Biblia kwa Jicho Jingine

Awali ya yote Nikupongeze kwa Uandishi Ulio pangilika,

Je wewe Ni bilionea Asigwa wa Fb?

Tatu na mwisho, je nje ya Jamii forum unaweza kukaribisha maswali na hoja juu ya MUNGU?!

Imeandikwa
"Itafuteni KWELI nayo KWELI itawaweka HURU"
 
umenisisimua mahali
ndiyo maana nikawa nashangaa Y? ukitaja jina la YESU mapepo na mambo mabovu yanakimbia/kuweweseka?
lakini nikawa najiuliza Y? ukitaja jina la Mtume (Saw) yaani hata mapepo haya ropoki
asee hapo NIMEPATA kitu
Em taja wewe hilo jina la YESU kama hayo mapepo yatakurupuka, think big ...
 
popote pale unapotaja jina la YESU haijalishi
unataja kwa kilugha au kwa kibongo
but mapepo yana Hali ya utambuzi
na jina la YESU NI fireee kweli kweli.
so mapepo yatatambua kuwa umemgusia YESU mwana wa MUNGU
kuna tofauti kubwa Kati ya YESU mwana wa Mungu na issa bint Maryam
dats Y? kwa waislamu hata ukisema kwa jina la issa bint Maryam Pepo hazitapata tabu sanaaa
but washa moto kwa kibwagizo cha jina la YESU KRISTO mwana wa Mungu aseee.
Ni sawa na kusema kwa damu ya YESU na kwa damu Ya issa
All in all Jina la YESU litaendelea kuwa Kubwa kuliko hata jina la Mtume (SAW)
Em taja wewe hilo jina uone kama mapepo yatakurupuka. Huoni kama there is somthing behind...., na kwa nini Mungu achague watu wa kuamsha mapepo kwa jina hilo..? Kwa nn isiwe kwa yeyote tu akitaja itokee...? Utasema labda viwango vya imani ok kwan wao wanamini nini, na wengine wanamini nini ...., maswali ni mengi sana ......
 

MKUU lipo jina linalofanya nijibu hivyo
tangu nizaliwe mpaka nakuwa hivi
SIJAWAHI SIKIA JINA LA MTU LIKIPONYA/KUTOA PEPO/KUOGOPEKA
ZAIDI YA JINA MOJA TU......
nadhani unalifahamu siyo ngeni kwako bali ni jina la YESU KRISTO MWANA WA MUNGU
hata ukileta battle Kati ya
jina la YESU vs Mtume (SAW)
la mtume lazima litakaaa
hivi hujawah jiuliza Y? jina la YESU ni fireee compare to Mtume(SAW)????
Najivunia kuwa na jina la YESU lenye NGUVU...
Em taja wewe kama utaponya mtu hata mmoja au hata mtu kutikisika tu ..., lingekuwa linanguvu basi ingelikuwa ni kwa yeyote atakayelitaja mambo yatokee, but utakuta ni kwa hao wainjilist na wachungaji wa kileo ndo wana hizo mbwembwe, kwa nini mapadre na wasabato hawalitumii kuponya ...? Think big ...
 
Unachokisema ni kweli kabisa mkuu.

Hata Malaika wanayeishi na Mungu huko juu hawamuelewi huyu Mungu ni nani.
Katika kozi ambazo haziishi mbinguni ni kozi inayoitwa "Kumuelewa Mungu".

Hii ni kozi inayosomwa milele na milele na milele yote na kila kiumbe alichokiumba Mungu, si Malaika wala si wanadamu wala si kiumbe chochote cha kiroo kinaweza ku-graduate katika kozi hii.

Huko mbele nitaelezea concept moja makini sana ambayo kwa kifupi ni kuwa Mungu hujifunua kwa kila kiumbe chake kwa Level ya kiroho waliyo nao hao viumbe wake kwa kuwa yeye ni mkuu mno huwezi kumuelewa akija kama alivyo.

Na ni kweli kuwa Mungu ana mfumo wa utawala kama ulioko huku duniani, lakini yuko accessible kwa kila kiumbe chake, hakuna protocol ngumu ya kumuona kama ilivyo huku duniani, ila angalizo ni moja tu kuwa Mungu huyo unayemuona wewe si Mungu yule anayemuona Serafi au Kerubi, ndio maana wenye uhai wanne wale husihi tu kuimba mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu milele yote.

Si kwa sababu wanapenda kumsifu sana ila ni kwa sababu Kila siku wanamuona katika version mpya ambayo walikuwa hawajawahi kuiona, na katika hili kazi yao kuu ni kuitaja sifa kuu waiyoiona kwa wakati huo.
Na kwa kuwa daima anapanda katika viwango kwao kulingana na ufahamu wao, wao huishia tu kusema Mtakatifu Mtakatifu Mtakatifu maana hata wao wanashindwa kumuelewa.

Kwa hiyo ukienda Mbinguni leo ukataka kuonana na Mungu utapelekwa moja kwa moja na utakaa karibu naye kabisa, ila perception yako kwake italingana na uwezo wako wa ku conceive mambo ya Kiroho kwani wakati unadhani unamfahamu kumbe hata bado hujaanza kumfahamu.
Dahh, mkuu uko deep sana, hizi ni nyuzi nazozifatiliaga kwa undani, km hutojali nitakuchek kwa maarifa zaid.

Ubarikiwe sana.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Nimeamua kuandika makala hii kwa heshima ya Jukwaa hili lakini pia kwa ajili ya kuchochea udadisi lengo likiwa kumpa kila asomaye uthubutu wa kutaka kufukiri nje ya Box.

Makala hii ni mjumuisho wa vitabu vingi vya kiroho kikubwa kikiwa Biblia, Simulizi za Kiyahudi, Vitabu vya Mafunuo ambavyo baadhi ya walioishi duniani walibahatika kuyapata kutoka wa Mungu mwenyewe lakini pia baadhi ya mawazo yangu ili kuweka mtoririko mzuri wa kimakala.

Makala hii huenda ikapingana na unachokiamini, lakini chanzo cha fikra mpya hujengwa katika tofauti ya kimitazamo, na hapo ndipo mwanadamu hukua kimawazo, kwa hiyo ukiona yaliyomo humu yanapingana na uelewa wako ni vema uachukulia tu kama masimulizi ya hadithi za kufikirika, maana lengo la uzi huu si kuchafua au kuvuruga imani ya mtu yeyote.



Hapo mwanzo Mungu aliziumba Mbingu na nchi nayo nchi ilikuwa giza tena utupu.

SEHEMU YA KWANZA(UTANGULIZI)
Hapo zamani sana kabla ya mwanzo wa kila kitu alikuwepo Mungu pekee bila kiumbe chochote kile kilicho hai wala kilicho mfu, Mungu huyu kwa utashi wake kabisa na kwa mapenzi yake kabisa bila kushurutishwa na yeyote akaamua kujipanua kwa “kuuwekeza utu(uhai) wake” ndani ya vitu vingine ili tu kutimiza yale ambaye yeye aliyaona yanaifurahisha nafsi yake.
Mungu huyu aliamua kujigawa katika vipande vikubwa vitatu ambavyo vyote vilibeba Uungu wake kwa ukamilifu wa 100%, vipande ambavyo vingemuwezesha yeye kwanza kutekeleza tukio zito lililokuwa mbele yake, lakini pili kurahisisha kile ambacho anataka kwenda kukifanya kwa kuwa kwa vyovyote vile kwa hulka yake alitaka kuugawa uhai wake(kuusambaza) kwa viumbe vyake atakavyoviumba lakini pia kuwa navyo karibu kama familia moja.

Viumbe hivi kwa vyovyote vile visingeweza kumuelewa na wala haviwezi kumuelewa milele yeye ni nani, kifupi vinaelewa kile tu ambacho ameruhusu kieleweke kwao kwa wakati huo, pamoja na hilo bado hivyo alivyoviruhusu vieleweke vimekuwa “hekima nzito kweli kweli” , hekima ambayo imeviharibu viumbe hivyo vilivyoamua kuitumia vibaya uelewa mdogo waliopewa kuibeba si wa malaika wala wanadamu wala kwa viumbe vyote vya rohoni alivyoamua kuviumba.
Kwa msingi huu Mungu huyu akaamua kufanya kazi katika nafsi tatu, ya kwanza akaiita Mungu Baba(Mungu Mwenyezi), ya pili akaiita Neno(baadaye alivaa mwili ili aje duniani kama mwanadamu) na ya tatu Roho baadaye alikuja kufahamika kama Roho Mtakatifu huku duniani.

Kimsingi nafsi hizi tatu zina nguvu kubwa sana na imekuwa vigumu sana kwa viumbe vyote vya rohoni na vya mwilini kujua hasa tofauti yao ni ipi na nani ni nani , lakini majukumu yao yamegawanyika kiutendaji zaidi, huku nafsi hizi tatu zikibaki kubeba Uungu wao kwa 100%.
Kifupi unayedhani ni Mungu Baba saa nyingine unakuta siye yeye ila ni Neno, na unayedhani ni Neno sometimes siye yeye ila Roho na unayedhani ni Roho saa nyingine siye ila ni Mungu Mwenyezi mwenyewe kwa kuwa kila mmoja ni tofauti na mwenzake na wakati huo kila mmoja yumo ndani ya mwezake, wote hawa ni nafsi tatu tofauti kabisa zinazojitegemea lakini pia nafsi hizi tatu ni moja.
Mungu Mwenyezi huyu yeye akaamua kuchukua jukumu kama la msimamizi mkuu na Master Planner wa kila kitu kinachoendelea huko kwenye mbingu za juu sana, mbingu tunazozijua sisi na hapa duniani, ni kama Senior Planner na administrator wa kila kitu.
Yeye ndiye mpangaji au designer, muandaa maono na senior Founder.

Neno yeye akachukua jukumu la kutekeleza maono yote yanayotoka kwa Mungu Mweyezi, yeye ndiye hasa fundi wa kutafsiri maono na mipango kutoka kwa kwa Mungu Mwenyezi na kuuingiza katika utekelezaji ili vyote vilivyopangwa kugeuka kuwa vitu tangible, lakini pia kunapotokea failure kama iliyotokea kwa Adam na mkewe bustanini Edeni, failure ambayo inatokana na design nzuri kabisa ya kukipa kila kiumbe chake uhuru wa kuishi maisha ya kuwa na utashi akichagua anachotaka na asichotaka bila kushurutishwa na yeyote basi Neno huja na kurekebisha kasoro hio kwa kufuata design kutoka kwa Mungu Mwenyezi.
Kifupi Neno huyu ndiye mwenye jukumu la kurekebisha kasoro hio na ndio maana maandiko yanasema “alichinjwa kabla ya kuwekwa misingi ya nchi kwa kosa la Adam na mkewe Hawa”

Roho yeye akabeba jukumu la uwezeshaji, yeye ndiye supplier wa nguvu na uwezo na materials za kiroho kuhakikisha kuwa plan zote kutoka kwa Mungu Mwenyezi, na utekelezaji wake kutoka kwa Neno unafanya kazi kama ilivyopangwa.
Yeye ndiye mwenye jukumu hasa la kuhakikisha kila kitu kinakuwa maintained katika viwango vyake kama ambavyo Master Plan inavyosema, lakini yeye pia ndiye msimamizi mkuu wa Uungu katika viumbe vyote vilivyoumbwa na vitakavyoumbwa.
Kabla ya Neno kuja kuanza kazi yake, Roho huyu hutangulia kwanza na kuyaaandaa mazingira, na mara baada ya Neno kumaliza kazi zake kama mtekelezaji, Roho hukabidhiwa jukumu pia la kuiendeleza kazi iliyofanywa na Neno lakini pia kuhakikisha kuwa quality na standards zake zinafikia Master Plan kama ilivyopangwa na Mungu Mwenyezi.

Kumbuka hawa watatu ni wamoja na ni tofauti pia, wakati unadhani sasa yuko Neno anafanya kazi, kumbe siye ila ni Roho na wakati unadhani ni Roho anafanya kazi unakuta ni Mwenyezi mwenyewe na wakati unadhani ni Mwenyezi yuko kazini kumbe ni Roho au ni Neno yuko kazini.
Biblia inasema Mungu[Jehova] kwa Neno lake[Neno] aliziumba mbingu na nchi na kwa Hekima yake[Roho] akazithibitisha(zikawa maintained).

Kazi ya uumbaji ilipoanza, Mungu Baba akaandaa Master Plan master, Plan hii ikaanza utekelezaji wake awamu kwa awamu kwa kadri alivyoona yeye kuwa inafaa kwa nyakati atakazoziweka yeye na kwa namna atakavyoamua yeye.

Umbaji huu uligawanyika katika vipande viwili (Spheres Mbili).
Uumbaji wa kwanza ulikuwa uumbaji wa viumbe vya Kiroho na uumbaji wa Pili ulikuwa uumbaji wa viumbe vya kimwili, pia Mungu akaamua kuweka baadhi ya viumbe vya kiroho na kimwili kusimamia kazi zake za uumbaji, kusimamia mifumo yake ya Kiuungu, kusimamia tabia na makuzi ya viumbe vya kiroho lakini pia akatoa wasaidizi chini ya kila aliyepewa jukumu la kusimamia.

Sphere za Kiroho
Katika uumbaji wa Sphere za Kiroho kuna spheres ndogo ndogo nyingi sana huenda zikawa mabilioni kwa sasa kwa uwa kazi ya uumbaji inaendelea na ni ya milele na milele.
Spheres hizi zina vipande vitatu,
• Kipande cha ndani kabisa
• Kipande cha katikati
• Kipande cha Nje
Kipande cha ndani kabisa ambacho wengi tunakifahamu kama Mbingu ya Mwenyezi Mungu, Mbingu hii ndipo mahali ambapo kiti cha enzi cha Mungu kipo na ndio hasa headquarter ya uumbaji wote maana ndiko ambako Mungu yupo.
Muundo wa kipande hiki au Mbingu hii umegawanyika pia katika sehemu kuu tatu.
1)Ya Kwanza ni sehemu ya Uungu inayoanza kwa Kiti cha Enzi cha Mungu kilicho upande wa Kaskazini wa Mbingu, kiti hiki kiko juu ya kila kitu kwa maana ya height na hakuna kitu kinachoruhusiwa kukaa nyuma yake, kiti hiki kimezungukwa na viumbe vinne vyenye uhai ambavyo vimejaa hekima na ukuu na utiisho wa ajabu kwa sababu ya kuwa karibu na Mungu muda wote na viumbe hivi vina act kama waangalizi wa kiti hiki lakini pia Uungu wa Mungu.

Mara baada ya kiti hiki cha Enzi kuna Sehemu ya Roho ambazo zinasimamia tabia kuu za Mungu ambazo ni 1)amani , 2) upendo, 3)utukufu mkuu, 4)nguvu , 5)uzima , 6 )hekima , 7) rehema.
Baada ya hapo kuna uwazi mkubwa sana kama bahari ya kioo na mbele yake kuna wazee 24 ambao nao wako katika sehemu ya Uungu wa Mungu, hawa ni kama “baraza” la Umungu, kumi na wawili wakiwa mkono wa kuume wa Mungu na Kumi na wawili wakiwa mkono wa Kushoto wa Mungu.

2)Sehemu ya Pili ni sehemu ya ibada ya Uungu ambapo kuna madhabahu ya dhahabu ya kutoa uvumba, madhabahu hii iko pembei kidogo mara baada ya kutoka kwenye viti vya wazee 24.
Hapa ndipo ambapo sala zote na dua zote na shukrani zote za wanadamu na viumbe vyote aivyoviumba Mungu hupelekwa na kufukizwa kama harufu ya manukato kwa Mungu, harufu hii kupelekwa moja kwa moja kwa Mungu mwenyewe kwenye kiti che enzi bila kiumbe yeyote kugusa maana hii ni haki ya Mungu pekee.

Katika sehemu hii ya pili pia mbele ya kiti cha enzi husimama malaika wakuu 7 wa Mungu ambao huutazama uso wa Mungu daima wakipokea amri za kutekeleza kulingana na jukumu la kila mmoja alilopangiwa, majukumu haya yanahusisha control ya galaxies zote ambazo zinakadiriwa kuwa zaidi ya Bilions, usimamizi wa Mifumo ya Uungu na utawala na majukumu mengineo kulingana na nyakati na ratiba ya Mungu.
Sehemu hii ya pili pia ni sehemu ya kila kiumbe ambacho kinataka kuwa na audience na Mungu awe ni malaika au viumbe vya rohoni au Adam enzi hajaanguka au yeyote anayetaka kujihudhurisha mbele za Mungu hapa anaruhusiwa kusimama na kuonana na Mungu moja kwa moja bila urasimu wowote.

3)Sehemu ya tatu ni sehemu kama ”mji” au city center ambapo kuna shuguli mbali mbali zinaendelea za kiofisi lakini pia za kimakazi kwa baadhi ya viumbe ambavyo vimepata nafasi ya kuishi mbinguni moja kwa moja kulingana na level yao ya ukuaji wa kiroho.
Hii ni sehemu iliyo busy sana na iliyo na “kelele nyingi” kila “mtu” akiwa na lake, ikiwa ni sehemu ya kuingia na kutoa na pilika pilika za kutosha kila mmoja akifanya lililompeleka makao makuu.
Kuna idara nyingi sana katika eneo hili ikwemo idara ya sifa, idara ya uumbaji, idara ya vita, idara inayohusika na wanadamu, idara za hukumu na mipangilio mingine mingi.

Kama nilivyosema kuna makazi huko mbinguni ya viumbe alivyoviumba Mungu, haya si makazi ambayo Yesu aliyaahidi kwa wafuasi wake, na ni wenye Uungu tu waio na makazi mbinguni lakini kila kiumbe kingine kina makazi yake, Mungu tu ndiye anayeishi na kukaa kwenye kiti chake cha enzi.
Hili Nitalielezea kwa mapana nikifika kwenye kipengele cha malaika na maisha ya malaika.

Katika spheres za kiroho kitu kinachitukuzwa sana ni Nuru au mwangaza wa utukufu, kwa maana kuwa ukuu wa kitu unaakisiwa na kiwango cha Nuru uliyo nayo, kuna viumbe vina nuru kubwa sana vingine vinayo ndogo, ukuu wa nuru unategemeana na ukaribu wako na Mungu lakini pia dimension ya ukomavu wako wa kiroho na viwango vyako vya rohoni.

Mara baada ya kipande cha Ndani kuna kipande cha kati kati ambacho ni kipande kilichotengwa maalumu kwa ajili ya makuzi ya kiroho, makuzi haya hutegemea na kusudi ambalo Mungu amemuumba kiumbe wake, wapo walioumbwa kuwa wakuu wa usimizi wa vitengo mbali mbali, wapo walioumbwa kuwa wakuu wasaidizi, wapo walioumbwa kuwa “raia wa kawaida” na kadhalika.
Sphere hizi za kati kazi ni nyingi sana na hupokea viumbe vinavyokuwa na kukuwa kiroho kila siku, makuzi ya kiroho hayadhihiriki katika umri ila katika kiwango cha nuru uliyo nayo katika ulimwengu wa roho.

Nje kabisa ya spheres hizi za kiroho kuna sphere yenye maisha ya kawaida ya viumbe vya Mungu ambavyo aliviumba, hapa ndipo mwanzo wa kila kitu alichokiumba, hapa ndipo akila kilichoumbwa kwa dimension yake kinakaa, wanadamu kwa dimension yao na spheres zao, malaika kwa dimension yao na spheres zao, viumbe vingine pia vya rohoni vina dimension yao na spheres zao vile vile na kila kimoja kikiwa kinaishi bila kukiingilia kingine wala kukibugudhi kingine kwa mipaka aliyioweka Mungu kwa hekima yake.

Katika sphere hizi ikitokea mfano malaika akataka kuingia katika sphere ya wanadamu itambidi ajibadilishe awe kama wao kwa kuvaa umbo lao vinginevyo hataonekana nao. Vile vile ikitokea mwanadamu akataka kuingia kwenye dimension ya malaika inabidi avue mwili avae roho vinginevyo malaika hawana uwezo wa kui nterract nao na kuna portal maalumu za kuingilia si kuvamia vamia tu.
Ikitokea umechakachua na ukaingia kwenye sphere isiyokuhusu kwako ni kosa na unatakiwa kuhukumiwa, na hiki ndicho kisa hasa cha wale malaika 200 waliovaa miili wakaja kuishi na wanadmu wakasababisha dunia kuchafuka kwa maasi yaliyopelekea gharika.

Spheres za Kimwili
Mara baada ya spheres za kiroho kuna spehere za kimwili ambazo nazo zimegawanyika katika vipengele saba, vyote hivi ni kwa ajili ya makuzi ya kiroho na kimwili ya viumbe vya mwilini.
Adamu alipopewa kuishi kwenye Bustani ya Edeni alipewa jukumu la yeye na viumbe vyake alivyokabidhiwa kukua katika sphere hizi zote saba akianzia katika sphere ya kwanza kabisa ambayo tunaiita bustani ya Edeni, bahati mbaya sana jamaa akajichanganya mapema kabisa.

Mara baada ya anguko la Lucifer iliundwa sphere nyingine inayojulikana kama sphere ya tatu au sphere ya giza au war sphere , ilichukua kama theluthi moja ya spheres zote za uumbaji wa Mungu kwa wakati huo.
Sphere hii ya giza kwa makosa ya Adam ikajitanua mpaka kwenye dunia yetu hii na kupelekea mwanadamu kuwa kiumbe mwenye Umungu na Ushetani ndani yake.

Nuru na giza vikawa ndani yake matokeao yake maisha yake yakawa ni mapambano na mahangaiko ya wema na ubaya vikiishi kwa pamoja ndani ya mtu mmoja kila kimoja kikishindaba kuvutia upande wake.
Juu ya dunia tunayoishi kwa sasa kuna sphere za nuru nne ambazo wengi wa wanadamu wanaokaribia kufa huziona na huona kama vile wanapita katika tunnel ya mwanga au njia Fulani ndefu sana ya mwanga tupu na kuelekea huko kwenye spheres za juu.
Wengi waliopata nafasi ya kufika kwenye sphere hizo za juu ya dunia walidhani wameishaingia mbinguni, na mara nyingi spheres hizo za nuru za juu ya dunia huwa zina ufanano na dunia hii isipokuwa zinakuwa ziko perfect sana na hazijachakachuka na giza kama tulilonalo huku, wengi wanaoingia hapo hupaita paradiso, lakini kimsingi hata paradiso yenyewe bado.

Chini pia ya dunia kuna spheres mbili za giza moja ikiwa ni giza tupu lililosheheni ushetani wa hali ya juu ambapo waovu wa dunia hii huenda kuchukua nguvu za giza kuja kuiharibu dunia, ni shemeu ambapo mapepo mengi sana yanapatikana na roho za wandamu waliokufa katika giza hugeuzwa kuwa maajenti wa kuzimu kuja kuvuruga maisha huku duniani, na hapa ndipo kuna kitu kinaziliwa kinaitwa majeshi ya wafu, vibwengo, vinyamkera , aliens na mengineyo.

Chini kabisa kuna sphere moja iliyo na giza kuu ambalo ndipo Lucifer mwenyewe yupo anaishi, huko ndiko kuzimu hasa ambapo ni makao makuu ya uovu wote kukisheheni hekima yote ya kishetani na viwanda vikubwa vya uharibifu na ubunifu wa kila namna lengo likiwa ni moja tu kumkomoa Mungu na viumbe vyake.
Nitaizungumzia Kuzimu kwa mapana yake baadaye mara baada ya kuwachambua malaika na maisha yao kwa upana wake.
Kabla ya hapo tuyazungumzie maisha ya ulimwengu wa kiroho kabla ya kuumbwa kwa dunia yetu, maisha yanayojumusiha pia uasi na anguko la Lucifer.

Sehemu ya Pili itafuata soon…..

Mkuu

Lete muendelezo tafadhali

Maana toka uhaidi mpaka mwaka umeisha Bado,tuko 2022 Bado hujashusha muendelezo.

Tumesubiri Sana timiza ahadi

Tupe muendelezo wa sehemu ya 3,4,5....
 
Back
Top Bottom