Jamaa ni msimuliaji mzuri sana wa visa/mkasa humu jukwaani. Ukiwa unasoma andiko lake pamoja na content anayozungumza lakini mpangilio pia huwa uko vizuri sana. Big Up Deep Pond
Usimfananishe DP na gmycn...wana aina mbili tofauti za kuhadithia ...gmycn anaweka kwenye mafumbo..na DP anafanya real life Drama( japokua wakati mwingine ni story tu)
Hili limekuwa tatizo kubwa sana hapa JF. Watu kutunga story na kuifanya kama ni tukio la kweli bila kuweka tahadhari kwa wasomaji. Na kuna wimbi kubwa la utunzi (fiction) wa kuomba ushauri kwenye mambo ya mahusiano au kimaisha na mikasa mbali mbali ambapo watunzi wanajifanya ni kama tukio la kweli. Hawajui tu lakini inaondoa mvuto wote wa kusoma. Mbona kuna watungaji wengi tu wa fiction na hueleza kabisa kuwa hii ni fiction na wana wasomaji wengi? Hata mimi napenda sana kusoma novel za fiction.