Bila Samia, Taifa Stars wasingefuzu

Bila Samia, Taifa Stars wasingefuzu

Hongera Samia kwa kuwezesha Taifa Stars kufuzu mpambano wa ubingwa wa soka Afrika.

Bila uwezo wako wa ajabu wa kutenda miujiza, haya yangetokeaje? Nakushukuru sana rais.

Hawa Taifa Stars wanapaswa kukupongeza wewe na siyo wewe kuwapongeza. Maana, kila walipokuwaza, nguvu zao za kimwili ziliongezeka. Kila wakiwazia picha yao, misuli yao ilizidi kupata nguvu. Kila wakikumbuka kushindwa, waliogopa kutekwa na kupotezwa. Pia, waliogopa kuvuruga amani. Hakuna kitu kimewawezesha kama kuwa nje wakizungukwa na mabeberu.

Kama wazalendo, wakikukumbuka wewe mlezi na mhimili wa taifa anayehurumia viumbe wote hata wadudu kama chawa, wallingiwa na mori wa kushinda.

Wakikumbuka matendo yako, huwa kama wamasai wakiogopa kushindwa na kujikuta wasikotaka.

Wakimkumbuka Abduli ndiyo usiseme. Ilikuwa ni lazima washinde.

HONGERA SAMIA KWA TAIFA STARS KUFUZU.
Screenshot_20251222-120716~2.png
 
Watu hawajakuelewa.. pole sana.
 
Wakati wa SAMIA

SIMBA + YANGA - final CAF Conferederation..2023 & 2024

STARS - 16 bora AFCON....2025
 
Hakika mkuu unakipaji cha kupaka waja mafuta kwa mgongo wa chupa ... Fasihi ni ukoko, mwandishi ni kijiko kwangua
 
Back
Top Bottom