Sasa nimetambua kwa hakika kuwa tatizo lipo kichwani mwa wabunge wa Bunge letu. Na hatimaye tatizo lipo kichwani mwa watanzania.
Viongozi wabovu wanachaguliwa kutoka katika jamii mbovu. Viongozi wabovu wanachaguliwa na wapiga kura wabovu, wasio na uelewa mpana, wenye upeo finyu, na wasio na nia ya dhati kuudhibiti umaskini wao!
Mifano ipo mingi tu, wananchi wanaona matatizo haya yote lakini utashangaa wakiohongwa kidogo tu, wakati wa uchaguzi wanakuwa wamesahau matatizo haya yote na kujidai eti watu fulani ni machaguo ya Mungu! Shame on you all! Hakuna chaguo la Mungu anayeweza kukubali watu wafe kwa kukosa huduma bora za afya, elimu na miundo mbinu ili eti wabunge wakae na kuendesha shughuli zao pahala bora kuliko wabunge wengine wooote africa! Labda kama huyo mtu ni chaguo la mungu wake na mkewe, na wanae na maswahiba wake, kijiweni kwake, lakini sio Mungu tunayemjua asiyependa uchafu na dhuluma.
Biblia inaandika, "....asiyewajali watu wa nyumbani mwake ni mbaya kuliko aliye ikana imani!...." Je, kwa kutojali huku kunakofanywa na Viongozi wetu, tunathubutuje kuwaita eti ni machaguo ya Mungu? Jibu ni rahisi tu, aidha viongozi hawa ni maswaiba wao ama akili zetu hazina akili!
Mtu mwenye akili hawezi kuwalaza watoto njaa kisa eti akanunue suti mpya ili awashinde jirani zake ama ili aendelee kushikilia rekodi mtaani kwao kwa kuwa na suti ya kisasa zaidi! Huyo lazima awe ZUZU, kama alivyosema hayati Babab wa Taifa!
Hiyo cha mtoto, tuje kwenye hao wabunge wenyewe sasa!
Sasa hivi wapo 340 wanatakiwa kuongezeka hadi kufikia 360! Tujiulize, tumefanya tathmini kujua hao 340 wamezidiwa na kazi ipi inayohitaji kuongezeka kwa hao wengine 20? Mbona wakati wa mwalimu Nyerere wabunge walikuwa wachache kuliko hawa, miundo mbinu mibovu kuliko hii, mashangingi hayakuwepo lakini wabunge hao waliweza kwenda kushughulika na kero za wananchi na wananchi wakaridhika. Sasa kuna miundombinu bora zaidi, mashangingi yapo, ukumbi wa bunge bora kuliko zamani, kero za wananchi bado sipo vile vile halafu eti mnataka kuongeza idadi ya wabunge, kuufanya ukumbi wa bunge kuwa wa kisasa zaidi. Najiuliza: Ili nini?
Ili walale zaidi na kusinzia? Ama kwa vile ni wengi wa wabunge ni wazee, it is therefore necessary to make them as comfortable as possible?
Na isitoshe, mashangingi yenyewe waliyopewa tunayaona mjini yamejazana yanatuletea foleni tu barabarani na hayatumiki tena kwenda huko majimboni kukutana na wananchi kama inavyopasa instead yanatumika kujenga heshima na sifa za kijinga mjini! What a shame?????????
Watanzania wenzangu, we are deep in some serious shit here, something needs to be done and done quickly, kila mmoja ajiulize tu kwa nafasi yake anatakiwa kufanya nini!