Kaka Pekee
JF-Expert Member
- Apr 3, 2018
- 336
- 559
Tanzanian Tycoon Rostam Aziz Sells Last Tranche Of Vodacom Shares For $220 Million
Tajiri Kongwe nchini Tanzania Rostam Aziz, Hatimaye amemalizia Ngwe ya Mwisho ya Mauzo fungu la mwisho la Hisa zake za Vodacom Tanzania kwa kuwauzia Vodacom South Africa.
Kwa Mujibu wa report kutoka Citizen newspaper, Aziz ameuza fungu lake la 588 million (Shea) iliyokuwa imebaki Vodacom Tanzania, ambayo ilikuwa ikisimamiwa na Mirambo Holdings, Moja ya kampuni zake za uwekezaji kwendaVodacom South Africa, kwa dili lililokamilishwa kupitia Dar es Salaam Stock Exchange Jumatano iliyopita.
Shea (Shares) hizo zilithaminishwa kwa takribani dola milioni mbili na ishirini $220 wakati wa mauzo. Msemaji wa Vodacom Tanzania hakutaka kutoa ushirikiano wakati alipoombwa kutoa maoni yoyote juu ya hilo.
Dili hilo limekuja karibu Miezi kumi tangu 'Washikadau' (shareholders) wa Dar es Salaam Stock Exchange-kuorodhesha kupitishwa kwa mauzo ya sehemu ya Mirambo Holdings iliyobaki Vodacom Tanzania
Rostam Aziz (55) ndiye aliyewezesha kuingia kwa Vodacom South Africa nchini Tanzania, awali alikuwa akimili wastani wa asilimia ya 35% fungu ndani ya Vodacom Tanzania.
Mwaka 2014, aliuza asilimia 17.2% ya fungu la Vodacom Tanzania iliyokuwa ikimilikiwa na kampuni yake ya binafsi ya uwekezaji Cavalry Holdings, iliyosajiliwa Jersey Island ikiwa na umiliki wa 17.8% ya hisa.
Rostam Aziz, ni bilionea wa kwanza nchini na bado anaongoza kwa biashara. Mbali na kumiliki hisa zake Vodacom Tanzania, amepata utajiri mkubwa kupitia mikataba ya uwekezaji na ujenzi wa Biashara za Mgodi Caspian Mining, Bandari ya Dar es Salaam, Majengo ya Biashara na Makazi nchini na Mashariki ya kati sambamba na uwekezaji kupitia vyombo vya habari nchini Tanzania (Channel Ten/Magic FM/ DTV/CTN/C2C nk).
Mwezi July Mwaka huu alizindua Biashara ya kiwanda cha Ujazaji gesi, Dar es Salaam (Petroleum Gas-LPG) yenye thamani ya dola za kimarekani $65Millioni.