benzemah
JF-Expert Member
- Nov 19, 2014
- 1,504
- 3,032
Serikali kupitia Ofisi ya Rais-TAMISEMI imeeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2023/24 imetenga jumla ya Shilingi Bilioni 8.75b kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa vituo vya afya 20 katika Halmaashauri nchini
Akizungumza Bungeni Naibu Waziri, Ofisi ya Rais–TAMISEMI, Festo J. Dugange amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ujenzi, upanuzi na ukamilishaji wa vituo vya afya ambapo vituo vya Afya vya Rukaragata, Kalenge na Nyabusozi ni miongoni mwa vituo vya muda mrefu na miundombinu yake inahitaji maboresho kulingana na mahitaji ya sasa.
Nduganga emesema Halmashauri ya Wilaya ya Biharamulo imetengewa shilingi milioni 500 kwa ajili ya upanuzi wa vituo vya afya viwili kati ya vitatu vyenye mahitaji.
Aidha, Dkt. Dugange amesema Utaratibu wa kutenge bajeti kwa ajili ya ukarabati na upanuzi wa vituo vya afya chakavu ni endelevu.