Bilioni 27.5 zilizotumika Sherehe za miaka 50 ya Uhuru zingeweza kununua mitambo 125 ya X-ray | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Bilioni 27.5 zilizotumika Sherehe za miaka 50 ya Uhuru zingeweza kununua mitambo 125 ya X-ray

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Jatropha, Jul 3, 2012.

 1. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #1
  Jul 3, 2012
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Ndugu wana bodi,

  Kwa muda mrefu sasa umekuwepo upotoshaji wa madai ya madaktari kwa lengo la kutaka kuwaaminisha wananchi kuwa madaktari wanapigania maslahi yao pekee. Jana Dr Chitage wa Jumuia ya Madakatari alitoa ufafanuzi mzuri katika taarifa ya habari kuwa katika vikao 6 vilivyofanyika baina ya madaktari na Serikali, 66% ya muda huo ulitumika kujadili namna Serikali itakavyoboresha sekta ya afya ikiwemo kuzifanyia hospitali zote hapa nchini ukarabati na kuzipatia vifaa vya tiba. Alitoa mfano kuwa katika madai yao madaktari walikuwa wakitaka kila hospitali ya wilaya ipatiwe mtambo wa X-ray, na akaenda mbali zaidi kwa kudai kuwa hivi tunavyozungumza hakuna hata hospitali hata moja ya umma ikiwemo Muhimbili yenye mtambo wa CT Scan.

  Kwa kuwa juzi Mhe Raisi Jakaya Kikwete akihutubia taifa alidai kuwa Serikali haina uwezo wa kifedha wa kutekeleza madaia ya madakatari, kwa hakika taarifa hizi za madakatari zimenifikirisha sana hasa kizingatiwa kauli ya Mtukufu Rais. Kwa hakika nilijiuliza maswali mengi sana Je ni kweli Tanzania ni nchi maskini kama Rasi anavyotaka wananchi tuamini?

  Ili kuzitendea haki pande zote mbili yaani Seikali inayodai haina uwezo wa kifedha kutekeleza madai ya madakatari; na madakatari wanaotaka kila hospitali ya wilaya ipatiwe mtambo wa X-ray pamoja na vifa vingine vya tiba niliamua kutazama upya vipaumbele vyeti kama taifa ili niweze kuunga mkono mdaia ya bRaisi Jakaya Kikwete kuwa Tanzania ni nchi maskini; ama kuwaunga mkono madaktari kuwa Seikali inao uwezo wa kutekeleza madai yao ikiwemo kuboreshwa maradafu kwa sekta ya afya ikiwemo kuboreshwa kwa miundo mbinu, mupatikanaji wa madawa na maslahi ya watumishi wa sekya ya afya.

  Katika kufanya hilo nilikumbuka hivi karibuni takribani miezi 6 iliyopita Serikali lilitumia takribani Bilioni 27.5 katika kuadhimisha sherehe za miaka 50 ya uhuru. kwa kuzingatia kuwa moja ya madaia ya madakatari ni kuwa kila hospiatalia katika ngazi ya wilaya ipatiwe mtambo wa X-ray kwa ajili ya uchunguzi wa wagonjwa. Kabla ya kuanzisha kwa mikoa mipya Tanznaia inakadiriwa kuwa wilaya 128. Hivyo niliingia katika mtandao na kutafuta bei ya mtambo mmoja wa X-ray na kugundua mtambo wa kisasa kabisa wa X-ray ni sawa na Dola 140,000 tu. Hivyo Bilioni 27.5 zilizotumika katika maadhimisho ya miaka 50m ya uhuru zingeweza kununua miatambo 125 kama hiyo pichani hapo chini.

  Kwa namna yoyoite ile kiwango kilichotumiwqa na Serikali inyoongozwa na Raisi Jakaya Kikwete miezi 6 iliyopita cha Bilioni 27.5 kwa maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru ni kikubwa mn. Hivyo sio sahihi kabisa kwa nchi inayoweza kutumia kiasi hiki cha fedha kwa sherhe tuu kudai kuwa ni nchi maskini. Kwa hakika ningewelewa zaidi Mhe Raisi Jakaya Kikwete kama kabla ya kufanya matumizi haya ya anasa angelihutubia taifa na kutuambia kuwa kutokana na uwezo mdogo wa kifedha wa Serikali ya Tanzania, nchi yetu itaadhimisha sherehe za miaka 50 ya uhuru kimya kimya lakini fedha zilizotengwa kwa ajili ya sherehe hizo kiasi cha Bilioni 27.5 zitatumika kununulia mitambo mipya ya X-ray ya kisasa kwa ajili ya hospitali za ngazi ya wilaya 125.
  [TABLE="width: 762"]
  [TR]
  [TD]Dola kwa kila mtambo mmoja wa wa Xray[/TD]
  [TD] Kiwango cha kubadili Dola kwa Tz Shs[/TD]
  [TD] Jumla ya Shilingi za Kitanzania zinzohitajika kununua mtamo mmoja wa X-ray[/TD]
  [TD] Kiasi cha fedha zilizotumika katika Sherehe za miaka 50 ya Uhuru Tar 09 Desemba 2011[/TD]
  [TD] Mitambo ya X-ray ya kisasa ambayo ingeweza kununuliwa na fedha hizo[/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD] 140,000[/TD]
  [TD] 1,570[/TD]
  [TD] 219,800,000[/TD]
  [TD] 27,500,000,000[/TD]
  [TD]125[/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Ndugu wanjf naomba tujiulize kwa kina ni nini athari za huu wimbo wa kila siku wa viongozi wetu hususan kutoka CCM kuwa sisi watanzania tu watu maskini na nchi yetu Tanzania ni maskini?

  Picha ya hapo chini ni moja ya mtambo wa kisasa wa X-ray unaoweza kununuliwa kwa Dola 140,000 tu Philips Diagnost 94 Remote Control System

  [​IMG]
   

  Attached Files:

 2. K

  Kima mdogo JF-Expert Member

  #2
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  halafu kuna mifala inasema Tanzania hakuna hela
   
 3. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #3
  Jul 3, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Shida ya nchi yetu ni vipa umbele na sio Ela!
   
 4. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #4
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,184
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Mkuu hizi ni hasira unatupa na stress wakati ndo tumetoka kula msosi wa mchana hapa
   
 5. Jimjuls

  Jimjuls JF-Expert Member

  #5
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 10, 2011
  Messages: 460
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 35
  Kwa hali hii unaweza kujikana sio mtanzania......au na sisi tuanzishe "BIMA YA ELIMU"
   
 6. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #6
  Jul 3, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  dah,,,,,mshukuru mungu kwa kula
   
 7. c

  cheichei2010 JF-Expert Member

  #7
  Jul 3, 2012
  Joined: Sep 18, 2010
  Messages: 932
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  si kuna mijitu mingine inatetea ujinga,hata haifikilii, na haya mabilioni yaliyoko nje wanasemaje?Bado zile fedha za EPA sijui hata kama zilitumika zilivyokusudiwa.Kuna hela za rada zinarudi utaona zinavyopigwa danadana,mpaka tusahau.Yaani hapa umezidishia njaa!
   
 8. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #8
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Zingewalipa Madaktari - Mishahara Mipya na Posho

  Zingewalipa Waalimu Malimbikizo ya Mishahara yao Wanayodai

  Hizo Sherehe ni Mitaji ya Viongozi na Watu kadhaa Ukiangalia Nchi za Magharibi hazina Sherehe kama hizo ni

  Nchi za kisoshalist na Kijamaa na iliyobaki ni CHINA tuu. Na CHINA wakishika Mwizi wa pesa hawajali wewe ni

  Nani ni kamba shingoni tu.
   
 9. Janja PORI

  Janja PORI JF-Expert Member

  #9
  Jul 3, 2012
  Joined: Jul 31, 2011
  Messages: 808
  Likes Received: 50
  Trophy Points: 45
  so hizo Billioni 200 za kuchukua madaktari nje ni sawa na mitambo ya X ray mingapi na hiyo machine ya scan ngapu
   
 10. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #10
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,184
  Likes Received: 565
  Trophy Points: 280
  Mkuu Bajabiri kwa hilo namshukuru Mungu sana
  Ila hawa watu wanatia hasira sana
  Kila siku ngonjera serikali haina hela ila za mambo ya ajabu ajabu na safari zao za nje kila siku ipo
  Za kualikana na kununua maVX zipo ila za maisha bora kwa wafanyakazi hazipo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 11. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #11
  Jul 3, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ccm ilaaniwe na ife milele
   
 12. t

  tara Senior Member

  #12
  Jul 3, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  kabisa,vipa umbele ni viburudisho wizarani na nauli za mweshimiwa dhaifu kwenda kupiga picha na kina 50 cent nje......vinginevyo tungekuwa mbali sana katika maendeleo.
   
 13. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #13
  Jul 3, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  tatizo letu huwa hatujui vipaumbele vyetu ni nini. Wanaotengeneza bajeti, huwa wanahakikisha katika mzunguko wao wanatenga pesa za kufanya events fulani ambazo kimsingi huwa hazina tija lakini ni namna ya kuhakikisha pesa za watanzania zinatumika. Juzi kumekuwepo na maonesho ya serikali za mtaa ALAT, pamoja na ukweli kuwa sherehe hizo zimesaidia baadhi ya mambo kuwa wazi kwa wananchi, lakini ni ukweli kuwa kiasi kikubwa cha hela kimetumika kwa shughuli hii.

  serikalini kutokana na watu kuwa na vipato visivyoridhisha, njia yao ya kupata pesa ni kupitia maadhimisho, sherehe, kongamano na mambo mengine ambayo wanalipana posho night za siku kadhaa
   
 14. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #14
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Na usisahau zili trilion 1.7 ambazo mashekh na maaskofu walituambia kuwa zinapotea kutokana na udanganyifu, ukwepaji wa kodi na misamaha ya kodi.
   
 15. pgasper

  pgasper JF-Expert Member

  #15
  Jul 3, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 311
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  liwalo na liwe
   
 16. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #16
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Na usisahau zile trilion 1.7 ambazo mashekh na maaskofu ktk tafiti zao walituambia kuwa zinapotea kutokana na udanganyifu, ukwepaji wa kodi na misamaha ya kodi.
   
 17. Yo Yo

  Yo Yo JF-Expert Member

  #17
  Jul 3, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 11,247
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 0
  Ritz njoo uone umbea huu.....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. m

  mob JF-Expert Member

  #18
  Jul 3, 2012
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,027
  Likes Received: 509
  Trophy Points: 280
  mkuu hii habari imenistua sana natamani wananchi wangelikuwa na uwezo wa kufikiria mambo kwa undani zaidi kungelileta mabadilika.
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  na kweli maana wengi tunapiga pasi ndefu yaani unapiga ukali asubuhi halafu mchana unajidai uko bize huendi kula mpaka jioni tena...hahahaah
   
 20. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #20
  Jul 3, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Nina mtoto wangu yuko hoi lakini nawaunga mkono madaktari...
   
Loading...