ARV
JF-Expert Member
- Sep 6, 2011
- 5,554
- 7,993
Bibi kizee mmoja alikuwa anasafiri kwenye basi usiku na siti ya nyuma yake alikaa kijana mmoja. Wakati safari inaendelea akawa anainama chini ya siti yake anachukua kopo la castle na kulipeleka mdomoni(kama anakunywa kitu) sasa yule kijana wa nyuma yake akawa anashangaa huyo bibi anavyofaidi maisha kwa kunywa castle toka safari inaanza, akatamani amuibie angalao apige pafu moja halafu arudisha haraka lile kopo kabla bibi hajashtuka,Basi akamtaimu bibi wakati analitoa mdomoni na kuliweka chini kwa haraka akapitisha mkono chini ya seat akachukua lile kopo akanywa funda moja kuuubwa, baada ya hapo tukasikia mtu anapiga makelele na kutema mate kama mtu anayetaka kutapika, Kumbe yule bibi alikuwa anaumwa Kifua kikuu na alichukua kopo lile la castle kwa ajili ya kutemea makohozi...