Bilioni 18 zilizokutwa katika akaunti ya wakili Arusha zina uhusiano na siasa za 2015?

mudavadi

Member
Apr 19, 2011
53
14
Itakumbukwa kwamba wiki karibu mbili zilizopita, wakili mmoja kijana wa mjini Arusha alitiwa mbaroni kutokana na kukutwa na takribani shilingi bilioni 18 kwenye akaunti yake ya ndani na uchunguzi wa awali umehusisha fedha hizi na shughuli haramu na sasa wakili huyo ameshafikishwa mahakamani na kusomewa mashitaka yake.

Habari zilizopatikana hivi karibuni zinadai kwamba fedha hizi, ambazo zinahusishwa na shughuli haramu za maharamia na kikundi cha Al Shabaab, zina mkono pia wa mmoja wa wanaowania kuteuliwa kugombea urais wa nchi hii kwa tiketi ya chama kimoja kikubwa, katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Inasemekana kwamba wakili huyu na mgombea huyu ni pete na chanda na mara nyingi amekuwa akimtumia katika masuala kadhaa yanayohitaji nguvu ya kifedha, kama vile michango ndani ya chama na hata shughuli za kiimani.

Sasa kama fedha haramu zinaruhusiwa kuingia katika utafutaji wa madaraka, mtu huyu akiingia madarakani, vitendo hivi haramu si vitahalalishwa?
 
malecela alivyochukua hela uarabuni na kuitwa abdala mwalimu alikemea vikali,akasema tumwogope kama ukoma.
kuna wengine wachuma hela haramu hapahapa nchini kwaajili ya madaraka 2015 wote ni wakuogopa kuliko ukoma.
 
Anayechukua toka Iran au anayetumia za EPA kwangu mie wote ni hatari tuu. Hivi sasa tunaona madhara ya watumia pesa kutafuta madaraka yanavyo tutafuna kwa mateso,no umeme,maji shida (Mwanza wazee wazima wanaoga ziwani) na upuuzi mwingine Kama maufisadi mbalimbali yanayoshindwa kukemewa kwa vile wafanya ufisadi huo wanajua siri ya Mfalme na Mfalme anaona akiwakemea wataitoa nje siri hiyo (hizo).
 
Kuna tetesi ya kwamba alilazwaga hapo Mount Meru hosptal,Je? Ameshatokaga? Na kuna tetesi ya kwamba kuna yule jamaa wa ile kampuni ya kitalii hp Arusha Mjini aliyehusishwa na mtandao wa Alshabaab na hata huyu naye alikuwa na shilingi ndefu sana,Je? Hajahusishwa na kuwa ki2 kimoja na huyu wakili Mwale?
 
malecela alivyochukua hela uarabuni na kuitwa abdala mwalimu alikemea vikali,akasema tumwogope kama ukoma.
kuna wengine wachuma hela haramu hapahapa nchini kwaajili ya madaraka 2015 wote ni wakuogopa kuliko ukoma.

Hapo kwenye majani, aliitwa JUMANNE
 
Hamna! Hakuna cha siasa wala urais wala nini. Mi Mwale namfahamu alishanipaga tenda kibao ofisini kwake za kazi ndogondogo, kifupi ni mtu wa madili, ni msomi lakini mishen-town flani anayedili na mafogo wa hapa, wengine majambazi. Sa ye ndo huwa anawarekebishia mambo yao ya kesi wanapokamatwa au kushtakiwa. Pia huwa anawafanyiaga udalali kuwauzia vitu vyao au kuwatafutia maplot ya biashara na kuwarekebishia mikataba nk. na hata wakiuza vitu vyao vya dili hela huwa anawapokelea halafu anakula commission, au anawasaidia kununua vitu halafu anakula commision yani kama hivyo. Kwa hiyo kuwa na hela za watu kwenye akaunti yake huwa ni kawaida sana tu. Mawakili wenye hela hapa A town hizo ndo dili zao. Kifupi kuna wenzie au washindani wamemchomea wamtoe sokoni.
 
hamna! Hakuna cha siasa wala urais wala nini. Mi mwale namfahamu alishanipaga tenda kibao ofisini kwake za kazi ndogondogo, kifupi ni mtu wa madili, ni msomi lakini mishen-town flani anayedili na mafogo wa hapa, wengine majambazi. sa ye ndo huwa anawarekebishia mambo yao ya kesi wanapokamatwa au kushtakiwa. pia huwa anawafanyiaga udalali kuwauzia vitu vyao au kuwatafutia maplot ya biashara na kuwarekebishia mikataba nk. Na hata wakiuza vitu vyao vya dili hela huwa anawapokelea halafu anakula commission, au anawasaidia kununua vitu halafu anakula commision yani kama hivyo. kwa hiyo kuwa na hela za watu kwenye akaunti yake huwa ni kawaida sana tu. Mawakili wenye hela hapa a town hizo ndo dili zao. Kifupi kuna wenzie au washindani wamemchomea wamtoe sokoni.

how old are u?
 
Nduka usitupotezee Bwn, haya mambo ni makubwa ya kuhujumu nchi, wewe unafurahia hao El-Shabab weje kwako utapona??? Wacha upuuzi, kama huna la kuchangia nyamaza kimya kama wengine!!!!!!!!!!!!!!

Kwa hiyo ili uone ninalo la kuchangia ulitaka nimtaje Lowassa? kuhusisha Al shabab kwenye hizi biashara za pesa haramu Arusha ni wehu.
 
Habari kubwa na ya kusikitisha kwamba Mwale Medium mtoto si riziki.
hiyo inawezekana kabisa,alipokuwa makumbusho dar kabla ya kuhamia arusha alikuwa na urafiki mkubwa na kijana mmoja mwenye tabia hizo,mpaka alipohama alimwachia nyumba aliyokuwa anakaa mwale na akaendelea kuilipia kodi!
 
Hamna! Hakuna cha siasa wala urais wala nini. Mi Mwale namfahamu alishanipaga tenda kibao ofisini kwake za kazi ndogondogo, kifupi ni mtu wa madili, ni msomi lakini mishen-town flani anayedili na mafogo wa hapa, wengine majambazi. Sa ye ndo huwa anawarekebishia mambo yao ya kesi wanapokamatwa au kushtakiwa. Pia huwa anawafanyiaga udalali kuwauzia vitu vyao au kuwatafutia maplot ya biashara na kuwarekebishia mikataba nk. na hata wakiuza vitu vyao vya dili hela huwa anawapokelea halafu anakula commission, au anawasaidia kununua vitu halafu anakula commision yani kama hivyo. Kwa hiyo kuwa na hela za watu kwenye akaunti yake huwa ni kawaida sana tu. Mawakili wenye hela hapa A town hizo ndo dili zao. Kifupi kuna wenzie au washindani wamemchomea wamtoe sokoni.

Mkuu, nashukuru kwa taarifa. kama ukiwa na taarifa tofauti na hizi utujuze mkuu
 
Hamna! Hakuna cha siasa wala urais wala nini. Mi Mwale namfahamu alishanipaga tenda kibao ofisini kwake za kazi ndogondogo, kifupi ni mtu wa madili, ni msomi lakini mishen-town flani anayedili na mafogo wa hapa, wengine majambazi. Sa ye ndo huwa anawarekebishia mambo yao ya kesi wanapokamatwa au kushtakiwa. Pia huwa anawafanyiaga udalali kuwauzia vitu vyao au kuwatafutia maplot ya biashara na kuwarekebishia mikataba nk. na hata wakiuza vitu vyao vya dili hela huwa anawapokelea halafu anakula commission, au anawasaidia kununua vitu halafu anakula commision yani kama hivyo. Kwa hiyo kuwa na hela za watu kwenye akaunti yake huwa ni kawaida sana tu. Mawakili wenye hela hapa A town hizo ndo dili zao. Kifupi kuna wenzie au washindani wamemchomea wamtoe sokoni.
Mtu B hapo kwenye bold ndio uko sahihi kabisa,kwa kifupi mshikaji ni master plan wa majambazi wengi hapo A-town,na kama tutamtendea haki basi anapaswa kuitwa Jambazi tu.Hivyo huwo mshiko katika account yake unaweza usihusiane kwa lolote na inshu za kisiasa zaidi ni inshu za kijambazi period
 
Wanaomjua huyo muwania urais 2015 watudadavulie humu tujue. Hilo la jamaa kuwa bwabwa wala siyo la siri tena. Wakati mmoja akiwa anafanya kazi pale TLC (CCM) mkoa alikutwa anafanyiwa mchezo mbaya na mmoja wa 'jamaa' zake. Watu kama hawa watatumaliza kwenye hii nchi maana usikute hata hao Al Shabaab na maharamia anawaweka humu humu nchini.
 
Mtu B hapo kwenye bold ndio uko sahihi kabisa,kwa kifupi mshikaji ni master plan wa majambazi wengi hapo A-town,na kama tutamtendea haki basi anapaswa kuitwa Jambazi tu.Hivyo huwo mshiko katika account yake unaweza usihusiane kwa lolote na inshu za kisiasa zaidi ni inshu za kijambazi period

Kwa kuangalia size ya fuba lililokamatwa, ufuatiliaji wa karibu wa Interpol (na hata serikali za nchi za magharibi ikiwemo USA), suala la kwamba fedha hizi ni matokeo ya ujambazi halipo (japo inafahamika kwamba jamaa ndiye benki ya majambazi). Kwanza ielewe kwamba hakuna tukio kubwa la ujambazi lililojitokeza na hata kuripotiwa hivi karibuni ambalo linaweza kuhusishwa na fedha nyingi kiasi hiki. Pili, as long as tukio hilo siyo cross border na ambalo halitishii mali au usalama wa Marekani, suala la ufuatiliaji wa Marekani lisingeingia hapa. Hakika suala hili ni kubwa na lina uhusiano wa moja kwa moja na vitendo ambavyo vinatishia usalama wa kimataifa and what comes closest ni uharamia na hilo la ugaidi wa Al Shabaab.

Huyo mgombea anayetajwa humu hakuwekwa bayana lakini kwa wafuatiliaji wa mambo ya A-Town si vigumu kujua huyo ni nani maana hata kwenye harambee za kanisa huonekana wote.
 
Back
Top Bottom