Adamu na Hawa Walizaa Watoto Wengine Zaidi ya Kaini na Abeli
Mwanzo 5:4
"Siku za Adamu baada ya kumzaa Sethi zilikuwa miaka mia nane; akazaa wana, waume na wake."
Hili andiko linaonyesha kuwa Adamu na Hawa walizaa watoto wengi – “wana, waume na wake”, sio Kaini na Abeli tu. Kwa hiyo, Cain aliweza kumuoa dada yake au mpwa wake (binti wa ndugu yake wa damu).
Kaini Alikimbilia Nchi ya Nodi na Kuoa huko , ushahidi wa maandiko huu hapa👇👇👇
Mwanzo 4:16-17
"Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mashariki mwa Edeni. Kaini akamjua mkewe, naye akachukua mimba, akazaa Henoko."
Jibu la wazi ni kwamba Biblia haijaorodhesha kila uzao kwa mpangilio wa wakati, bali inatoa tu matukio makubwa. Kaini aliweza kumuoa dada yake au mjukuu wa Adamu – kumbuka, watu waliishi miaka mingi (zaidi ya miaka 900 kwa Adamu – Mwanzo 5:5), hivyo uzao ulienea mapema.
Kuoa Dada Yako Halikuwa Dhambi,Katika nyakati za mwanzo za binadamu, sheria ya kuzuia ndoa za damu haikuwa imewekwa bado.
Mambo ya Walawi 18:9 (Sheria hii ilikuja baadaye)
"Uchi wa dada yako, binti ya baba yako au binti ya mama yako, mzaliwa nyumbani au nje, usimfunue uchi wake."
Sheria hii ilikuja kupitia Musa maelfu ya miaka baadaye. Katika mwanzo wa historia ya binadamu, ilikuwa ni lazima binadamu wa kwanza waoe ndugu zao ili jamii iendelee.
Uwepo wa Watu Mashariki mwa Edeni (Nchi ya Nodi),Haimaanishi kwamba walikuwepo watu wengine tofauti na uzao wa Adamu. Hii inaonyesha kwamba muda mrefu ulipita, uzao wa Adamu ulienea, na baadhi yao walikuwa wanaishi maeneo ya mbali kama Nodi. Biblia haisemi kila kitu kwa undani wa historia ya kila mtoto wa Adamu.