Harafu kingine nachotaka kufahamu kuna mdau hapo juu amesema Oscar ana PHD.Ni kweli??
Jamani kama anayo na pamoja mambo yote yanawezekana lakini kwa umri huo naanza kupatwa nawasisi wasiwasi hata kwa umri wake. Jamani miaka 29 una PHD bongo aahhh teh teh teh teh.
Passport yake ina jina la Oscar Rwegasira Mkasa na hata kwenye fomu ya tume amejaza majina yote matatu.
Suala la uraia wa Oscar ni jambo ambalo chadema wamekuta linazungumziwa kila kona ya biharamulo. Katika kura za maoni za ccm, Oscar alisema na ilirekodiwa na kurushwa na Biharamulo Cable TV kwamba yeye amezaliwa wilaya ya Biharamulo. Kijiji alichosema amezaliwa wanakijiji wanakataa na kusema wazazi wake sio watu wa hapo bali ni wahamiaji, tena wa miaka ya karibuni (around late 1980s) wakati Oscar ameshazaliwa. Oscar anaweza kuwa raia wa Tanzania lakini amelikoroga mwenyewe. Utata kwamba amezaliwa wapi ni yeye mwenyewe ameuanzisha kwa kutokuwa makini. Na jinsi alivyojaza fomu (at least iliyokuwa available to the public) kumeibua maswali mengi kuliko majibu.
Barua ya kutupilia mbali pingamizi la chadema ilipitia au ilitengenezwa Chato na siyo Biharamulo mjini kwenye halmashauri na ofisi za mkurugenzi. Kwani watu walioko Chato waliweza kuisoma na kuivujisha kabla haijafika biharamulo. Hapa kuna maswali mengi ya kujiuliza kwanini?
Chadema wameshauriwa na mawakili pamoja na ccm "anti-oscar" wang'ang'anie issue ya kutojaza fomu sawasawa. Kimsingi fomu ni moja na siyo mbili. Mkurugenzi kusema amepokea fomu mblili tofauti anakiri kwamba ama ameshindwa kazi yake kwa kushindwa kuhakiki hizo fomu (kipengele cha tatu hakikujazwa and it was so obvious) au ameshirikiana katika kugushi fomu alizokuwa nazo yeye kwenye ofisi yake.
Mkuu wewe ni mtu makini sana katika hoja zako lakini katika hili nadhani inabidi ufanye utafiti zaidi. WABONGO SIKU HIZI WAMEAMKA MKUU: Personally najua vijana kama 3 wamemaliza shule zao pale mlimani kwenye 200/2004 sasa hivi wako ukingoni mwa PhD zao na bado hata miaka 30 hawajafika. Mkuu na hawa siyo watoto wa mafisadi...ila ni wabongo wenzetu wamehaingaika kama sisi. Sema tuu ni kujiwekea priorities na kujua/kupata right channels.Kwa hiyo PhD kabla ya 30 inawezekana kabisa. Ushauri wangu..kama uko nje mwanangu beba box na ule kitabu otherwise ukija bongo na associate degree yako ya community college ni wachache watakaobabaika eti umesoma majuu (no pun intended bro!)
mkono wa magufuli upo hapo.......
Naam!
Kwanini kuna suala la Uhamiaji wakati yeye ni Mtanzania?
naam!
Mimi kwangu halina mantiki kwakuwa sidhani wahamiaji haramu wanapitiaga ofisi za uhamiaji. Lakini kama nilivyosema hapo awali Oscar anajilipua yeye mwenyewe na issue ya uraia kwa kutokuwa makini. Kwa mfano, kwenye uzinduzi wa kampeni (ingawa alikuwa haruhusiwa kufanya kampeni) mama yake inasemekana alikuwa mgonjwa alishindwa kufika, basi yeye alimyanyua mwanamke mwingine na kudai ndiyo mama yake mzazi wakati watu wanafahamu huyo sio mama yake mzazi. Ilileta miguno no minong'ono kwanini anadanganya wakati si lazima mama yake awepo pale? Watu wanajiuliza anaficha nini?
Wanavyodai wabishi wa Biharamulo ni kwamba alitaka ku prove hamna records uhamiaji inayosema aliingia tanzania kutoka uganda katika huo mwaka aliotajwa na chadema kwamba ndio aliohamia tanzania.
Mimi kwangu halina mantiki kwakuwa sidhani wahamiaji haramu wanapitiaga ofisi za uhamiaji. Lakini kama nilivyosema hapo awali Oscar anajilipua yeye mwenyewe na issue ya uraia kwa kutokuwa makini. Kwa mfano, kwenye uzinduzi wa kampeni (ingawa alikuwa haruhusiwa kufanya kampeni) mama yake inasemekana alikuwa mgonjwa alishindwa kufika, basi yeye alimyanyua mwanamke mwingine na kudai ndiyo mama yake mzazi wakati watu wanafahamu huyo sio mama yake mzazi. Ilileta miguno no minong'ono kwanini anadanganya wakati si
lazima mama yake awepo pale? Watu wanajiuliza anaficha nini?
Mzee mwana kijiji kuhusu suala la kumjua mama ushahidi unaweza kupatikana tatizo angekuwa ni baba hilo ndiyo lingekuwa tatizo kuthibitisha kama kweli ni baba yake.mmh.. sasa nani anajukumu la kuthibitisha kuwa huyo ni mama yake au si mama yake? Yeye akisema ni mama yake, watu wengine wanaweza vipi kusema siyo? Wao wanaushahidi gani kuwa si mama yake?
Mtanzania,
Haya ya kubadili majina naona yameshamiri sana CCM. Mimi yule mbunge wa Bukoba aliyepewa uwaziri mdogo wa mambo ya ndani miaka yote nikimjua kama Suedi hata wakati alipokuwa UN Geneva. Mara ghafla vin boom akageuzi jina na kupata ubunge wa CCM na sasa ni waziri mdogo. Labda na mimi nitabadilisha jina nijiunge na CCM:-
1. Pingamizi la chadema lilikuwa na sehemu mbili. Kwanza, Oscar sio raia wa Tanzania na pili hana sifa za kugombea kwasababu hakuchaza fomu sawasawa.
2. Kwenye fomu yake kipengele cha tatu kinauliza ulizaliwa wapi yeye akajibu "Bukoba".
3. Kipengele cha nne kinauliza ni halmashauri/wilaya/mji/manispaa gani na yeye hakujaza kitu. Chadema wanadai "Bukoba" haitoshi kumtambulisha mtu amezaliwa wapi na vilevile unaporudisha fomu kila kipengele kinatakiwa kiwe kimejazwa tena kwa Herufi kubwa.
4. Oscar katika utetezi wake amewasilisha copy ya passport yake, copy ya birth certificate (ambayo tarakimu ya kwanza kwenye serial number haisomeki) pamoja barua ya mafao ya kustaafu kazi ya baba yake Biharamulo.
5. Aidha, kwenye barua yake ya utetezi amesema bado anafuatilia vielelezo viwili, barua kutoka uhamiaji (hakusema itakuwa na nini) pamoja na cheti cha ndoa cha wazazi wake.
6. Mkurugenzi amesema vielelezo vilivyo kwisha wasilishwa vinatosha kuthibitisha kwamba Oscar ni raia wa Tanzania.
7. Na kuhusu kujaza fomu sawasawa, Mkurugenzi pamoja na Oscar wamekiri kwamba fomu iliyobandikwa nje ya ofisi ilikuwa na makosa lakini fomu mbili ambazo mkurugenzi anazo zilikuwa zimejazwa kwamba anatoka mji wa bukoba. Hivyo kujazwa fomu moja kimakosa hakuwezi kumtengua Oscar kwenye kinyang'anyiro (ingawa hiyo fomu yenye makosa ndiyo ilikuwa available to the public for scrutiny).
8. Chadema wamekata rufaa leo mchana. Jaji makame na wenzake wanaingia Biharamulo kesho kuijadili rufaa ya chadema. Wana masaa 48 kuja na jibu.
Kuna watu walinotisi mara moja mabadiliko ya kutoka kutumia jina la "Mukasa" kwenda kwa "Rwegasira"... well
Na Frederick Katulanda, Mwanza (Mwananchi)
WAKATI kampezi za uchaguzi mdogo wa kiti cha ubunge katika Jimbo la Biharamulo Magharibi zikiwa zimeanza, mgombea wa CCM katika kinyanganyiro hicho, Oscar Rwegasira, amewekewa pingamizi kwa madai kuwa si raia wa Tanzania .
Habari kutoka Biharamulo na ambazo zimethibitishwa na Msimamizi wa uchaguzi wa jimbo hilo, Zuberi Mbyana, zilisema pingamizi hilo limewekwa na mgombea wa Chadema Dk. Anthony Mbassa.
Mgombea huyo wa CCM, aliteuliwa baada ya kuwashinda wapinzani wake katika kura za maoni kwa kupata kura 309.
Walioshindwa katika hatua hiyo ni na kura zao katika mabano ni, Agricola Magotto (120), Mwajemi Mustapha (23), Hassan Rwabudongo (15), Mussa Matata (10) na Nitibihora Burchard (5).
Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Mbyana alikiri kupokea pingamizi hilo na kwamba tayari ofisi yake imekwishamwandikia mgombea wa CCM, kumtaka kujibu pingamizi hilo.
Alisema katika pingamizi hilo, mgombea wa Chadema anadai kuwa mgombea wa CCM, hana sifa za kuwania nafasi hiyo kwa sababu si raia wa Tanzania.
Alisema kwa mujibu wa mweka pingamizi, mgombea wa CCM ni raia wa Uganda na kwamba wazazi wake wote wa wawili walitoka Uganda.
Msimamizi huyo alisema mgombea huyo wa Chadema anadai kuwa wazazi wa mgombea mwenzake, hawajawahi kuomba uraia hapa nchini.
Barua tuliyomwandikia mgombea wa CCM ni yenye kumbukumbu namba BBC/30/3/Vol. X/114 ya Juni 10, 2009 ambayo nimemtaka ajibu tuhuma za pingamizi alilowekewa na Chadema alisema msimamizi huyo.
Mkuu wa operesheni ya uchaguzi wa Chadema, John Mrema, alisema katika pingamizi hilo, Chadema wamebaini kuwa mgombea wa CCM, ameshindwa kueleza mahali alikozaliwa.
Baada ya kubaini hilo na kufuatilia uhamiaji na kwingineko, wamebaini kwamba wazazi wake mgombea huyo walingia nchini mwaka 1971 wakitokea Bunyoro nchini Uganda na kuishi eneo la Misenyi, alidai Mrema.
Alidai kuwa mgombea huyo wa CCM, alizaliwa Uganda mwaka 1970 na si katika kijiji cha Rukalagata Biharamulo kama anavyodai.
1. Passport yake ina jina la Oscar Rwegasira Mkasa na hata kwenye fomu ya tume amejaza majina yote matatu.
2. Suala la uraia wa Oscar ni jambo ambalo chadema wamekuta linazungumziwa kila kona ya biharamulo.
3. Katika kura za maoni za ccm, Oscar alisema na ilirekodiwa na kurushwa na Biharamulo Cable TV kwamba yeye amezaliwa wilaya ya Biharamulo. Kijiji alichosema amezaliwa wanakijiji wanakataa na kusema wazazi wake sio watu wa hapo bali ni wahamiaji, tena wa miaka ya karibuni (around late 1980s) wakati Oscar ameshazaliwa.
4. Oscar anaweza kuwa raia wa Tanzania lakini amelikoroga mwenyewe. Utata kwamba amezaliwa wapi ni yeye mwenyewe ameuanzisha kwa kutokuwa makini. Na jinsi alivyojaza fomu (at least iliyokuwa available to the public) kumeibua maswali mengi kuliko majibu.
5. Chadema wameshauriwa na mawakili pamoja na ccm "anti-oscar" wang'ang'anie issue ya kutojaza fomu sawasawa.
Wanavyodai wabishi wa Biharamulo ni kwamba alitaka ku prove hamna records uhamiaji inayosema aliingia tanzania kutoka uganda katika huo mwaka aliotajwa na chadema kwamba ndio aliohamia tanzania.
Mimi kwangu halina mantiki kwakuwa sidhani wahamiaji haramu wanapitiaga ofisi za uhamiaji. Lakini kama nilivyosema hapo awali Oscar anajilipua yeye mwenyewe na issue ya uraia kwa kutokuwa makini. Kwa mfano, kwenye uzinduzi wa kampeni (ingawa alikuwa haruhusiwa kufanya kampeni) mama yake inasemekana alikuwa mgonjwa alishindwa kufika, basi yeye alimyanyua mwanamke mwingine na kudai ndiyo mama yake mzazi wakati watu wanafahamu huyo sio mama yake mzazi. Ilileta miguno no minong'ono kwanini anadanganya wakati si lazima mama yake awepo pale? Watu wanajiuliza anaficha nini?
Hivi kweli kinachotutatiza ni Oscar kubadili jina la uzawa? Hivi haiwezekani ikawa ni mkakati wa kumfanya mgombea wake akubalike zaidi katika jimbo atakalogombea? Inasemekana Hillary Bowmann Clinton, kama feminist mkereketwa, alipoolewa hakutaka kuchukua jina la mume wake. Lakini mumewe alipotaka kugombea ugavana Arkansas aliambiwa kuwa watu wa jimbo hilo hawatamuelewa kama yeye akiwa mtu aliyeolewa, asipochukua jina la mume wake. Hillary kwa vile alitaka mumewe ashinde akabadili jina la ubini na kuchukua jina la mumewe and the rest kama wanavyosema wengine, is history. Mimi naamini kwa strategist yeyote anayetak mgombea wake akagombee huko vijijini atajitahidi kwa kila namna kumuunganisha huyo mgombea na sehemu hiyo. Kama itabidi kubadili jina liwe la kihaya zaidi, atafanya hivyo. Kama itabidi mgombea anywe lubisi, atafanya hivyo. Kama itabidi mgombea aanze kuongea kwa lahfudh ya kihaya atafanya hivyo. Yote hayo ni katika kutafuta ushindi. Au mnataka kutuambia kuwa angebakia na jina lake la wawali basi watu wasingemwekea pingamizi? Yote haya ni politics. Kwenye jina, naona kama inavyoanza kuwa kawaida yetu, tunageuza kichuguu kuwa mlima!
Amandla.......
Hillary Bowmann Clinton ndio nani huyo?
Touche, McCain. Kabla hajaitwa Rodham! Nitarekebisha. Nilisahau kwamba wamarekani mko wengi humu! Hasa Clintonites.
Amandla......
Wewe ni msukuma wa IMALASEKO? Jaga mtwe.Ndohomayo!!
Nimesikia mkubwa wangu ushauri wako, ngoja nijitahidi tahidi kubeba beba box na kukaangalia ka community college.