Mi nimefurahishwa sana na nyimbo ya John Komba aliyoitoa hivi karibuni na kutamba kwenye Mkutano Mkuu Kizota kuwa Bila ya CCM Nchi Ingekuwa Wapi? Ni hakika kuwa motto anapokuwa hajala mchana ukimtuma dukani mbio anakwenda ila akishiba ndo anaanza kiburi na kukataa kutumwa na hata kuanza kukandia ugali maharage aliokula mchana na hata nyama akisema kila siku nyama kila siku nyama. Hii ndio hali halisi ambayo wananchi wengi wa Tanzania hasa wapinzani wa siasa wa CCM wamekutwa nayo. Wengi walisomeshwa na mamilioni ya serikali zilizopita za CCM na wengi bado wanaitegemea serikali ya CCM iliyopo kusomesha watoto wao kwa mikopo ilhali wao wenyewe (wazazi) wakiwa kwenye maofisi ya serikali ya CCM wakiiba hela za serikali na kuishia kulaumu. Wote tunatembelea kwenye barabara za lami na safari ya Mwanza sasa ni masaa 12 kutoka Dar na mengineyo mengi ambayo kila mmoja anayafahamu. Mimi nadhani hata humu JF kila mmoja ajiulize mazuri aliyotendewa na anayoendelea kutendewa na CCM na serikali zake sio kuangalia negatives tu ambazo kila kiumbe anazo. Unaweza msema baba ako neno lolote unalotaka lakini huwezi tukana hata maungo yake! Tujiulize kwanini tuichukie CCM? Kwa kipi na yote haya mazuri ya CCM na serikali zake? Big Up John Komba!