Bilioni 30.9 ku upgrade ukumbi wa Bunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bilioni 30.9 ku upgrade ukumbi wa Bunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Buchanan, Jun 15, 2010.

 1. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #1
  Jun 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Na Mwandishi Wetu, Dodoma

  UKUMBI mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, unaotumika kwa shughuli za Bunge utavunjwa na kusukwa upya ili kuruhusu utengenezaji wa viti vya kisasa vitakavyofungwa vifaa maalumu vya mawasiliano ya teknolojia ya kisasa.

  Hatua hiyo pia itaongeza idadi ya viti kutoka 340 vya sasa hadi viti 360 ili kumudu idadi ya wabunge wanaotarajiwa kuongezeka katika Bunge lijalo.

  Itakumbukwa jengo hilo ambalo ni la kwanza Afrika Mashariki na la tatu kwa Bara la Afrika, hadi kukamilika kwake liligharimu zaidi ya sh bilioni 30.9.

  Hatua hiyo ilitangazwa jana na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, wakati akitoa mwongozo wa kiti cha Spika, kutokana na hoja iliyoibuliwa na Mbunge wa Ukerewe, Gertrude Mongela, aliyehoji sababu za Bunge kutumia teknolojia ya zamani kuhesabu kura za ndiyo na hapana zilizopigwa kwa wabunge ili kuunga mkono au kupinga hotuba ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2010/2011.

  Akifafanua muundo mpya wa Bunge, Spika Sitta alisema kila kiti cha mbunge kitakuwa na runinga pamoja na mawasilino ya kisasa ya kompyuta, ambayo yatamwezesha kuuliza swali na kupata majibu kutoka kwa waziri anayehusika bila kusimama wala kutumia vikaratasi.

  "Kwanini tunatumia teknolojia ya zamani, jibu lake ni dogo tu, ni kwamba hili jengo viti vyake vitafumuliwa vyote na kusukwa upya na kazi hiyo itafanyika mara baada ya kuvujwa Bunge. Michoro ya kazi hiyo imeshakamilika na kazi hiyo imefanywa na Mbunge wa Hai, Fuya Kimbita (CCM), yeye na ujumbe wake wamekwenda kwenye mabunge ya Scotland na mabunge mengine kuangalia jinsi ya kulirekebisha Bunge letu liwe la kisasa zaidi," alisema Spika Sitta
  .

  Kwa Habari Zaidi Soma Tanzania Daima
   
 2. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #2
  Jun 15, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Jamani mabilioni mengine yanateketezwa kukarabati ukumbi wa Bunge bila sababu ya maana. Hivi kama huna hata nguo za kuvaa unaweza kuwaza kununua gari? Zaidi ya hayo wanataka waongeze idadi ya wabunge ili waendelee kula kodi zetu! Si wangezipeleka hizo fedha kununua dawa hospitalini, kununua madawati ya wanafunzi wa shule za msingi, nk?
   
 3. p

  pareto 8020 Member

  #3
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 7, 2010
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Is this a priority? Katika kipindi hiki kigumu cha uchumi, nadhani pamoja na umuhimu
  wa kuwa na bunge la kisasa, isingekuwa busara kufanya hiyo upgrade inayotazamiwa.
  Kwa mtazamo wangu, at this point in time, wangefanya upanuzi wa kawaida wa kuwezesha kuongeza viti kulingana na idadi mpya ya wabunge pasipo kufanya new installation ya high-tech PA system kwa sasa....maybe in future hali ya uchumi ikiboreka wangeweza kufikiria HIGH-TECH.....

  ==========================================================
  Ukumbi wa Bunge kubomolewa

  UKUMBI mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, unaotumika kwa shughuli za Bunge utavunjwa na kusukwa upya ili kuruhusu utengenezaji wa viti vya kisasa vitakavyofungwa vifaa maalumu vya mawasiliano ya teknolojia ya kisasa.
  Hatua hiyo pia itaongeza idadi ya viti kutoka 340 vya sasa hadi viti 360 ili kumudu idadi ya wabunge wanaotarajiwa kuongezeka katika Bunge lijalo.
  Itakumbukwa jengo hilo ambalo ni la kwanza Afrika Mashariki na la tatu kwa Bara la Afrika, hadi kukamilika kwake liligharimu zaidi ya sh bilioni 30.9.
  Hatua hiyo ilitangazwa jana na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, wakati akitoa mwongozo wa kiti cha Spika, kutokana na hoja iliyoibuliwa na Mbunge wa Ukerewe, Gertrude Mongela, aliyehoji sababu za Bunge kutumia teknolojia ya zamani kuhesabu kura za ndiyo na hapana zilizopigwa kwa wabunge ili kuunga mkono au kupinga hotuba ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2010/2011.
  Akifafanua muundo mpya wa Bunge, Spika Sitta alisema kila kiti cha mbunge kitakuwa na runinga pamoja na mawasilino ya kisasa ya kompyuta, ambayo yatamwezesha kuuliza swali na kupata majibu kutoka kwa waziri anayehusika bila kusimama wala kutumia vikaratasi.
  “Kwanini tunatumia teknolojia ya zamani, jibu lake ni dogo tu, ni kwamba hili jengo viti vyake vitafumuliwa vyote na kusukwa upya na kazi hiyo itafanyika mara baada ya kuvujwa Bunge. Michoro ya kazi hiyo imeshakamilika na kazi hiyo imefanywa na Mbunge wa Hai, Fuya Kimbita (CCM), yeye na ujumbe wake wamekwenda kwenye mabunge ya Scotland na mabunge mengine kuangalia jinsi ya kulirekebisha Bunge letu liwe la kisasa zaidi,” alisema Spika Sitta.
  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekitetea Chama Cha Mapinduzi (CCM) bungeni kuhusu utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi kuwa bado unaendelea katika mwaka wa fedha 2010/2011.
  Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (CHADEMA), aliyehoji kutotekelezwa kikamilifu kwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi wakati serikali ikielekea katika Uchaguzi Mkuu na kuwa ilani ilipaswa kuwa imetekelezwa kwa asilimia 100.
  Waziri Mkuu alisema fedha zitakazotengwa katika mwaka wa fedha 2010/2011 zitakwenda kukamilisha utekelezaji wa ilani hiyo katika baadhi ya maeneo, kwani ndio mwaka wa tano wa Serikali ya Awamu ya Nne kukamilisha ahadi zake kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi. “Nataka niseme tu kwamba muda wa serikali kumalizia ahadi zake bado upo na hii bajeti ya mwaka 2010/2011 ndiyo bajeti yetu ya tano ambayo ndiyo itakayotuwezesha kukamilisha ahadi zetu zilizobaki,” alisema Pinda.
   
 4. pcman

  pcman JF-Expert Member

  #4
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 9, 2008
  Messages: 743
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  something is wrong somewhere.
   
 5. W

  WildCard JF-Expert Member

  #5
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sitta ni MBADHIRIFU hasa. Wala hajui, hajali, haoni hali ya huduma za jamii zikoje hata kwenye jimbo lake. Kila nikiangalia kwenye luninga majengo ya mabunge ya wenzetu yako vilevile. Hapa jirani Kenya wenye uchumi mkubwa kuliko wetu, jengo lao ni lilelile, hawakai kwa raha na kutanua kama hawa wa kwetu. Lakini wasikilize hoja zao mle ndani. Utapenda. Kule Uingereza jengo lile la Bunge ni la muda mrefu tu. Mbwembwe hizi anazotaka Sitta ziwekwe mle kule House of Commons hazipo. Tunaelekea wapi? Tulikuwa hapa Karimjee, hapakutufaa, tukajenga ule ukumbi wa Msekwa. Haukutosha. Tukajenga huu wa sasa. Tunataka kutumia tena haya mabilioni. Hatuweki vyombo vya maana. Tunatafuta vya Mchina. Nilidhani Wabunge watakuwa KIOO chetu. Wangefanana nasi, kumbe ni watu tofauti kabisa tukishawachagua! Nani ataiokoa NCHI hii?
   
 6. JS

  JS JF-Expert Member

  #6
  Jun 15, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  This is absurd in all its aspects. 30 billion taxpayers money ilitumika kujenga huo wa sasa why didnt they think of it in the first place kwamba ilihitajika teknolojia ya kisasa kuendesha shughuli za Bunge na instead wakajenga na kuapply teknolojia ya zamani?? Hiyo teknolojia ilikuwa haijavumbuliwa hapo kabla wakati wanaspend 30 billion kujenga huo ukumbi wa sasa???(ambayo i beleive ilikuwepo tayari).

  When will ever set priorities in this country?:mad::mad::mad::mad::mad:
   
 7. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #7
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  NIMECHOKA! Kweli tuna kazi....
   
 8. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #8
  Jun 15, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tatizo siyo Sitta mkuu, ni mkulu bilanga! Hizi ndizo mentality za kimasikini, tunakopa ili tununue perfume na tai nzuri..... kama siyo kweli tofauti yake na hii ni nini??? zaidi ya 45% ya budget tumekopa halafu tujenge barabara na miundombinu ya umwagiliaji sisi tunakopa ili kulifanya Bunge letu liwe na jumba la kisasa zaidi kuliko yote Africa, huku uchumi wetu ni wa tatu kutoka mwisho?

  Absolutely nuts
   
 9. C

  Chupaku JF-Expert Member

  #9
  Jun 15, 2010
  Joined: Oct 15, 2008
  Messages: 1,043
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Hiyo sio kazi ya Kashilillah kweli? We are yet to see things.
   
 10. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #10
  Jun 15, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Ndiyo maana wahisani wanatunyima hela zao, hatuna priority kabisa - Ntemi Kazwile upo sahihi, hili ni tatizo letu watanzania.

  1. Tukakurupuka kununua ndege ya Rais ipo kiko wapi?
  2. Tukakurupuka kununua Rada ipo kiko wapi?

  Hatujajifunza tu? Sitta na Pinda mmesahau umaskini wa wapiga kura wenu? Si priority kwa sasa, nikiwa mwananchi na mlipa kodi wa nchi hii siafiki kabisa matumizi ya hizi pesa.
   
 11. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #11
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Sisi ni Mabingwa wa kuweka rekodi katika hali ya umaskini komavu,

  1. Nchi ya kwanza Afrika kuialika timu ya brazil kucheza kwenye ardhi ya afrika.

  2. Nchi ya kwanza afrika mashariki na kati kuwa na bunge zuri, kubwa la kisasa linalotunga sheria za kizamani.

  3. Nchi ya kwanza afrika ambayo ilitoa kiongozi aliyekutana na Raisi Obama.

  4. Nchi ya kwanza africa ambayo raisi wa marekani aliishi karibia wiki.

  5. Nchi ya kwanza afrika ambayo ina rekodi nyingi lakini wanachi wake ni dhoofu bin hali

  Mwenye rekodi nyingine anakaribishwa.
   
 12. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #12
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie ndio navyochoka na nchi hii tunasema hatuna pesa yet tunatoa Bilioni 30 kujenga ukumbi for f*** sake. Kuna watu wanakufa na njaa dodoma, iringa, shinyanga, sumbawanga sie tunajenga bunge la kifahari jamani mwogopeni mungu. Yaani hadi hasira napata haki ya nani!!!
   
 13. Kiranga

  Kiranga JF-Expert Member

  #13
  Jun 15, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 34,605
  Likes Received: 6,175
  Trophy Points: 280
  Mimi nilishasema hawa "viongozi" wetu hwajali kumaliza au hata kupunguza umaskini, wanajijali wenyewe tu.

  Ni kama vile una baba aliyeshiba anatumia hela nyingi kununua expensive dessert na wine, huku watoto wake wanakufa kwa njaa.
   
 14. mpuuzi

  mpuuzi Member

  #14
  Jun 15, 2010
  Joined: May 29, 2010
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  UKUMBI mpya wa Bunge la Jamhuri ya Muungano, unaotumika kwa shughuli za Bunge utavunjwa na kusukwa upya ili kuruhusu utengenezaji wa viti vya kisasa vitakavyofungwa vifaa maalumu vya mawasiliano ya teknolojia ya kisasa.
  Hatua hiyo pia itaongeza idadi ya viti kutoka 340 vya sasa hadi viti 360 ili kumudu idadi ya wabunge wanaotarajiwa kuongezeka katika Bunge lijalo.
  Itakumbukwa jengo hilo ambalo ni la kwanza Afrika Mashariki na la tatu kwa Bara la Afrika, hadi kukamilika kwake liligharimu zaidi ya sh bilioni 30.9.
  Hatua hiyo ilitangazwa jana na Spika wa Bunge, Samuel Sitta, wakati akitoa mwongozo wa kiti cha Spika, kutokana na hoja iliyoibuliwa na Mbunge wa Ukerewe, Gertrude Mongela, aliyehoji sababu za Bunge kutumia teknolojia ya zamani kuhesabu kura za ndiyo na hapana zilizopigwa kwa wabunge ili kuunga mkono au kupinga hotuba ya Bajeti ya Serikali ya mwaka 2010/2011.
  Akifafanua muundo mpya wa Bunge, Spika Sitta alisema kila kiti cha mbunge kitakuwa na runinga pamoja na mawasilino ya kisasa ya kompyuta, ambayo yatamwezesha kuuliza swali na kupata majibu kutoka kwa waziri anayehusika bila kusimama wala kutumia vikaratasi.
  “Kwanini tunatumia teknolojia ya zamani, jibu lake ni dogo tu, ni kwamba hili jengo viti vyake vitafumuliwa vyote na kusukwa upya na kazi hiyo itafanyika mara baada ya kuvujwa Bunge. Michoro ya kazi hiyo imeshakamilika na kazi hiyo imefanywa na Mbunge wa Hai, Fuya Kimbita (CCM), yeye na ujumbe wake wamekwenda kwenye mabunge ya Scotland na mabunge mengine kuangalia jinsi ya kulirekebisha Bunge letu liwe la kisasa zaidi,” alisema Spika Sitta.
  Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amekitetea Chama Cha Mapinduzi (CCM) bungeni kuhusu utekelezaji wa Ilani yake ya uchaguzi kuwa bado unaendelea katika mwaka wa fedha 2010/2011.
  Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalumu, Susan Lyimo (CHADEMA), aliyehoji kutotekelezwa kikamilifu kwa ilani ya Chama Cha Mapinduzi wakati serikali ikielekea katika Uchaguzi Mkuu na kuwa ilani ilipaswa kuwa imetekelezwa kwa asilimia 100.
  Waziri Mkuu alisema fedha zitakazotengwa katika mwaka wa fedha 2010/2011 zitakwenda kukamilisha utekelezaji wa ilani hiyo katika baadhi ya maeneo, kwani ndio mwaka wa tano wa Serikali ya Awamu ya Nne kukamilisha ahadi zake kwa mujibu wa ilani ya uchaguzi.
  “Nataka niseme tu kwamba muda wa serikali kumalizia ahadi zake bado upo na hii bajeti ya mwaka 2010/2011 ndiyo bajeti yetu ya tano ambayo ndiyo itakayotuwezesha kukamilisha ahadi zetu zilizobaki,” alisema Pinda.
   
 15. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #15
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lahaula! Jamani hivi hawa wenzetu ambao wako kwenye jengo hilo kweli wanawawakilisha wananchi waliowapa kura kuingia humo ama wanajiwakilisha nafsi zao? Hivi kweli Tanzania tunayo 'starehe' ya kuweza kutumia fedha zote hizo kukarabati jengo ambalo limejengwa si muda mrefu uliopita? Kwa nini wasiwaze kuweka vibwagizo hivyo wakati wanalijenga? Hata ujenzi wenyewe wa ukumbi huo mpya wa kifahari ilikuwa ni ubadhilifu wa hali ya juu. Kulikuwa na haja gani hasa ya ukumbi mpya ambapo wa zamani ulikuwepo? Wabunge wa nchi maskini kama Tanzania wanataka kujilinganisha na wabunge wa nchi tajiri? Je, kuna mbunge yeyote aliyejitokeza kuhoji uhalali wa matumizi hayo mabovu ya fedha za wananchi maskini? Kweli tuna tatizo kubwa sana nchini kwetu kuliko tunavyoweza kulielewa!
   
 16. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #16
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Mie ndio maana nasema brother Sitta ndio wale wale tu anajiita Champion au Mpiganaji wa ufisadi lakini yeye mwenyewe ndio huyo huyo tu
   
 17. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #17
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  mimi naona wange upgrade wabunge wenyewe kuliko kuliupgrade jengo la bunge kwa kufanya hivyo ingeleta tija zaidi. Na wenye kuupgrade wabunge ni sisi na muda ni tarehe wenyewe ni tarehe 31 Oktoba 2010. Wabunge wakiwa upgraded hawatakubali hela zote hizo ziende kwenye bunge ambalo muda wote liko tupu.
   
 18. Mkosoaji

  Mkosoaji JF-Expert Member

  #18
  Jun 15, 2010
  Joined: Aug 24, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nilichoguswa mimi kwenye hii habari kama mliisoma vizuri, assessment ilifanyika SCOTLAND. Yaani maana yake kwa lugha nyingine tunajilinganisha na wenzetu SCOTLAND badala ya KENYA, UGANDA na hata SOUTH AFRICA.
   
 19. W

  WildCard JF-Expert Member

  #19
  Jun 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Sio Kashilila. Ni Sitta. Hata nyumba aloopangishiwa pale Dodoma ni balaa kodi yake wakati robotatu ya maisha na makazi yake ni hapa Dar! Bunge la anasa namna hii haliwezi kuihoji chochote Serikali. Ikulu ya Chamwino nayo ijengwe upya kwa ramani za kisasa. Iliyopo ilimfaa Mwalimu tu!
   
 20. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #20
  Jun 15, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kuepusha ugonjwa wa moyo najipa moyo kwamba sijaisomam wala kuisikia hii habari
   
Loading...