu kumpata ndugu yao akiwa salama salimini... Pesa zinatafutwa lakini sio uhai..
Nimeona watu wengi wakiijadili B1, hiyo sio pesa ya mchezo na haipatani kirahisi kama kuokota mwekundu njiani.... Ni pesa ambayo kila mtu anatamani kuipata, lakini huu mnanda ni next level... Hii sio singei.... Ni MNANDA!
Sio watu binafsi tu hata private investigations nyingi ndani na nje ya nchi zingependa kuchangamkia tenda.... Tusichokijua wengi ni kwamba tunaiwaza tu B1 na masifuri yake 9.... Lakini kuipata ni jambo la kwanza na maisha utakayoishi baada ya kuipata ni jambo jingine kabisa.... Unaweza kuipata leo na baada ya wiki tu tukaanza msako wako!
Tuwe watu wa tafakari na tuo... Dunia ina siri nyingi na kwamwe hatuwezi kuzijua zote... B1 ni chicken feed lakini ukiwapa nyenyere kundi zima ni msosi wa msimu mzima!
Good morning Tanzania