Bila ya Rehema yake mwenzenu basi tena

Bila ya Rehema yake mwenzenu basi tena

wewe sikia acha kujilizaliza MP nikupe watoto wa kutosha wanaotaka ndoa unaishi dunia gani wewe ???

Note: Wadada hawatafutwagi wewe kuwa busy wanakujaga wenyewe ni wewe tu kuangalia yupi ni yupi issue ujue KUJIPOSITION
 
Mmmm!!!
 

Attachments

  • ImageUploadedByJamiiForums1445577158.039028.jpg
    ImageUploadedByJamiiForums1445577158.039028.jpg
    21.1 KB · Views: 166
Hahahahahah

Nimewahi kua na washkaji wengi walio kama mleta mada

Its real desperate pole mkuu kosa lako ni moja tu dunia ipo kasi zaidi kuliko mwendo wako!
 
You are just desperate and i tell you wont succeed. Ni kosa kwenda kanisani ukiwa unapepesa macho uone msichana wa kuoa maana inaonekana hata ibada hufanyi ila unaenda kuangalia nyago za waschana na kukompea huyu kaolewa au bado. Unajitaabisha kuomba wakati hujui unaomba ili Mungu afanye nini. Mungu ni independent na hasaidiwi kazi. Wakati anampa mke adam hakuna mtu alomsaidia, wakati anampa mke Isaka hakuna mtu alomsaidia. Ukiamua kufata principle za Biblia kutafta mke hakikisha unamlingana Mungu vizuri ili kila hatua utakayofanya ifanyike kwa uongozi wa roho mtakatifu. Waone wazee wa kanisa au mchungaji wakusaidie tatizo lako kama umeshindwa. Ila naamini kama ungejua unachofanya usingefika kote huku tatizo kuna tatizo mahali kwenye kichwa chako upande wa rohoni na mwilini. Asomaye na afahamu.

Na shukuru ndugu ila naomba nijitetee kusema sijui ninachokiomba si mimi tu nisiejua bali ni wote hatujui na ndio maana Yesu ndie atuombeaye kwa Mungu, kusema naenda kanisani kwaajili ya kutafuta wadada nakiri tokea moyoni sijawai fanya hivyo nasema hivyo kwani yote huanzia ndani ya dhamiri na dhamiri yangu niendapo kanisani ni kusali kuomba na kuabudu na si vinginevyo. Hayo ya kumpenda mtu ndani ya kanisa hutokea tuu kama itokeavyo sehemu nyingine, sasa kuna ubaya gani kumuomba Mungu akupe mwongozo kwa msichana fulani ambae umesha mpenda? Mf, wakati fulani sikuwa na kazi, nikamuomba Mungu anipatie kazi, na aliponifanikishia sikuomba tena kupata kazi bali niliomba ile kazi niifanye kwa ufanisi. Nilipokua sijampata mtu niliempenda niliomba kwa Mungu anikutanishe nae, sa katika ubinadamu. Kuna hisia za upendo, nilipo muona mtu fulani nilivutiwa nae, nilienda mbele ya Mungu kumwambia juu ya fulani kama ndie au la, kama ndie kuwepo na wepesi kumfikishia ujmbe na akiupokea kwa amani basi ndie, ikiwa sivyo basi sie, naendelea tena na maombi ila kwa sasa ni kwaajili asie kuwepo, akitokea namshirikisha Mungu kumbuka alisema njooni tusemezane leteni hoja zenu tujadiliane, sa kosa langu wapi wakati muda wote siachi kumshirikisha Mungu?
 
Back
Top Bottom