Bibi Cheka atoboa siri ya mafanikio yake

Michael Amon

JF-Expert Member
Dec 22, 2008
8,775
3,610
0001hiphop.jpg

KIKONGWE machachari kwenye tasnia ya muziki wa Bongo fleva Bibi Cheka, amesema hakukata tamaa tangu akiwa kijana, alijipa moyo kuwa siku moja kila mtu atamjua kutokana na juhudi zake binafsi.

Cheka alisema hakuna kitu anachochukia kama kusikia mtu akisema 'siwezi.' Alisema kila anapomsikia mtu akisema hivyo, humchukia maisha yake yote hasa akiwa mwanamke.

Bibi Cheka kwa sasa anatamba na wimbo wa 'Ni wewe'ambao ameimba na Mheshimiwa Temba wa Kundi la Wanaume Family chini ya Saidi Fella na yeye akiwa mmoja wa wanamuziki wa kundi hilo.

Cheka alisema kilichomfanya ajiingize kwenye kundi la Wanaume Family ni ndoto zake za siku nyingi kuwa mtu maarufu ambaye amefikia hapo kwa juhudi zake.

"Sikukata tamaa na siku zote nilitamani kila mmoja anijue na kutambua kazi yangu nikiwa mwanamke na kupitia Wanaume Family hilo limewezekana hadi wewe umekuja kuniuliza,kabla ya hapa tungeonana wapi?"Alihoji.

Bi Cheka alimalizia kwa kuwataka wanawake wenzake wamuunge mkono badala ya kumbeza na kumuona ni muhuni kwani kazi ni kazi ili mradi ni ya halali na mkono unakwenda kinywani.

"Kazi hii ya kuimba imenifanya nisiwe mzigo kwa familia kwani natatua shida zangu ndogondogo,"alisema bila kutaja alipata kiasi gani cha fedha kutokana na wimbo huo.

E-mail: meezy@youngmaster.co.tz
 
Inabid wasanii maunderground muwe wavumilivu kama bibicheka,kahustle toka utoton mwake(enzi za kina remy ongala) hatimaye katoka,sahv anakula mafao ya uzeen na wakina Temba tembele mmwee!
 
Dah! Lakini ana moyo kweli. Mimi nampongeza kweli kwa uvumilivu aliokuwa nao. Inabidi na sisi vijana tuige mfano wake.
 
Ame hustle sana..lakini to bad hato kaa kwa muda mrefu katika game..si tu kwaajili ya umri bali aafya pia..nakumbuka Media Day Bonanza alianguka baada ya kuona umati wa watu wakitaka kupiga nae picha .akawa overwhelmed ..alivoshuka jukwaani tu..chaliii..preshaa juu..kuna haja ya mazoezi on top of that hajui umri wake..hua ana guess tu!!
 
Mambo yaki-kataa yamekataa!!, huku ni kujiumiza, Umri haukubali, huyu hana wajukuu ama watukuu?, hawaoni anavyo hangaikaaaa!!!!!! Khaaaa!!!
 
Lakini kweli mkuu.
 
Mambo yaki-kataa yamekataa!!, huku ni kujiumiza, Umri haukubali, huyu hana wajukuu ama watukuu?, hawaoni anavyo hangaikaaaa!!!!!! Khaaaa!!!

ana wajukuu na vitukuu ndo ivo na mapanga ya wanaume anataka kuyakata..sasa hao akina said fella wanavomvalisha majinsi ya buku 7 na makoti mchana wa saa saba..na zile raba za watu wa Arusha..wanaziita "teremka tuongee" basi ana jistukiaaa akiona mnamtazama anajifunika kanga usoni..mana akipanda jukwaani watu wanaangua vicheko..hana tofauti na bambo wa ze comedy..mi nilivomuona na nlikua bwiii..nilichekaa kwa sauti mbaka nikaanguka kwenye kiti akantazama akajifunika kanga..ha ha ha nna tabia mbaya!!
 
huo ndo umbea wenyewe,lol
 
Ha ha haaaa!! Aisee ningekuwa hapo ningekutandika viboko sita hadi nane vya nguvu kwa kumcheka bibi wa watu.
 
Inabid wasanii maunderground muwe wavumilivu kama bibicheka,kahustle toka utoton mwake(enzi za kina remy ongala) hatimaye katoka,sahv anakula mafao ya uzeen na wakina Temba tembele mmwee!

hahaha alianza rap kabla sokoine hajafa.,nyerere hamjui mkapa..hiyo ni kabla ya vijiji vya ujamaa..
 
Back
Top Bottom