Bil 3/- zatua Mwanza kulipa fidia ujenzi daraja Kigongo - Busisi

elivina shambuni

JF-Expert Member
May 31, 2018
461
295
1578388755484.png

JUMLA ya Sh bilioni 3.145 zimepokelewa mkoani Mwanza na Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kwa ajili ya kuwalipa fi dia wananchi. Watu hao ni watakaopisha ujenzi wa Daraja la Kisasa la Kigongo- Busisi lililopo Wilaya za Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza. Hilo ndilo daraja refu zaidi katika Afrika Mashariki (EAC).

Hayo yalielezwa jana wilayani hapa na Kaimu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Mwanza, Pius Mwami alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kuanza kwa malipo ya fidia kwa wananchi. Malipo hayo ya fidia ni ahadi iliyotolewa na Rais Dk John Magufuli wakati wa ziara yake ya kikazi Desemba 7 mwaka jana.

Alisema Rais Magufuli alipokuwa katika ziara ya kikazi Desemba mwaka jana, aliahidi kuwa serikali ingetoa fedha kwa ajili ya kuwalipa wananchi wanaostahili kulipwa fidia hiyo kwa mujibu wa sheria. “Tayari tumepokea fedha shilingi bilioni 3.145 ambayo ni ahadi iliyotolewa na yeye kwa ajili ya kuanza kuwalipa wananchi fidia ili waweze kupisha ujenzi wa daraja letu la Kigongo- Busisi,” alisema. Alisema fedha hizo ambazo tayari zimewasili mkoani Mwanza, zinatarajia kulipa fidia jumla ya kaya 165, ambapo kaya 132 ni za maeneo ya Kigongo na kaya 33 ni za Busisi.

Alifafanua kuwa pia jumla ya makaburi 75 katika eneo la Kigongo na matatu yaliyoko Busisi, nayo yatafidiwa kupitia kiasi hicho cha fedha, kilichotolewa na serikali. “Tunamshukuru sana Rais wetu kwa kutoa fedha hizi kwa wakati, ambazo naamini zitarahisisha shughuli za ujenzi huu,” alisema. Aliongeza kuwa wananchi wote wanaostahili kulipwa fidia zao, watalipwa, kwa mujibu wa sheria. Alisema hakuna mwananchi ambaye hatalipwa
 
Safi Sana maendeleo hayana chama waharakishe kulikamilisha kabla hajatoka madarakani pesa zisijeliwa
 
Siku hizi Bunge hawana kazi. Mambo ambayo yangetokea bungeni kwenda kwenye utekelezaji saivi yanatoka kwa jiwe moja kwa moja Bunge nalo linapata habari hizi kama sisi. TWAFWAAAA!
 
JUMLA ya Sh bilioni 3.145 zimepokelewa mkoani Mwanza na Serikali kupitia Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS), kwa ajili ya kuwalipa fi dia wananchi. Watu hao ni watakaopisha ujenzi wa Daraja la Kisasa la Kigongo- Busisi lililopo Wilaya za Misungwi na Sengerema mkoani Mwanza. Hilo ndilo daraja refu zaidi katika Afrika Mashariki (EAC).

Hayo yalielezwa jana wilayani hapa na Kaimu Meneja wa Tanroads Mkoa wa Mwanza, Pius Mwami alipokuwa akitoa taarifa kwa waandishi wa habari juu ya kuanza kwa malipo ya fidia kwa wananchi. Malipo hayo ya fidia ni ahadi iliyotolewa na Rais Dk John Magufuli wakati wa ziara yake ya kikazi Desemba 7 mwaka jana.

Alisema Rais Magufuli alipokuwa katika ziara ya kikazi Desemba mwaka jana, aliahidi kuwa serikali ingetoa fedha kwa ajili ya kuwalipa wananchi wanaostahili kulipwa fidia hiyo kwa mujibu wa sheria. “Tayari tumepokea fedha shilingi bilioni 3.145 ambayo ni ahadi iliyotolewa na yeye kwa ajili ya kuanza kuwalipa wananchi fidia ili waweze kupisha ujenzi wa daraja letu la Kigongo- Busisi,” alisema. Alisema fedha hizo ambazo tayari zimewasili mkoani Mwanza, zinatarajia kulipa fidia jumla ya kaya 165, ambapo kaya 132 ni za maeneo ya Kigongo na kaya 33 ni za Busisi.

Alifafanua kuwa pia jumla ya makaburi 75 katika eneo la Kigongo na matatu yaliyoko Busisi, nayo yatafidiwa kupitia kiasi hicho cha fedha, kilichotolewa na serikali. “Tunamshukuru sana Rais wetu kwa kutoa fedha hizi kwa wakati, ambazo naamini zitarahisisha shughuli za ujenzi huu,” alisema. Aliongeza kuwa wananchi wote wanaostahili kulipwa fidia zao, watalipwa, kwa mujibu wa sheria. Alisema hakuna mwananchi ambaye hatalipwa
Inasikitisha sana kuona tunatumia bilioni 700 kujenga daraja kuunganisha wilaya mbili ambazo kimsingi zote zipo ng'ambo moja. Fedha hizo zingetosha kujenga barabara ya lami ya km 700. Tunayo makao makuu ya mikoa ambayo haijaunganishwa na lami. Kweli tunahitaji kuondokana na udikteta la siyo tutapoteza fedha nyingi sana kwasababu ya wanasiasa wanaotaka kusafisha njia zao kuelekea uchaguzi.
 
Back
Top Bottom