Bila tija mshahara usiongezwe serikalini

Bila tija mshahara usiongezwe serikalini

Watumishi wa umma ni wavivu, wamekosa ubunifu na bado wanalilia mshahara uongezwe Mei Mosi. Nashauri pasiongezwe hata senti mpaka pathibitishwe kuongezeka kwa tija, tuwapime mpaka 2019 labda.
Mnataka tija wakati budget inatekelezwa kwa % zisizo na tija.
 
uko sahihi sana

lazima KPI iwe introduced kwa wafanyakazi wa serikali

wengi wavivu, hawajielewi, hawajiamini, hawajui procedures, sio wabunifu, hawana kipya yaani....
Jamani tusitake kuvuna tusipo panda. Niliwahi kufanya kazi serekalini budget nilizo panga hazikuwahi kutekelezwa kwa zaidi ya asilimia 40!, kwa muda wa miaka 3 mfululizo. Wakati naondoka niliwashauri waajiri mtu wa elimu ya chini ya ile ya kwangu kwani kazi zile zilikuwa ndani ya uwezo wake na mshahara wake ulikuwa chini.
 
Unataka tija kutoka kwa mtumishi Bila we kumpa. Motisha Na tija ni kama pande mbili Za shilingi.Vyote vinaenda pamoja.
 
Watumishi wa umma ni wavivu, wamekosa ubunifu na bado wanalilia mshahara uongezwe Mei Mosi. Nashauri pasiongezwe hata senti mpaka pathibitishwe kuongezeka kwa tija, tuwapime mpaka 2019 labda.
Tija ys kiserikali iko vipi hebu fafanua sio unaropoka maneno usiyoyajua!
 
Motisha ongeza tija...mshaurini vzr huyo baba bashite anayejidhania ni genius.
 
Huyu atakua katumwa na Lumumba kuisemea maana serikali yake ya awamu ya 5 Rais wake mpendwa kachemka ktk kila nyanja kwanza kashindwa kwenye ajira nadhan ata uyu ni mmoja wapo,kashindwa kuboresha maslahi ya watumishi mwaka wa Tatu sasa,kashindwa kupandisha madaraja mwaka wa pili sasa ila alichofanikiwa ni kuchezea fedha za maskini kununua madiwan,wabunge wa upinzani ili serikali yake isikumbushwe madhaifu yake! Poor this government
 
Kweli kila walipo 4 mmoja mwehu hakukosea yule Dr wa muhimbili.
 
Hahaha utawaua huko serikalini, tija ni msamiati mpya huko. Lini na wapi serikali ikaleta tija?!
 
Watumishi wa umma ni wavivu, wamekosa ubunifu na bado wanalilia mshahara uongezwe Mei Mosi. Nashauri pasiongezwe hata senti mpaka pathibitishwe kuongezeka kwa tija, tuwapime mpaka 2019 labda.
Fafanua hiyo tija serikalini!
 
Back
Top Bottom