Bila CCM sisi Tungekuwa Wapi?

golii

Member
Nov 13, 2012
48
1
Mi nimefurahishwa sana na nyimbo ya John Komba aliyoitoa hivi karibuni na kutamba kwenye Mkutano Mkuu Kizota kuwa Bila ya CCM Nchi Ingekuwa Wapi? Ni hakika kuwa motto anapokuwa hajala mchana ukimtuma dukani mbio anakwenda ila akishiba ndo anaanza kiburi na kukataa kutumwa na hata kuanza kukandia ugali maharage aliokula mchana na hata nyama akisema kila siku nyama kila siku nyama. Hii ndio hali halisi ambayo wananchi wengi wa Tanzania hasa wapinzani wa siasa wa CCM wamekutwa nayo. Wengi walisomeshwa na mamilioni ya serikali zilizopita za CCM na wengi bado wanaitegemea serikali ya CCM iliyopo kusomesha watoto wao kwa mikopo ilhali wao wenyewe (wazazi) wakiwa kwenye maofisi ya serikali ya CCM wakiiba hela za serikali na kuishia kulaumu. Wote tunatembelea kwenye barabara za lami na safari ya Mwanza sasa ni masaa 12 kutoka Dar na mengineyo mengi ambayo kila mmoja anayafahamu. Mimi nadhani hata humu JF kila mmoja ajiulize mazuri aliyotendewa na anayoendelea kutendewa na CCM na serikali zake sio kuangalia negatives tu ambazo kila kiumbe anazo. Unaweza msema baba ako neno lolote unalotaka lakini huwezi tukana hata maungo yake! Tujiulize kwanini tuichukie CCM? Kwa kipi na yote haya mazuri ya CCM na serikali zake? Big Up John Komba!
 
NIngeweza kukubaliana na wewe ndugu yangu golii kama hao viongozi wasafi sana wa CCM yako wangekuwa wanamuogopa Mungu na kulinda raslimali za taifa letu.Lakini kwa sababu ya ulafi wao kwangu mimi hakuna walichokifanya.Hao waliojilimbikizia mali ndio waliopata nafasi za kusomeshwa bure lakini anagalia wanachokifanya.Ingekuwa amri yangu ningewanyonga wote.
 
Huyu Golii anajua hela zinazofanya hayo maendeleo kidogo zinatoka mifukukoni mwa hao ccm mafisadi
Mkuu hizo ni kodi zetu zinazopanda kila uchwao,ccm ni wezi wezi ,na tutawatoa 2015
 
Bila sisiemu, kiwango cha umaskini kingekuwa kimeshapungua kwa kiasi kikubwa sana.
Bila sisiemu, hali ya maisha kwa wananchi walio wengi ingekuwa nzuri. M
Bila sisiemu, miundombinu ya barabara, reli, bandari, viwanja vya ndege n.k. ingekuwa mizuri.
Bila sisiemu, viwanda vyetu vingekuwa vimeimarika na kuongeza uzalishaji zaidi kwa ajili ya soko la ndani na nje.
Bila sisiemu, huduma za jamii kama vile afya, maji, umeme n.k. zingekuwa zinapatikana vizuri kwa gharama nafuu, na kwa uhakika zaidi.
Bila sisiemu, vongozi wa sisiemu na serikali wasingekuwa wanaenda kutibiwa nje ya nchi.
Bila sisiemu, chaguzi zetu zingekuwa za huru na haki na msamiati wa kuchakachua usingekuwepo
Bila sisiemu, rasilimali za nchi zingekuwa zinanufaisha wananchi na sio wageni.
Bila sisiemu, twiga wetu wasingekuwa wanapanda ndege.
Bila sisiemu, mchanga wetu wenye dhahabu na vito vingine vya thamani usingekuwa unasafirishwa kwenda nje.
Bila sisiemu, EPA, Meremeta, Tangold na yanayofanana na hayo yasingekuwepo.
Oohhh orodha ni ndefu.....unaweza kuendeleza hapa. Kubumbuka kuanza na kibwagizo hiki 'bila sisiemu'.......
 
Mi nimefurahishwa sana na nyimbo ya John Komba aliyoitoa hivi karibuni na kutamba kwenye Mkutano Mkuu Kizota kuwa Bila ya CCM Nchi Ingekuwa Wapi? Ni hakika kuwa motto anapokuwa hajala mchana ukimtuma dukani mbio anakwenda ila akishiba ndo anaanza kiburi na kukataa kutumwa na hata kuanza kukandia ugali maharage aliokula mchana na hata nyama akisema kila siku nyama kila siku nyama. Hii ndio hali halisi ambayo wananchi wengi wa Tanzania hasa wapinzani wa siasa wa CCM wamekutwa nayo. Wengi walisomeshwa na mamilioni ya serikali zilizopita za CCM na wengi bado wanaitegemea serikali ya CCM iliyopo kusomesha watoto wao kwa mikopo ilhali wao wenyewe (wazazi) wakiwa kwenye maofisi ya serikali ya CCM wakiiba hela za serikali na kuishia kulaumu. Wote tunatembelea kwenye barabara za lami na safari ya Mwanza sasa ni masaa 12 kutoka Dar na mengineyo mengi ambayo kila mmoja anayafahamu. Mimi nadhani hata humu JF kila mmoja ajiulize mazuri aliyotendewa na anayoendelea kutendewa na CCM na serikali zake sio kuangalia negatives tu ambazo kila kiumbe anazo. Unaweza msema baba ako neno lolote unalotaka lakini huwezi tukana hata maungo yake! Tujiulize kwanini tuichukie CCM? Kwa kipi na yote haya mazuri ya CCM na serikali zake? Big Up John Komba!

Cha muhimu unachotakiwa kujiuliza hapa ulipo ni lini ulitakiwa uwe hapa? Mimi jibu langu BILA CCM TUNGEKUWA WAPI? napenda kukujibu tungekuwa tumeendele kuliko AFRIKA KUSINI iwapo CCM isingekuwepo madarakani kwani tumeshuhudi wizi usiovumilika juu ya rasilimali zetu.
 
Bila ya CCM uamusho na mihadhara ya dini isingekuweepo; Bila ya CCM wizi wa raslimali zetu usingekuwepo. Bila ya CCM tungeendelea zaidi. Bila ya CCM udini usingekuwepo. Bila ya CCM viongozi wala rushwa wasingekuwepo. Bila ya CCM elimu ingekuwa bure. Bila ya CCM umeme, maji na huduma za afya zingekuwepo
Mi nimefurahishwa sana na nyimbo ya John Komba aliyoitoa hivi karibuni na kutamba kwenye Mkutano Mkuu Kizota kuwa Bila ya CCM Nchi Ingekuwa Wapi? Ni hakika kuwa motto anapokuwa hajala mchana ukimtuma dukani mbio anakwenda ila akishiba ndo anaanza kiburi na kukataa kutumwa na hata kuanza kukandia ugali maharage aliokula mchana na hata nyama akisema kila siku nyama kila siku nyama. Hii ndio hali halisi ambayo wananchi wengi wa Tanzania hasa wapinzani wa siasa wa CCM wamekutwa nayo. Wengi walisomeshwa na mamilioni ya serikali zilizopita za CCM na wengi bado wanaitegemea serikali ya CCM iliyopo kusomesha watoto wao kwa mikopo ilhali wao wenyewe (wazazi) wakiwa kwenye maofisi ya serikali ya CCM wakiiba hela za serikali na kuishia kulaumu. Wote tunatembelea kwenye barabara za lami na safari ya Mwanza sasa ni masaa 12 kutoka Dar na mengineyo mengi ambayo kila mmoja anayafahamu. Mimi nadhani hata humu JF kila mmoja ajiulize mazuri aliyotendewa na anayoendelea kutendewa na CCM na serikali zake sio kuangalia negatives tu ambazo kila kiumbe anazo. Unaweza msema baba ako neno lolote unalotaka lakini huwezi tukana hata maungo yake! Tujiulize kwanini tuichukie CCM? Kwa kipi na yote haya mazuri ya CCM na serikali zake? Big Up John Komba!
 
Tungekuwa na kina Sugu,Lema Kama viongozi wa nchi nafikiri jibu utamalizia mwenyewe
 
Back
Top Bottom