Nimesema mara kadhaa hapa kwamba suala la COVID-19 ndio moja ya sababu kuu ya kushindwa Trump, watu hawaelewi.
Mimi nadhani ni character.
C-19 ni kama imekuja tu kuongeza ladha mwishoni mwishoni hapa.
Kwa sababu, kama sababu kuu ingekuwa ni C-19, basi ungeona huo ushindi umepenyeza hadi kwenye bunge [Reps na Senate], State legislatures, na kwenye ugavana wa majimbo.
Hilo halijatokea.
Matter of fact, GOP wameongeza viti kwenye House of Representatives. More than likely the house will be split 50-50 or thereabouts. Hivyo, siku za Nancy Pelosi kuwa spika zinahesabika.
Kwenye senate more than likely GOP wata maintain majority, albeit a slim one. But a majority nonetheless.
Kwenye state legislatures, GOP wameweza ku flip state legislatures 3, na hivyo kuongeza idadi ya majority ya legislatures zinazoongozwa na GOP.
Na hilo suala ni muhimu sana kwa redistricting ambayo yaweza ku determine house majority for the foreseeable future.
Kwenye ugavana pia, GOP wana viti vingi kuliko Dems. Asilimia 52 hivi, kama sijakosea.
Hivyo, hakukuwa na blue wave kama ambavyo polls zilikuwa zinadai.
Kilichokuwepo ni rejection tu ya Donald Trump, hususan kutokana na tabia yake.
Kama ingekuwa ni rejection ya GOP policies, ni lazima ingekuwa reflected kwenye nafasi zingine.
Mfano, ni majuzi tu hapa senate GOP wamem confirm Justice Amy Coney Barret kwenda kwenye Supreme Court. Lakini hilo halijawa cost kwenye sanduku la kura.
Na kuna GOP wengi saana ambao hawakumpigia kura Trump, bali walipiga kura dhidi yake kwa kumpigia kura Biden.
Hilo kundi halitokuwepo tena 2024. Litarudi nyumbani.
The 2020 US election was a referendum on Donald Trump mainly because of his character.