Biashara yangu imedorora sana, hali hii ni kwangu tu au wote?

chiefnyumbanitu

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
906
426
Habari za jioni wana JF? Mimi ni mfanyabiashara, ndogo ndogo aina ya bidhaa ninazo uza ni bedshit, taulo, mapazia, n.k cha kushangaza nilikua nafanya biashara vizuri na kuniingizia kipato kiasi lakini toka ameingia rais mpya hasa wiki hizi mbili biashara imekua ngumu kupita kiasi, mauzo yale ya laki mbili kwa siku yameshuka hadi elfu arobaini, mpaka najiuliza ni mimi tu nliyoanza kuishi kwa shida namna hii au na nyinyi wenzangu?

===========

Similar cases:
Biashara yangu inayumba siku hadi siku.

Sitaki kumtupia lawama anko Magu moja kwa moja ila ukweli hali sio nzuri
Nilikuwa na uwezo wa kulala mpaka na faida ya laki tano kwa siku kwenye kabiashara kangu kakuungaunga ila nowdays nikilala na laki faida nashukuru sana

Mzee achia hela uraiani pleasee tutarudisha watoto kayumba muda si mrefu
 
serio hapo unesea usingefunga, tuendelee kuishi kwa matumain ndugu huenda biashara ikabadilika tu.
 
Mpaka mnyooke! Vijana wa leo mlikuwa mnashinda Kwny Mitandao kumtukana kikwete na kusifia Utawala wa Nyerere tulikuwa tukiwaeleza hali ilivyokuwa wakati wa Mwl hamkuwa mkielewa sasa nashukuru sana Mtoto wa Chato anaturudisha kwny Maisha mliyokuwa mnasifia.
 
na heshima itakuwepo pia
 
ebu tupe sili ya mafanikio
Mkuu cha kwanza hakikisha biashara yako ipo "formalized" sajili katika mamlaka husika kama BRELA na Manispaa/Halmashauri upate leseni ya biashara. Pia hakikisha una TIN ili uwe unalipa kodi, lipa kodi zote kwa wakati.

Baada ya hapo lijue soko lako linahitaji nini... jua wateja wako wanauhitaji wa vitu gani halafu uwape kwa bei nzuri sio bei za kuwanyonya.

Kingine hakikisha bidhaa zako zina ubora mzuri na wekeza katika matangazo inavyostahili.

Kwa ufupi ni hivyo tu mkuu.
 
Mkuu mauzo yake sio mazuri, shilingi elfu 40 akishalipia kodi ndio biashara itaenda vizuri.?

Me ningemshauri abadilishe biashara kwa kuuza bidhaa za vyakula kipindi watu wakiwa na kipato kidogo. Kuliko kuendelea kuuza mashuka na mapazia.
 
Back
Top Bottom