Biden atashinda, Trump is done

Hilo linawezekana lakini nalo litaleta changamoto litaondoa umuhimu wa majimbo ya kura chache watakuwa hawana umuhimu sana majimbo makubwa wataamuwa nani awe raisi na hilo wazee wao ndio waliliona. chukulia mfano jimbo kama la Maine sababu wako wachache kura 4 tu na hizo kura wanagawa hapo wanapoteza ushawishi sababu vyama haviwezi kutumia nguvu kutafuta kura moja ila kwa majimbo kama CA ndio wanaweza kutafuta hata 20. Mimi nadhani hakuna system perfect 100% ila na mapungufu yake hii ni best system kwa USA inawapa wadogo sauti. Senators ambao wanalinda katiba ya nchi na kumchunga Rais asifanye mambo kinyume na katiba huko wote uwakilishi sawa. Ndio maana hata Biden akishinda bado Rep wakishikilia Senators wana power kubwa tu. Kikubwa hakuna mkubwa wa kila kitu kuna check and balance kila mmoja anamchunga mwenzake asipitilize.
 
NY sio kubwa kwa size lakini wana 29 votes wakati Nevada ni kubwa kwa size lakini wana 6 wao ni population ndio inaamua.
Acha kubadili badili magoli ili kuendeleza ubishi! Ulichokuwa umesema ni kwamba hata ushinde kwenye majimbo makubwa HAWAKUPI USHINDI kwa sababu kumewekwa mfumo wa makusudi kuhakikisha majimbo madogo na yenyewe yanakuwa na sauti:-

Ni kutokana na kauli yako hiyo ndipo nikakuambia hakuna cha mfumo maalumu wa kuwapa sauti wadogo wala nini bali it's all about anumber of electoral colleges ambayo allocation yake is based on size and POPULATION!! Hiko ndicho nimesema ingawaje suala la population nililotaja unaliacha kwa makusudi na kujikita kwenye size huku ukisahau wewe mwenyewe hukuzungumzia popote kuhusu population!!
Sasa kwa mfano uliotoa Tanzania kwa kuwa mfumo wetu ni kura nyingi sawa unachosema unaweza kupata kura mikoa yenye watu wengi tu Mwanza na Dar ukashinda ila sio ukubwa wa size
Again, kwa makusudi unazungumzia suala la size!! Hivi kuitaja Dar es salaam na Kanda ya Ziwa unaamini kabisa nililenga kuzungumzia size badala ya population? Btw, ukitoa Lindi yenye geographical challenge kutokana na eneo kubwa kuwa covered na Selous, hivi unaweza kupuuza proportionality ya land size to population?
Tungekuwa na mfumo kama wa USA ndio Dar na Mwanza zingekuwa muhimu kushinda ila kuna mikoa midogo ingekuwa na sauti kubwa kutuamulia kiongozi kama leo hii Nevada wenye 6 points wanawahukumu wenye 55 points.
Narudia tena na tena, Nevada wanaonekana kuhukumu kwa sababu tu PA, NC zina uwezekano mkubwa wa kwenda Republican wakati Democrats wanahitaji ushindi wa jimbo lolote kati ya yale yaliyobaki including hiyo NV!

Hivi sasa Pennsylvania na Georgia hakuna mgombea ambae ameshafikisha angalau 50% huku GA both Biden na Trump wakiwa na % sawa huku PA Trump akiongoza!!

Ikitokea GA au PA wamemchagua Biden, hakuna tena atakayemsubiria Nevada kufanya maamuzi kwa sababu Electoral Colleges zake ni chache mno kuweza kupindua meza!!!
Sasa suala la swing states limeingiaje kwenye issues za majimbo madogo?! Ni matumaini yangu hufikirii kuchanganya madesa kwa kudhani swing states ni yale majimbo madogo!!
 
New york times wanaheshimika??,Na nani? That far left propaganda machine is no more a credible news to rely on,just like CNN hakuna tofauti sana.Sasa leo ukisema cnn hii ya sasa eti inasheshimika lazima useme inaheshimika na nani,only liberals..
Hata foxnews Ni Republican watupu [emoji2][emoji2]

Sent from my TECNO P703 using JamiiForums mobile app
 
Ukisoma comment zangu za awali nimesema hizi votes wamepeena kwa wingi wa watu lakini pamoja na yote hawa wenye kura chache sababu ya wingi wa watu siku zote wanaonekana wana sauti ndio maana utakuta wakati mwingine wanapiga kampeni sana katika majimbo ambayo yanaonekana ni madogo ila hesabu zao zinakuwa wakipata hata vote 10 watashinda. Kwangu mimi naona ni system nzuri sana tu ila hivi sasa Georgia Biden kisha chukua uongozi na kura almost 99% zimehesabiwa kwa hiyo anachukuwa bila Nevada kiurahisi. Mimi na wewe hatutofautiani kabisa unachosema ni sawa ila kama tutaanzisha mjadala je system kama hii ingetufaa sisi huku na faida zake ni zipi na hasara zake ni zipi.
 
Fikiria jimbo kama Texas, kura nyingi za democrat zinatoka kwenye majiji yao matatu (Houston, Dallas na Austin). Majiji haya ndiyo yenye watu wengi weusi. Kama kungekuwa utaratibu wa kugawana kura basi na wao wangepata nafasi yakuchangia, kuongeza electoral vote kwa mgombea waliyemchagua. Lakini kwa mfumo wa sasa hill billies ndiyo wanatamba.
 
Fox news wamepewa maagizo wasimuite Biden president elect pale atakapokuwa kafikisha 270. Trump anatia huruma na hao vibaraka wake Fox
 
Hebu ongeza sauti mh. Mjumbe.
 
Fox news wamepewa maagizo wasimuite Biden president elect pale atakapokuwa kafikisha 270. Trump anatia huruma na hao vibaraka wake Fox
Mpk wigi litamdondoka leo.
 
Kwa sasa wako
253-214

Hii ngoma Trump atawin
Ana win aje mzee au unaota? Trump ili ashinde anahtaji kushinda majimbo yote yaliobaki kitu ambacho ni ndoto katika majimbo hayo karibu manne Biden anaongoza japomkwa margin ndogo na kura zilizobak kuhesabiwa ni kati ya 5% to 1% tu
 
Utabiri unaelekea kufanikiwa.
 
Ana win aje mzee au unaota? Trump ili ashinde anahtaji kushinda majimbo yote yaliobaki kitu ambacho ni ndoto katika majimbo hayo karibu manne Biden anaongoza japomkwa margin ndogo na kura zilizobak kuhesabiwa ni kati ya 5% to 1% tu
Kura zinarudiwa kuhesabiwa baadhi ya majimbo... Jioni hii wanaanza kurudia kuhesabu Georgia..
 
Watu wanahesabu kura camera ziko live kuwarekodi. Tanzania sijui tutafikia lini level hiyo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…